Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

0006

Haya ndio maswala ya kuangalia na pengine kuchunguzwa na Takukuru...

Hapo juu hizo hela za matumizi mbali mbali ni milioni 6.9 ambayo pia wanadai ni mshahara wa wahitimu 22 wakijumlishwa. Bado watu wana shangaa kwa nini wana taaluma wote wana kimbilia siasa?
 
Makaayamawe,
Mkuu wangu nimeandika hivyo kwa kuelewa kwamba kuchukua Posho mara mbili sio Rushwa.. sasa ikiwa Takukuru wanaweza ingilia hizi posho basi yapo mengine makubwa zaidi ambayo mimi na wewe tungependa wayachunguze. Yawezekana sii Rushwa kwa mtazamo wako lakini yote ni Ubadhirifu wa fedha za serikali..kifungu cha sheria kipo!

Mkandara,
  1. Mkuu, ubadhirifu wa matumizi ni pale pesa inapotumika bila kuwa imeidhinishwa kisheria. Hizo posho zimesainiwa na Raisi mwenyewe na kupitishwa kwenye bajeti na hivyo sio RUSHWA. TAKUKURU hawana uwezo kisheria kuzichunguza.
  2. Kama wananchi hatuzipendi hizi posho, tunatakiwa kuingia mitaani kupambana na Kikwete kwa kuziidhinisha.
  3. Hili la TAKUKURU kuwachunguza wabunge ni mbinu tu ya kuwanyamazisha.
 
Je kuna sheria yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu kwa mhusika kulipwa posho mara mbili kwa shughuli moja ile ile? Kwa hiyo Mazee Makaayamawe unataka kutwambia kuwa Rais aliidhinisha kwa wabunge na viongozi wengine kulipwa posho mara mbili kwa shughuli moja? Naomba ufafanuzi kwa hili na ikiwezekana uthibitisho, kwa sababu huo utakuwa ni ufujaji na ufisadi wa kodi za wananchi.
 
Geeque,
Mara nyingi sheria hutungwa kukataza kitu haramu na sii kuruhusu vitu ambavyo vinafanyika siku zote labda tu tafsiri ya ruksa yenyewe iwe kwa kipimo fulani otherwise ruksa ni ruksa..Navyofahamu mimi posho mbili au mishahara miwili sio deal tena toka kifo cha Azimio la Arusha, Ikiwa mishahara miwili imeruhusiwa kwa kazi moja iweje swala la posho liwe deal..Daktari wa serikali anayetibu bure Muhimbili na kupewa mshahara humwoingoza mgonjwa ktk hospital yake na huko hulipwa tena kwa maradhi yale yale.
Mkuu wangu mbunge ni mwakilisho wa wilaya mnapomkabidhi kazi nyingine nje ya kazi alotumwa bungeni sioni kosa la kulipwa ziada hata kama yupo na analipwa ktk kikao cha Bunge.
Kama tunataka haki Basi Miiko na maadili ya viongozi yarudishwe kama yalivyokuwa wakati wa Azimio la Arusha.. kila kitu kilikuwa Loud and Clear.
 
Haya tunayoyaona sasa yanadhihirisha kwamba nchi yetu kwa sasa haina uongozi, ndiyo maana kila mmoja anakuja na maamuzi yake na tena hayafuati sheria, bali maamuzi binafsi (discretion).

Swala la wabunge kulipwa posho mara 2 limekufa natural death, TAKUKURU hawawezi kufanya lolote, walikuwa wanataka kutishia mtu mzima nyau. Serikali itaufyata kwa kuwa na wao wana madhambi yao, so wameamua kuua kesi zote kwa kututoa kafara sisi wananchi.

Spika anajua wazi kwamba swala hilo likivaliwa njuga, hata mawaziri nao wanahusika kwa kuwa wamekuwa wakilipwa posho mara 2 wanapokuwa kwenye safari zao za kikazi ndani ya nchi na bado wenyeji wao (taasisi husika) zimekuwa zikigharimia mpaka malazi na chakula cha mawaziri.

Huu ujinga na upuuzi vitaisha pale ambapo tutakapokuwa na katiba ambayo itakuwa na nguvu ya kusimamia haki kwa wananchi pasipo kuwapendelea walio madarakani. Katiba ya sasa inawapendelea walio madarakani na ndio maana wanajiamulia wao wanavyopenda, maana wanajua hatuwezi kuwafanya kitu.

Kama katiba yetu ingekuwa inatoa uhuru na inahakikisha kwamba Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU, na DPP wanawajibika ipasavyo na kunakuwa na mechanism ya kuwashughulikia ikitokea kwamba wameshindwa kuwajibika, wala tusingekuwa tunaongelea huu ujinga ambao uko obvious kwamba ni makosa, lakini walio madarakani wanaonyeshana ubabe (fahari wapiganapo zinazoumia ni nyasi), tunaoumia ni sisi walipa kodi ambao tunachangia hizo posho na ilhali mishahara yetu ni ya kubahatisha.

Ili kupata katiba mpya, mabadiliko yanatakiwa kuanzia kwenye Bunge. Watanzania (wananchi wa kawaida) hatuna ubavu wa kudai katiba mpya na vyama vya upinzani havina ubavu wa kuilazimisha serikali ilete katiba mpya. Dawa na kuongeza wabunge wa upinzani, ambao watadai katiba mpya kwa niaba ya wananchi. Kila siku serikali iliyo madarakani wanasema sheria ni mbovu lakini ukiwaambia tuweke katiba mpya wanasema hakuna uhitaji wa katiba mpya, bali ni marekebisho madogo tu. Matokeo yake ndo huu ujinga, watu wanachemka na hatuna namna ya kumshughulikia tunabaki kulalamika tu.
 
- Hivi gazeti la Rai, linamilikiwa na nani? Na ni nini interest ya huyo mmiliki on this ishu ambayo ni pure waste of our time, kwani wabunge wanapochukua hizo posho si wanasaini somwhere panapoonyesha kwamba wamechukua posho mbili, sasa kama Takukuru wanao ushahidi haya makelele ni ya nini?

- Mkuu Makaayamawe, uko right on the money ukubwa wa posho na marupu rupu ya wabunge sio kosa la wabunge, ni kosa la sheria ndio maana Obama anawabana ma-CEO wale tu waliochukua hela za serikali, wengine hawagusi kwa sababu sheria iko wazi kwamba wako sawa nayo, mimi ningetegemea by now tuanze kuona ushahidi wa wazi unaoonyesha saini za wabunge katika kuchukua posho mbili, huku wakiwa wanajua kwamba wanavunja sheria, hao wakishikwa peleka wote Segerea, tutaenda kuwachambua huko nani ni nani,

- Lakini kama hakuna ushahidi unaosimama wenyewe, basi it is about time sasa tukarudi kwenye vyeti feki vya viongozi wetu!

Respect.

FMEs!
 
Yaani siasa za bongo raha kweli. Mafisadi kila kona, wengine wanawashambulia wenzao, wakati huhuo wenyewe wanafisadi kwa ruksa ya walalahoi. Tutafika kweli?
 
Lowasa katika hotuba yake ya mwisho pale bungeni kabla ya kujiuzulu alisema wazi kwamba hakuna mtu msafi ndani ya serikali kama kila mtu akichunguzwa.
 
