Kama wabishi afanyaje? We shibuda atamuelewa kweli zitto?Kama Zitto angekaa na wabunge wenzake wa CHADEMA na kujadiliana nao kabla ya ku-issue hii statement kingeharibika nini? And what it the point ya ku-mtaja (kumpongeza January Makamba) kwenye hili?
Nilitegemea wabunge wa Magwanda wangepinga ongezeko hili la kutisha lakini kimya sioni tofauti kati ya magwanda na Magamba wote sawa.
Nakubaliana na Mh.Zitto sidhani kama kwa nchi yetu kwa hali ilivyo kiuchumi huu ni wakati muaafaka kujipandishia posho "HAYA NI MATUSI KWA WALALAHOI"!!!!Imefanyika kimya kimya kwa sababu wanaelewa kuwa si uungwana na nini itakua reaction ya walalahoi kuhusiana na swala hili,hii inadhihirisha ya kua wao pia wanawasiwasi na aibu kwa uamuzi huu vinginevyo hakua na umuhimu wa usiri kwa jambo hili kama wanafikiri kua ni muhimu.Mbali na kupinga hatua hii,ninamapendekezo ya kua posho za wabunge ziwe zikitolewa kutokana na michango yao katika shughuli za bunge ili kuhepuka ulipwaji wa wabunge ambao wanaenda bungeni kuchapa usingizi kama Mh.Wassira.MUNGU IBARIKI TANZANIA,TUNUSURU NA MAAMUZI YA CHAMA(CCM)NA SERIKALI KWA MAAMUZI YAO YASIOKUA NA MANTIKI.Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao
source: Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu taarifa ya kupandishwa posho za Wabunge kimyakimya - Wavuti
Kama Zitto angekaa na wabunge wenzake wa CHADEMA na kujadiliana nao kabla ya ku-issue hii statement kingeharibika nini? And what it the point ya ku-mtaja (kumpongeza January Makamba) kwenye hili?
Hamna noma 2015 waongeze nafasi za wabunge zifike hadi 10,000 au kila watu 3000 mbunge mmoja alafu unakaa vipindi viwili tu kwa mtindo huo tutakuwa tunagawana keki ya taifa. Maana huko ndiko kwa kuchumia au kutajirikia kwa wabongo.