Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Naona hesabu ni janga la kitaifa!





Ongezeko hapa ni shilingi 130,000 (yaani 200,000 ukitoa 70,000). Ongezeko hili ni asilimia 186 (i.e. 185.7 = 130,000x100/70,000). Hiyo 154% sijui mwandishi anaipataje!

Kama lengo ni kusema kiwango kipya ni mara ngapi ya kiwango cha awali....basi angeweza kusema "kiwango kipya cha posho ni zaidi ya mara mbili (au karibia mara tatu) ya kiwango cha awali" na kama ni katika muktadha rasmi sana au ule wa kitaaluma zaidi angesema "kiwango kipya cha posho ni mara 2.86 ya kiwango cha awali"

Hilo lako ndio janga 2.86 ndiyo 286% yangu......nitake radhi ndugu
 
kwa hili chadema in particular viongozi wa kitaifa wanapaswa kuhakikisha kuwa cdm inakuwa na sera itakayowaongoza wabunge wake kupokea posho zinazoendana na hali halisi ya nchi. kinyume chake leo haitaonekana kama ni tatizo lenye athari kubwa lakini,wananchi hasa sisi wanachama na wapenzi wa cdm ambao tumekuwa tukitoa raslimali zetu na kuwezesha cdm kupata hayo mafanikio tutajuwa tumeangushwa kweli kweli
 
Nje ya mapesa kama haya na uwaziri, kugombea UBUNGE kutakuwa rahisi sana nchi hii.
 
umenena vyema mkuu lakini waliziacha hizo posho na wana mikakati gani yakuigomea posho pamoja na kuwa zinaingia benki moja kwa moja
Kwa kuwa ni swala la kisheria na ili sheria ibadilishwe lazima wabunge wengi wawa unge mkono itu ambacho kimekuwa kigumu kiasi kwamba hata ndani ya CDM kuna wanafiki wanazitaka sana hizo posho...Mfano Shibuda yeye alisema anaomba iwe 500,000 kwa siku...lakini Zitto yeye alisema zitakuwa zinatumia kwenyemfuko wa jimbo lake kama sikosei...hivyo wengi wanaiona hii ndiyo njia sahihi kwa sasa kuzitumia kwenye jimbo au wewe unapendekeza nini.....?
 
Kama Zitto angekaa na wabunge wenzake wa CHADEMA na kujadiliana nao kabla ya ku-issue hii statement kingeharibika nini? And what it the point ya ku-mtaja (kumpongeza January Makamba) kwenye hili?
Na kwa nini amsitaje? Kwa mujibu wa taarifa na hoja hii anayoitetea Zitto, ni yeye tu na Januari Magamba ambao wanapinga posho za wabunge na za vikao.

Tatizo letu, ni kuwa hata kama mtu kutoka chama chengine atakuwa amefanya la maana, tunang'ang'ania kuponda tu. Nina hakika kama wataibuka wabunge wa vyama vyengine wakiwemo wa CCM (ingawaje nina wasiwasi kwa njaa zao hawatafanya hivyo) kupinga posho, wengine hume wataanza kufokafoka "wameiba sera zetu". Watanzania, tuangalie maslahi ya nchi na wananchi bila ya kujali nani anayasimamia na kuyatetea. Fair Play kwenye siasa ni kupongeza jema la mpinzani wako.
 
Hilo lako ndio janga 2.86 ndiyo 286% yangu......nitake radhi ndugu
Pole mkuu sikuwa na maana ya kukudhalilisha...kitendo cha wewe kuona tatizo katika hiyo habari peke yake kinaniambia unajua hesabu!

Hata hivyo hoja yangu ni kuwa huwezi kusema kuna ongezeko la 286% (wala 154%)! Ongezeko ni shilingi 130,000 na hiyo ni sawa na asilimia 186 (na sio asilimia 286 wala 154) ya shilingi 70,000.
 
i think uve a personal grudge with zitto. i remember also cdm's chairperson hon mbowe called 4 scrapping of these allowances. why did u only pick on zitto? its high time cdm as a party issue its stand rather than leave this matter to discretion of individual mps of either receiving or rejecting the increase
 
Nimesimama kwenye kauli ya mtoa habari na si vinginevyo....nanukuu "Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154,"......2.86(286%) ndiyo mara tatu yenyewe approximately......huwezi kusema 130,000 ndio ongezeko mara tatu......hakuna janga na mimi ni mtaalamu wa hesabu
 


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
Alipoulizwa kama amechukua posho hiyo ya Sh200,000 alisema hajafanya hivyo kwa sababu hazifuatilii.

"Sijui hata kama zimeanza kulipwa au la kwa sababu huwa sizifuatilii na haka kama suala la posho hilo zilijadiliwa wakati wa vikao vya mwanzo mimi sikuwepo kwa sababu tulikuwa kwenye kesi yetu Arusha na bungeni tulikuja mwishoni wakati wa Muswada wa Katiba," alisema Mbowe..

Duh..Mbowe hajui kwa sababu hajui na kwakuwa hajui, full usaniii...
 
Hii ndio sababu ya watu kutumia pesa nyingi wanapogombea ubunge kwa vile wanauhakika kuwa pesa yao itarudi pia professors na wanataaluma (Phd holders) wengine wanaona hukuna sababu ya kufanyia kazi professions zao wote wanakimbilia siasa na baada ya kukaa huko miaka 5 wakirudi wanakuwa wameshapoteza mengi katika professions zao!
 
Nimesimama kwenye kauli ya mtoa habari na si vinginevyo....nanukuu "Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154,"......2.86(286%) ndiyo mara tatu yenyewe approximately......huwezi kusema 130,000 ndio ongezeko mara tatu......hakuna janga na mimi ni mtaalamu wa hesabu
Hapo kwenye red umepotosha nilichokisema kwenye post yangu..lakini nakusamehe bure tu.
Hata hivyo hoja yangu ni kuwa huwezi kusema kuna ongezeko la 286% (wala 154%)! Ongezeko ni shilingi 130,000 na hiyo ni sawa na asilimia 186 (na sio asilimia 286 wala 154) ya shilingi 70,000.

Hapo kwenye blue nimeshakusoma....tuache tu thread iendelee kwa hoja yake ya msingi.
 
Hii yote inatudhihirishia tuna wanasiasa wa aina gani. Hapa hatuangalii chama, tunaaangalia wanasiasa wetu walivyotutelekeza na kulinda maslahi yao binafsi.
Eti mbunge anadai, ninanukuu "posho imeongezwa kwa sababu mishahara ya wabunge ni midogo sana. Na si wabunge tu, hata watumishi wote wa umma mishahara yao ni midogo. Mimi nilikuwa na kazi yangu na nilikuwa ninapata pesa nzuri tu".
-
Kwa nini wasiwatetee watumishi wa umma ikiwa wanajuwa kuwa mishahara yao midogo, badala yake wanazuwia chao kimya kimya, mtumishi wa umma atajiju.
- Kwa nini kama mbunge aliona mshahara wa bunge ni mdogo, asibakie kwenye kazi yake?
- Kwa nini bunge lisiwaongezee mshahara na kufuta kabisa posho, posho zinazochangia kuliangamiza taifa?

Hawa watu wanatufanya tusiwe na imani nao tena. Tuliwachagua kutetea maslahi ya nchi na wananchi na sio kutetea matumbo yao. Kwa nini Watanzania hatufiki wakati tukasema basi? Basi kudanganywa! Basi ahadi za uongo!

Juzujuzi niliona jinsi wananchi wa mkoa mmoja Amerika ya Kusini (nchi nimesahau), ambapo mgombea kiti cha umeya alikuwa anafanya kila awezalo kuwafuta wagombea wenzake (ikiwemo mauaji). Siku ya kupiga kura, wananchi wa mkoa mzima walisusa kupiga kura, akapiga kura yeye, mkewe na manyang'au wenzake tu. Kwa aibu, aliamua kuwachia ngazi.

Huu ndio uzalendo. Hii ndio jawabu ya wananchi wanaokataa kuburuzwa. Huku ndiko kuwaadhibu viongozi walafi, wezi, wapenda madaraka, wanaojali maslahi yao na kuwawacha wananchi waishi kwa kudra. Watanzania tunaburuzwa, lini tutasema Basi imetosha!?
 
  • Thanks
Reactions: Zed
Zitto's ostentatious nature is a reason behind his low popularity among his Chadema fellow high-profile figures. The guy is too bigheaded and think that he can stand on his own even in sober matters that seem to otherwise disturb Magamba's interests. His move to pressure on the Government to scratch sitting allowance was conspicuously plausible but only lacked his party's blessings before being mooted in the assembly. Unfortunately Zitto ignored the importance of his party's ratification of the issue and decided to take the task by his own, apparently for the sake of winning public approval. His plans have then proved failure and in the end sitting allowances have been increased.

Mwita25, let us agree that Zitto is fighting a noble war for a noble course and is doing so with whole his heart while sensing some of his own are against his stand regarding the ending of the sitting allowances. You know, for instance, Shibuda and some of his likes have categorically opposed the ending of the sitting allowances.

In a party, where uniformity is translated to be collective responsibility, Zitto would be seen as "one man show" but true democracy is more than uniformity or "zidumu fikra za wengi". True democracy entails respecting of the diversity in opinion as long as it is in harmony with the party's manifesto.

Most of the people who criticize Zitto are driven by the hangover of CCM's "zidumu fikra za mwenyekiti". Let us acknowledge that sometime you can not wait for uniformity especially when the readiness isn't there. Let us see Zitto's position as the role of an individual person in fostering true democracy within the party and good governance within the parliament and not the betrayal of common responsibility.
 
Natafuta neno zaidi ya ukichaa lakini silipati: yaani Tumeshindwa kulipa madeni ya wazee, tumeshindwa kutoa mikopo kwenye vyuo vya elimu ya juu, tumeshindwa kuzibiti ongezeko la watoto wa mitaani, tumeshindwa kutoa ajira kwa vijana, Tumeshindwa kuwapatia wanafunzi wa shule za msingi japo mlo mmoja kwa siku, kwa kigezo cha serikali haina fedha….. Hii ni dharau kubwa sana kwa wabunge kuongezewa posho wakati kuna wafanyakaziwa muhimu kuliko wabunge, Walimu, madaktari, police, hawa nao vipi? Acheni kucheza na kodi za Watanzania kwakutaka kuwanyamazisha wabunge. Watanzania Tuungane kwa pamoja katika kupinga unyonyaji huu wa kihuni kabisa
 
Nilitegemea wabunge wa Magwanda wangepinga ongezeko hili la kutisha lakini kimya sioni tofauti kati ya magwanda na Magamba wote sawa.
wapinge mara ngapi? soma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani (ya waziri kivuli wa fedha) then ndio urudi hapa jf
 
Kwa kuwa ni swala la kisheria na ili sheria ibadilishwe lazima wabunge wengi wawa unge mkono itu ambacho kimekuwa kigumu kiasi kwamba hata ndani ya CDM kuna wanafiki wanazitaka sana hizo posho...Mfano Shibuda yeye alisema anaomba iwe 500,000 kwa siku...lakini Zitto yeye alisema zitakuwa zinatumia kwenyemfuko wa jimbo lake kama sikosei...hivyo wengi wanaiona hii ndiyo njia sahihi kwa sasa kuzitumia kwenye jimbo au wewe unapendekeza nini.....?


Acha kupotosha watu kwa ushabiki wako wa kitoto, mh. Selasini yule mp wa CDM alisema bungeni kuwa amegundua posho ni ndogo sana na msimamo wa kupinga posho si wa chama ni wa watu binafsi wenye vyanzo vyao vingine. Kwa taarifa CDM wamesaini hizo posho na tayari wanalamba viwango vipya.

We kalia ushabiki wako wa viongozi na vyama. Hakuna kitu hapo watu wanatetea matumbo yao.
 
Nimesimama kwenye kauli ya mtoa habari na si vinginevyo....nanukuu "Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154,"......2.86(286%) ndiyo mara tatu yenyewe approximately......huwezi kusema 130,000 ndio ongezeko mara tatu......hakuna janga na mimi ni mtaalamu wa hesabu

Kwa simple arithmetics, kama posho ilikuwa 70,000 na imeongezeka hadi 200,000, hesabu zake zinakuwa hivi 70,000 + y% ya 70,000 = 200,000. yaani 70,000 + (y/100)*70,000 = 200,000. Ikikokotoa y utapata ni asilimia 186.713 (186.713%).

Waandishi wetu msome hesabu angalau hata zile nyepesi tu.
 
kwenye hili hakuna chama tawala au cha upinzani........wote wanashabikia kulipora taifa..................huku hakuna vigezo vya kulinganisha mapato ya wabunge na watendaji wengine serikalini..................................kama ni kubana mkanda si tubane wote lakini wabunge hawataki kwa sababu bunge lao wamelitukuza mithali ya Mwenyezi Mungu pale walipoliita bunge tukufu na wao ni waheshimiwa na sisi wengine hatuna hiyo taswira......ni walalahoi ila muhimu sana katika kuhalalisha ulaji wao kila baada ya miaka mitano

Kama vile tunavyotaka katiba mpya ipunguze madaraka ya raisi, napendekeza pia kwenye katiba mpya tupige marufuku kuliita bunge tukufu huku likiwa limejaa waovu. Utukufu ubaki kwa Mungu pekee, hawa jamaa kwakujiona wanakaa na kufanya kazi kwenye bunge tukufu wanajisahau na kudhani nao ni watukufu!!.
 
Sikuhizi najuta kuzaliwa Tanganyika!

Ikumbukwe pia kwamba, wakati watukutu sorry ..watukufu hao (wakiendelea kutunga sheria) kandamizi na zile za manufaa kwao, ni wakwepa kodi nambari 1. Hii inatosha kupima uwezo na nia zao kuwa wachumia tumbo. Huwezi kutunga sheria kubana watu ilihali wewe mwenyewe hutaki kutekeleza sheria husika. Hawa wanao lipwa kiduchu ndiyo walipe kodi...wao na mijidola/mamilioni yao wasikatwe kodi, TRA wanahamasisha kila mtanzania kulipa kodi,...mbona hawasemi wabunge nao walipe kodi kwa fedha yoyote inayolipwa kwao kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine hususani sekta binafsi? Au kwa vile nao ndo....mh!

Lipa kodi upate huduma zaidi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom