Posho, sheria au Haki

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,379
3,826
Nilifurahishwa na makala ya Mabala gazeti laMwananchi la Jumapili. Mojawapo yahoja alizotoa ni kuhusu posho wanazopewa waheshimiwa je katika hali waloyonayo Watanzania tuendelee kutoa posho kwa vile sheria ipo au tuzingatie iwapo ni haki yao wapate?
 
Sasa ndugu Mzamifu wewe unasemaje?
Toa maoni yako na unachosimamia wewe kwa upande wako!
Kuweka alichosema Mabala bila kucomment ni kutochanganya na zako!

Sheria ni kweli ipo, lakini 80% YA wATANZANIA WANAISHI VIJIJINI, AMBAPO WANAISHI chini ya kipato cha 1US$.
kWAHIVO ni upumbafu sana kugawana posho za aina hiyo kibinafsi!
 
Nilifurahishwa na makala ya Mabala gazeti laMwananchi la Jumapili. Mojawapo yahoja alizotoa ni kuhusu posho wanazopewa waheshimiwa je katika hali waloyonayo Watanzania tuendelee kutoa posho kwa vile sheria ipo au tuzingatie iwapo ni haki yao wapate?

Kama posho hizo zimewekwa kisheria basi ni wajibu wao kuzipokea na ni haki yao kuzitumia.
 
Sasa ndugu Mzamifu wewe unasemaje?Toa maoni yako na unachosimamia wewe kwa upande wako!Kuweka alichosema Mabala bila kucomment ni kutochanganya na zako!Sheria ni kweli ipo, lakini 80% YA wATANZANIA WANAISHI VIJIJINI, AMBAPO WANAISHI chini ya kipato cha 1US$.kWAHIVO ni upumbafu sana kugawana posho za aina hiyo kibinafsi!
Samahani sikuwa hewani kitambo kidogo. Nionavyo mimi posho hizi zinawanyonya wananchi kwa vile zingeweza kutuiwa kwa manufaa mengine kama afya, elimu, umeme nk.
 
Kama posho hizo zimewekwa kisheria basi ni wajibu wao kuzipokea na ni haki yao kuzitumia.
Sawa lakini sheria ikionekana inawapendelea watu wachache huku wengine wanaumia basi iachwe tu? kisingizio eti baadhi ya waheshimiwa wanazitumia hizo posho kuwasaidia watu wao kiachwe. inawezekanaje mtu mmoja akawasaidia watu wa jimbo zima kwa posho hizo?
 
Back
Top Bottom