Posho haiwezi kunitemesha ubunge-Mrema

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Mrema1(17).jpg

Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema



Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema, amewaponda wabunge wanaotaka kujiuzulu ubunge kutokana na posho kuwa ndogo, kwa kuwaeleza kwamba wasitawaliwe na tamaa ya fedha kwa sababu ubunge hauhitaji mpaka uwe

milionea ndipo uweze kuwatumikia wananchi waliokuchagua.
Mrema alisema hawezi kujiuzulu ubunge eti kwa sababu posho ni ndogo bungeni kwani wananchi walimchagua ili

awatumikie kuwaletea maendeleo na siyo kwenda kufuata posho.
“Mimi siachii ngazi ng’o, fedha siyo ishu kwangu nawatahadharisha tunaolipwa posho na malupulupu tusitawaliwe na tama ya fedha wananchi wanatuamini hivyo tuwatumikie,” alisema Mrema.

Mrema alisema ni kweli posho ni ndogo kwa wabunge, lakini hata hizo kidogo zinazotolewa inategemeana na huyo anayepewa anazitumia vipi maana ukizidisha matanuzi haziwezi kutosha na siku zote fedha huwa hazitoshi hata kama

kila mbunge angelipwa posho ya Sh. milioni 10.
Mrema aliongeza kuwa kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwamba kuna wabunge wanataka kujiuzulu ubunge kwa sababu posho ni ndogo, hayo ni maoni yake.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom