Posho za Ubunge nazo zifutwe

Niliumia sana kuona na kusikia eti ndio yalikuwa majibu ya Prime Minister......hata mwanangu hawezi kujibu ujin... kama ule, hivi hawa jamaa wanavyojifanya miungu watu tukishawachagua hiyo shilingi kumi utamuombea wapi?? kwanza walio wengi wameshahama hata huko majimboni na wanabiashara zao huko kunakoitwa mjini...utamwona wap[i??? wengine hawapokei hata simu, mbunge wangu mmoja siku moja tulikuwa na miadi kwa ishu fulani (sio ya pesa ila ya kimaendeleo kwa wote) muda ulipofika ili nimkumbushe, naona simu inapokelewa na mtu aliyejitambulisha msaidizio wake.....haya nipe basi simu niongee nae...oooh kalala piga baaadae, napiga tena ooh yupo kwene kikao!! Upuuuzi mtupu

Kwa sababu hiyo ya kwamba wakitoka tu hapo nje wanawasaidia wengine, basi kila raia wa Tanzania apewe posho maana karibu kila mtu anatoa msaada kwa mtu mwingine asiyejiweza. Kuna ombaomba wengi tu njiani ambao wanapata msaada kutoka kwa watu mbalimbali na hakuna mtu anayewapa posho kwa ajili hiyo. Kama mbunge anataka kumsaidia mtu, afanye hivyo kupitia mshahara wake.

Tabia ya wabunge kugawa pesa bila mpango itatujengea utamaduni mbaya wa kuona kama mbunge ni charity organization. Hapo wenye pesa za kugawa tu ndio watakaopata uongozi ktk nchi hii, hili jambo tulikemee. Tufikie viwango vya USA ambako wananchi wanawachangia wagombea wanaowapenda hela ya kampeni, tofauti na hapa kwetu ambapo mgombea anatafuta hela ya kuwapa wapiga kura wake. Mwananchi akimchangia mgombea, atakuwa na ujasiri hata wa kumwajibisha na kumshinikiza atekeleze ahadi zake kuliko aliyepewa T-shirt, kanga na kofia.

Tunawachagua ili watutengenezee mazingira ya sisi wenyewe kujiletea maendeleo. Watunge sera nzuri ili biashara zetu zikue, na watoto wetu wapate huduma nzuri za elimu na afya. Natarajia mbunge apiganie zahanati, hospitali, wauguzi na madaktari na sio agawe hela ya matibabu kwa wapiga kura wake. Suala la posho halina utetezi, linawanufaisha zaidi wakubwa na sio madaktari, manesi (ndo maana wanatudai rushwa), waalimu na kada zingine za chini. Posho ni dhambi, maana posho za wakubwa kwa siku zinazidi mshahara wa mwezi wa mwalimu!

Ndugu zangu wadanganyika waziri mkuu jana kaeleza kuwa posho za wabunge zinaishia nje tu kwa kuwasaidia jamaa zao.
Hivi ni kweli unaweza kuonana na waziri mkuu hivihivi tu kwa kuomba msaada wa pesa kama hujala kirungu cha polisi?

Sasa mzunguko woote huo wa nini? Serikali si iwalipe hao JAMAA moja kwa moja bila kupitia kwa wabunge

Waache tu mwisho wao unakaribia.cha msingi ukiingia utawala wa ukweli tutanue magereza lazima wafirisiwe na kufungwa maisha.
Hatuwezi kuvumilia unyanyasaji kama huu.

pesa za kuhonga watatoa wapi mkiondoa hizo posho?
alikosea angesema hata nyumbani hazifiki zinaishia gest.

Yaani pinda ni boga sijawahi kuona ..anatoa sababu as if ni katibu tarafa..hivi hii nijitu mingine inakuwaje viongozi.?? yaani mawazo utadhani muuza kashata..aghhhh
Maskini Watz, tumepoteza karibia miaka "35" ya uhuru na kibaya zaidi waliotupotezea huo muda are the one deciding on our (precious/hopeless???) destiny!

Hawa ndo viongozi wetu kwa sasa, tusijiulize wamekuaje viongozi maana sote tunajua walichukua form wakagombea, na wengine (hata huyu) wakakosa mpinzani kwenye maeneo yao. Wamepita bila jasho. Tukilalamika haitusaidii, the only available solution ni kuchukua form na kuwachallenge ujinga wao kwenye uchaguzi. Tusitegemee kusemewa na akina Zitto, Mbowe, Lema na Lissu. Tuingie msituni nasi wengine ku avoid ujinga huu, tutakunja mikono na kusubiri kufanyiwa na wengine mpaka lini? Tushiriki mapinduzi ya nchi yetu, tusikae tu kutazama na kulalamika.

Hawa ndo watoto wa wakulima wa kizazi cha tz! Inaingia kwenye akili za waheshimika tu tena za wale wenye Magamba, ya kuwa unaweza kuhalilisha kulipwa posho ili ukasaidiye watu. Kwani hao wanaomba ziondolewe ili zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo, hayo maendeleo ni ya watu wa Msumbiji, Rwanda au Cosovo? Kwamba ni bora ziendelee kulipwa kwa njia ya allowance kwa waheshimika ili baadaye wawasaidiye hao wanaowaomba kuliko kuzipeleka kwenye maendeleo ya wana Msumbiji, Wanyarwada au wa-cosovo. Kazi kweli kweli

CCM na wabunge wao wapo kimaslahi binafsi zaidi sio kwa maslahi ya maskini wa tanzania. hayo yanajidhirisha katika utendaji wao na maneno yao. wewe unafikiri ni kwanini wananunua uongozi na kuchakachua? Jibu ni Moja: Ni ili wale wawe na matumbo makubwa, na mali nyingi waweze kuitwa "mheshimiwa" kokote anakopita. Ikiwezekana hata kuweka hela nyingine nje ya nchi kama Chenge.

watanzania miaka 50 sisiemu kuwa madarakani imekula kwenu, mtakufa na njaa, ujinga, na magonjwa yenu.

Nimeshangaa sana kusikia eti kuondoa posho kwa wabunge ni hoja ya serikali ya ccm kupitia mpango wa maendeleo wa miaka 5.Watanzania ni wepesi kusahau kwani Dr Slaa alishaahidi ktk kampeni.Kuweka suala la posho kwenye mpango huo ni kutekeleza ahadi za Dr Slaa kwa mlango wanyuma.
source:soma mwananchi la 11.9.2010 na habari leo 2.9.2010

Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
Imeandikwa na Levina Kato; Tarehe: 2nd September 2010 @ 07:50 Imesomwa na watu: 1328; Jumla ya maoni: 11

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema, akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atashusha bei ya vifaa vya ujenzi ili kuwezesha wakazi wa Dodoma kujenga nyumba za kisasa na kuondokana na nyumba za tembe walizonazo hivi sasa.

Dk Slaa alitoa ahadi hiyo juzi, alipohutubia wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Winza Kibakwe wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.

Katika hotuba yake hiyo alisema atapunguza gharama ya saruji, mabati na bidhaa nyingine zinazohusika katika ujenzi ili kuwezesha watu wengi kuishi katika nyumba bora.

Akitania, Dk Slaa aliwaambia wananchi hao kuwa, rubani wake alipata shida kukiona kijiji hicho kwa sababu nyumba zote zimeezekwa kwa tope - tembe.

“ Imenichukua muda mrefu angani wakati rubani wangu alipokuwa akijaribu kutafuta kijiji chenu, hatukuona nyumba zenu,” alisema Dk Slaa ambaye alifika kijijini hapo kwa helikopta.

Mwanasiasa huyo alisema, hawadhalilishi wakazi wa Kibakwe ila anawaeleza ukweli, kwamba wanapaswa kuishi katika nyumba bora.

Alisema, akichaguliwa kuwa Rais, Serikali yake itapunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika vifaa vya ujenzi hasa vinavyotengenezwa nchini, kama vile saruji, ili kuwezesha masikini kujenga nyumba bora.

Akitolea mfano, Slaa aliiambia hadhara hiyo kuwa serikali yake itapunguza marupurupu kwa wabunge na kuelekeza fedha hizo katika mfuko wa miradi ya maendeleo.

“Ni dhihaka kwa wawakilishi wenu (wabunge) kupata fedha nyingi kutokana na vikao vya Bunge, wakati ninyi mnalala katika nyumba za tembe,” alisema wakati akielezea nini atawafanyia Watanzania.

Katika hadhara hiyo pia Dk Slaa alimtambulisha mgombea ubunge Benson Kigaila ambaye aliahidi kujenga shule katika jimbo hilo, ili watoto wengi wa masikini wapate elimu, hasa wasichana.

Lakini akiwa Kiteto, Manyara jana, Dk Slaa alitoa ahadi nyingine kuhusu vifaa hivyo vya ujenzi, akisema akiingia madarakani atavifutia kodi zote zinazovigusa.

Cha ajabu na kweli wanadai eti mpango wa maendeleo wa JK ndo umependekeza kuondoa posho na wameujadiri na kuupitisha,lakini CDM wakisema posho ziondolewe ndo kwanza CCM wanakuwa wakali...

sasa unajiuliza kama kweli mpango wenu ndo uliasisi kuondolewa posho na mkaupitisha inakuwaje matendo sasa yanauma?ama walifanya kisiasa bila kujua itakula kwao....they are so funny!

Chukua Chako Mapema
kwa maana halisi ya abreviation ya chama chao ipo wazi kuwa wapo kimaslahi zaidi hawazi kuacha posho

swala la posho ni hoja ya msingi...tatizo namna ya kulijadili...swala la kisheria haalimaliziki kisiasa... sote tunafahamu posho zipo kisheria...kamwe hazitotoka kwa porojo za majukwaani na kelele za magezetini....CCM hawawezi kupeleka mswada wa kubadili sheria hiyo inayohalalisha wizi kupitia poshoo.... ni kazi yetu wanamapindizi tukiongozwa na Chadema.... ZIto na CHADEMA yote kwa ujumla WAPELEKE MSWADA Binafsi hii ndo suluhu ya swala hiilii...... umaarufu wa kijinga huku bado mtanzania wa kawaida anaumiaaa tumechokaa.

jamani hizi sasa za kitoto tutacha lini .FB ni mtandao wa kisomi sio wa sias tujadili mambo kisomi kwas mstakabali wa Taifa..... Swala la Hoja ya Nani sio la msingi kwetu... SWALA MSINGI POSOO ZIONDELEWEW EWE HOJA YA CHADEMA AU CCM. tuache sias nchi haijengwii kwa porojo hizii.....

watanzania ni wtu wa kuongea sana na kuropoka ila sio watendaji..... hoja posho itazungumza sana m, magazeti yatauza sana laikini kwa sela hizi za U ccm na UCHADEMA.... hazifutwi n'go. let be realistic on matter that touches the future of our nation

sUALA LA POSHO KWA WATUMISHI WA UMMA NAONA linaingia katika sura mpya kwa mh waziri mkuu kuamua kutukana watanzania waziwazi. Mheshimiwa katetea hili suala ila kwangu mie namna anavojitetea ni katika njia ya (1) kusisitiza wabunge waendelee kupewa posho (2) watumishi wengine wa umma wanyimwe.

Nasema hivi kwa vile mheshimiwa katamka kuwa upande wa waheshimiwa wabunge posho zao zinaishia pale nje ya mjengo kwa vile kuna wapiga kura wanawasubiri kuomba.
Kwa hio basi, sie tunakubali mheshimiwa kuwa ni ombaomba sababu hata serikali kuu ni ombaomba kupita zote duniani. Lakinbi ukumbuke umasikini huu unachangiwa kwa kiasi kikubwa na (1)mikakati mibovu ya kuendeleza walio wengi hasa vijijini (2) mikataba mibovu (3) ufisadi uliotamalaki serikalini.
Sasa kosa ni la nani? kwa hio unatupigia tarumbeta kuwa tuje kuomba dodoma?
Be a gentleman please. Wewe kwa nafasi yako ni mtendaji, ingawa pia ni mwanasiasa
NAJUA UMETUCHOKA WATANZANIA, ILA TUTAPATA TU MKOMBOZI 2015
NA WEWE SI MTOTO WA MKULIMA MANAKE SIO OMBAOMBA

Alisifiwa sana kwa busara na uchapa kazi kipindi anaingia kwenye uwaziri mkuu.Kumbe aisifuye mvua imenyea.Sasa mizengo pinda anawanyea watanzania.