Mkandara,
  1. Mkuu, ubadhirifu wa matumizi ni pale pesa inapotumika bila kuwa imeidhinishwa kisheria. Hizo posho zimesainiwa na Raisi mwenyewe na kupitishwa kwenye bajeti na hivyo sio RUSHWA. TAKUKURU hawana uwezo kisheria kuzichunguza.
  2. Kama wananchi hatuzipendi hizi posho, tunatakiwa kuingia mitaani kupambana na Kikwete kwa kuziidhinisha.
  3. Hili la TAKUKURU kuwachunguza wabunge ni mbinu tu ya kuwanyamazisha.
Hapana mkuu wangu ubadhirifu wa fedha za serikali ni pamoja na natumizi kama haya, kwa mfano, ule ununuzi wa Rada pamoja na kwamba ulipitishwa lakini ulikuwa kinyume kabisa.. Tunaibiwa kwa makatasi.
Ikiwa kiongozi yeyote atapitisha malipo makubwa kuliko thamani ya kitu ama huduma, hiyo pia ni ubadhirifu wa fedha za serikali.. Tunayaona Bungeni, Jeshini, Magereza, Wizarani na idara zote za serikali jambo ambalo huwezi likuta ktk mashirika binafsi. trust me kazi wanayoifanya wabunge haina thamani sawa na malipo wanayopewa hata kidogo - Ni Ubadhrifu!
 
Halafu na hawa mnategemea wapitishe sheria zinazolinda maslahi ya Watanzania?
 
Nukuu za hekima za "Mheshimiwa Spika":

  • Endapo kuna watu wanawaonea wivu kwa kuwa wanafaidi, wasubiri mwakani ili wajiandae kuingia katika ulingo wa siasa kuwania nafasi hizo.

  • Mchana kutakuwa na semina ya Muswada wa Sheria ya Watoto na kusisitiza kuwa katika semina hiyo, "itifaki" imezingatiwa.

  • Ni jambo la kiungwana kabisa kumkirimu mgeni kwa chai na si jambo geni hata kidogo na posho hizo hawapewi wabunge tu hata wenzetu waandishi wa habari wanapata,alisema.

  • Aliwataka wanaopaza sauti kuhusu wabunge kulipwa posho hizo wakati ofisi ya Bunge ilishawalipa kwa kuwepo kwao bungeni kuacha malumbano hayo badala yake washughulikie masuala ya msingi likiwamo la "Kilimo kwanza"
.................................Kwa maneno mengine anamaanisha "Mwenye Wivu Ajinyonge"...............
 
Na tukisema chama chao ni chama cha mafisadi watu oohh! Haitakuwa ajabu wa Epa,Richmond na whatever so called... wakaja na kauli kama hizi.Haina tofauti na wananchi lazima wale nyasi ila ndege ya prezda inunuliwe.Guys watch out your midomo!
 
Hii nchi imejaa mafisadi, cha kutisha ni kwamba baadhi ya hao mafisadi wanajiita wapiga vita ufisadi.

Ni wazi kwamba na wao wangekuwa na mbinu za kuchukua EPA wangechukua tu, kwa kuwa hawana sasa wanatuibia kwa posho na double payments!!!
 
Hivi itakuwa kosa tukiwaita "WAHISHIWA" badala ya kuwaita "waheshimiwa"? Manake naona wameishiwa busara.

Mhishiwa so and so..:D
Mhishiwa so and so...
:D
 
Halafu na hawa mnategemea wapitishe sheria zinazolinda maslahi ya Watanzania?

Hawawezi kabisa kuzipitisha. Hawa ni wezi wakubwa. Tena ni bora hivyo wako Bungeni hawana nafasi ya kufanya wizi mkubwa. Wakiingia serikalini hawa manyang'au itakuwa hatari kweli kweli. Afadhali wenzao walikuwa wakiiba kwa kujificha. Hawa wanafanya daylight robbery.

Fedha husika ni za Serikali, kwa hiyo hatua ya kwanza ya kuzuia wizi huu ni Waziri Mkuu kutoa Agizo la kukataza Wizara na Taasisi zake zote kutoa fedha hizo. Hayo mengine ya uchunguzi etc yafuate baadae.

