Posho zote pamoja na ruzuku kwa vyama vya siasa ni wizi na ujambazi usiovumilika. Tunaomba posho na ruzuku vifutwe mara moja.
1.Mbunge ama mfanyakazi atayelalamika kufutwa kwa posho ajiwajibishe mwenyewe kwa kukubali kuwaachia wengine watao kubali fanya kazi chini ya mshahara husika.
2. Chama cha siasa kitakacholalamika kufutwa kwa ruzuku ama kushindwa kujiendesha kwa michango ya wanachama wake, ina maana chama hicho hakikubaliki, ni halali yake kijifie, kwanini kuendesha chama kwa jasho la watu wengine ambao hawana vyama? Hii ni sawa na mahakama ya kadhi ama baraza la maaskofu kuendeshwa na kodi ya wananchi.
Nakumbuka tulipokuwa kule (kabla ya uchaguzi wa 2005) BCS......nilisema hili jambo...........ee bana eee baadhi ya watu walipinga sana.........sababu kubwa ni eti CCM itakuwa na advantage zaidi ya vyama vingine......nashukuru sana Mkuu kwa kuileta tena hii hoja..........