Magazeti mengi ya leo kama sio yote yamepambwa na headlines zinazomhusu Mzee Pinda (PM) akitetea ulipwaji wa posho kwa watumishi wa umma kwamba zinalipwa kwa mujibu wa sheria na zingine zipo kwenye katiba ya nchi. Mzee huyo aliyewahi kujiita mtoto wa mkulima (????) amekwenda mbele zaidi kama ilivyo kwa watetezi wengine wa "wizi wa mchana kweupe" wenye jina la posho kwamba haziepukikii (ni inevitable kwa kithungu) kitu ambacho ninakipinga kwa nguvu zangu zote. Double payment au posho haziwezi kuwekwa mzani mmoja na chakula, maji, hewa na vingine ambavyo bila hivyo hatuwezi kuishi.Mbona watanzania wengine wanaishi kwa 150000 kwa mwezi? Wakati ninajiandaa kumjibu kwa barua ndefu nimeona nipost thread hii japo kupunguza hasira zangu kidogo zilizosababishwa na matamshi yaliyokosa uzalendo ya Mzee Pinda. Mzee Pinda, kumbe pale sheria inapowafavour mnapenda kuirefer sheria lakin pale inapokwenda kinyume na matakwa yenu mnaipindisha mtakavyo-mfano mmojawapo ni suala la EPA. Sheria haisemi mwizi akiiba aombwe arudishe then yaishe lakini bila aibu hivi ndivyo serikali yako ilivyofanya.

Nina maswali yafuatayo naomba Mzee Pinda anijibu. Hivi ni sahihi kwako kwa mbunge anayelipwa milioni 7 za mshahara kupewa posho on top kwa kazi hiyo hiyo moja? Hii kama ni sheria basi ni ya kidharimu kupita maelezo na inapaswa kufutwa haraka sana unless sheria zetu zinatungwa na Mungu. Hivi ni sahihi kwenu ninyi ambao ni watanzania kuliko wengine kuendelea kulipwa malipo mara 2 wakati:

1. Kuna mama mmoja mjamzito anafariki kila baada ya saa moja kwa magonjwa yanayoepukika?
2. Mwalimu anayefundisha katika mazingira magumu aendelee kulipwa laki moja na nusu kwa mwezi mzima?
3.Watoto wetu waendelee kukaa sakafuni wanaposoma darasani? Kuna primary iko dar std 1-6 wanakaa chini std 7 pekee wana madawati
4. Akina mama wanaosubiri kujifungua hospital ya Bombo Tanga, Temeke na kingineko waendelee kulala watatu kwenye kitanda kimoja?
5.Mkulima wa mahindi wa Mpanda aendelee kudhulumiwa na walanguzi kwa ukosefu wa barabara?
6.Wagonjwa wetu waendelee kukosa dawa kwenye mahospitali?
7. Orodha ya matatizo ni ndefu sana sitaweza kuimaliza

Mzee Pinda wabunge na watumishi wengine ni watanzania kama sisi. Sioni sababu ni kwanini wao waishi kama wako peponi na sisi wengine tuendelee kuteseka kama tuko jehenamu. Posho zinaweza kuwa zipo kisheria sawa lakini haziendani na hali halisi ya uchumi wetu na maisha wanaoshi majority ya tax payers wetu. Kwa level yako unapaswa kwenda beyond sheria inasemaje unless utuambie wewe ni PM wa wabunge na watumishi wengine wa serikali.

Back
Top Bottom