Kuonyesha wizi na uzembe wa wabunge hawa (nimeondowa waheshimiwa), posho hii ikiondolewa tu hata hivyo vikao vya wizara na taasisi watakuwa hawahudhurii ipasavyo. Badala yake watazua safari nyingi za kutembelea makampuni binafsi ambayo yao yatatoa hongo ili wawatetee Bungeni. You cannot beat these people.
 
Zitto akwama bungeni

[Source Tanzania Daima]

na Sauli Giliard, Dodoma

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), jana alikumbana na wakati mgumu baada ya wabunge kugoma kuunga mkono hoja yake ya kutaka kuwazuia wabunge kuwamo katika bodi za mashirika ya umma.

Zitto alitaka yafanyike marekebisho katika muswada wa korosho uliowasilishwa jana bungeni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, ambapo alibainisha kuwa ni vema kipengele cha kuwazuia wabunge kikajumuishwa.

Alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wanasiasa kutoingizwa katika bodi za mashirika ya umma, ikiwamo korosho, ili kuepusha migongano ya kimasilahi.

Pendekezo hilo aliliwasilisha jana asubuhi, lakini jioni wakati wa uhitimishaji, wabunge hawakumuunga mkono, hali iliyofanya kutupwa kwa marekebisho hayo.

Katika utetezi wa kutaka kukubalika kwa hoja yake, Zitto alibainisha kuwa katika Bunge kuna wabunge 322, lakini waliomo kwenye mashirika hayo ni 35 tu, ambao wengine wamekuwa wakizunguka katika bodi zaidi ya moja.

Alisema madhara ya wanasiasa kuwamo katika bodi hizo kuna sababisha mgongano wa kimasilahi wakati wanapofanya maamuzi kadhaa katika mashirika ya umma, jambo ambalo kimsingi linaathiri ufanisi wa chombo husika.

“Kuna umuhimu wa wanasiasa kuondolewa katika bodi hizi. Huwa tunapopita katika mashirika ya umma tunapata matatizo makubwa kwa Kamati yetu ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Mashirika ya Umma,” alilieleza Bunge.

Zitto alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utoah, alishawahi kupendekeza jambo hilo ili kuleta ufanisi katika mashirika hayo.

“Hili jambo si geni, ni ukweli usiopingika kuwa kuwapo kwa wabunge katika bodi za mashirika ya umma kwa namna moja au nyingine kunashusha uwajibikaji wa mashirika hayo,” alisema Zitto.

Pamoja na utetezi huo, bado Zitto hakuweza kupata uungwaji mkono wa wabunge.

Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai, ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho cha jioni, alimtaka Zitto akubaliane na matokeo, kwa kuwa hoja yake haikuungwa mkono na wabunge.

“Mheshimiwa Zitto, ulitoa hoja ya kuwapo kwa marekebisho katika muswada wa korosho lakini kutokana na kutoungwa mkono na wabunge, pendekezo hilo haliwezi kuwa halali,” alisema Ndugai.

Awali, Zitto alibainisha kuwa anashangazwa na muswada huo mpya kutoweka bayana kuhusu suala hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisababisha mkanganyiko wa utendaji kazi, hasa unapofika wakati wa kufanya maamuzi yenye kuiwajibisha bodi ya shirika Fulani.

muswada huo utakaounda bodi ya korosho na kufuta ile ya mwaka 1984, alipingana na kipengele kinacholilinda soko badala ya mkulima wa korosho.

Katika hilo, alibainisha kwamba, soko huwa linajilinda lenyewe na kushauri wakulima walindwe kwa kuwa katika soko, kuna wafanyabiashara wakubwa wenye nguvu za kuwanyonya wakulima wadogo.

Zitto alisema, licha ya takwimu kuonyesha kwamba, msimu uliopita pekee, korosho za thamani ya dola milioni 40 ziliuzwa nje na kuchangia pato kubwa la taifa, bado sekta hiyo haipewi kipaumbele kama zilivyo sekta nyingine na kutolea mfano ile ya madini.

Naye Mbunge wa Mtwara, Mohamed Sinai alitaka afya za wakulima zipewe kipaumbele katika sheria hiyo mpya inayotarajiwa kutungwa endapo mswada utapita, ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha wenye viwanda vya kubangua korosho kuwapima mara kwa mara wafanyakazi wao.

Alisema, moshi unaotoka katika viwanda huwaathiri wafanyakazi hao mapafu huku mafuta yakiwaharibu ngozi licha ya kupewa ujira mdogo usioendana na kazi nzito wanayoifanya.

“Moshi wa korosho unawaharibu mapafu, mafuta yanaharibu ngozi yao, wafanyakazi wanatakiwa wapimwe afya zao,” alisisitiza mbunge huyo.

MY TAKE:

Ni obvious kuwa First priority ya Wabunge wetu wa CCM ni ulaji na sio kuwatetea wapiga kura waliowapeleka pale. Kila mwaka posho za waheshimiwa wetu zinaongezeka bila kujali hali ya mwanachi wa kawaida ikoje. Mimi naimba kila siku kwamba dawa yake ni kuwa na chama cha upinzani chenye nguvu at any cost bungeni. Nachoshwa sana na huu upumbavu wa kutuvuga kwamba wewe ni mpambanaji unakosoa madudu ya serikali kwelikweli, unapiga kelele kwenye luninga mpaka mishipa inakutoka halafu unamalizia kwa kuunga mkono mia kwa mia hoja ya kijinga. Watanzania amkeni. "Sidanganyiki" ndio iwe kauli yetu 2010.
.
 
Kuna mmoja kasema Wabunge wetu hawana busara. Busara ya kufanya nini? Kama mtu alikwenda Bungeni kwa lengo la kuchota, na sasa anachota kwa sana, amekosaje busara? Aliyekosa busara ni mwananchi anayenyonywa kishenzi na huku anabaki kuimba "kidumu chama cha mapinduzi!"

Asiye na busara ni myonyaji ama ni yule anayekubali kunyonywa?

Wenzetu Waingereza wanaita kudai malipo na kulipwa zaidi ya mara moja kwa kitu kile kile Double dipping. Ni kama mtu anafikisha lori la kokoto nyumbani kwako na akadai malipo kwa mkeo, kisha akakukuta njiani akakulipisha tena. Hiki kitu ni OK kwa Sita wetu!

Kukilacho kii nguoni mwako. Wanyonyaji namba wani wa Watanzania ni viongozi wao. Nasikia kuna viongozi wana ofisi Dar na Dodoma, na wakienda huku wanadai per diem kule!

Sita anasema tunaonea mirija yao wivu! Inatuumiza jamani, sio wivu! Mtanyonya mpaka tone la mwisho? Si mtabaki na mizoga? Au hata mizoga kwenu ni nyonya tu!
 
Naye Mbunge wa Mtwara, Mohamed Sinai alitaka afya za wakulima zipewe kipaumbele katika sheria hiyo mpya inayotarajiwa kutungwa endapo mswada utapita, ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha wenye viwanda vya kubangua korosho kuwapima mara kwa mara wafanyakazi wao.

Alisema, moshi unaotoka katika viwanda huwaathiri wafanyakazi hao mapafu huku mafuta yakiwaharibu ngozi licha ya kupewa ujira mdogo usioendana na kazi nzito wanayoifanya.

“Moshi wa korosho unawaharibu mapafu, mafuta yanaharibu ngozi yao, wafanyakazi wanatakiwa wapimwe afya zao,” alisisitiza mbunge huyo.

Waangalieni aina ya wawakilishi tulio nao! Badala ya kudai mazingira yatakayozuia hayo madhara kuwapata wafanyakazi yeye anadai ati wapimwe afya zao!

Zitto ana kazi kweli.

Amandla.....
 
Back
Top Bottom