POSHO: Bunge lamjibu Zitto Kabwe; atoa msimamo wake

Kabla hamjaenda mbali na mjadala hii hapa chini ndiyo barua ya zitto sasa cha muhimu kwa sasa ni ku-assess kama hayo majibu ya bunge yanakidhi maombi ya Zitto. Kwa maoni yangu bunge limeplay politics at its best, maana wao kama waajiri hawampi zitto hizo posho mikonomi sasa kuna ugumu gani kuzideposit huko KDI anakotaka. After all hii haitainvolve any bunge official to do it manually. Kwamba et labda spika itabidi akapange foleni benki....... inasikitisha kuona bunge linashindwa kwa statement yako maana yake ni kwamba zitto hajakataa posho ila anataka posho yake yeye ipelekwe KDI na si kwamba anataka iwanufaishe watz wote. Mawazo yangu hayo jamani. Hapa naona umimi zaidi ya kingine.
 
ninawasiwasi kuhusu baadhi ya wabunge wa chadema,as far as suala zima la teamwork linavyohusika. kama tunavyowasikia wenyewe kuhusu suala kufutwa posho inaonekana ni suala la kichama na kambi yao nzima ya upinzani. sasa iweje mtu mmoja aanze ku execute mpango mzima wa chama peke yake? ndo maana zinajengeka hisia za ubinafsi ndani ya chama na hata uzito wa issue yenyewe unapungua inapapelekwa hoja na mtu mmoja mmoja tofauti na ambavyo ingepelekwa na kambi ya upinzani kama hoja ya pamoja. 2. tukiangalia majibu ya ofisi ya bunge, kwamba utaratibu uliopo sasa ni" kumlipa mbunge moja kwa moja" hatuoni kwamba kuna umuhimu wa kupeleka hoja kwanza bungeni au popote panapohusika ili kuubadili kwanza utaratibu huo ili hoja ya kuzifuta iweze kupata nguvu?
Kabla ya kuoga maji ya mtoni unajaribu kina chake kwanza! Hongera sana Zitto/cdm!
 
Naunga mkono hoja ya hoyce. Mpango huu ungekuwa na maana na uzito wa kipekee kama kwa mfano wabunge wote wa upinzani au hata CHADEMA peke yao wangeandika barua ya pamoja kukataa posho hizo na kutoa maelekezo ya wapi zipelekwe. Hata hivyo, bado hawachelewa. Ni opportunity nyingine kwa kambi ya upinzani kuwin support ya umma kwa kweli wapo serious.

Haiwezekani kwa wabunge wote wa chadema kuandika barua moja ya kuwawakilisha kwa sababu mkataba uliopo ni kati ya bunge na mbunge mmoja mmoja. Hivyo ili hili swala litekelezeke kila mbunge anatakiwa aandike barua yake binafsi ya kukata posho yake kama alivyofanya zitto.
 
Haiwezekani kwa wabunge wote wa chadema kuandika barua moja ya kuwawakilisha kwa sababu mkataba uliopo ni kati ya bunge na mbunge mmoja mmoja. Hivyo ili hili swala litekelezeke kila mbunge anatakiwa aandike barua yake binafsi ya kukata posho yake kama alivyofanya zitto.
Kwanini wasiandike mmojammoja,baada ya kukubaliana kichama?
ACHENI USHABIKI JAMANI,MNATURUDISHA NYUMA!!!
 
Hakika endelea na moyo huu kila mara simama imara katika kujenga na kuona ufisadi huu unakuwa na kukataliwa kabisa maana kama ndio chadema ndio wanapiga vita ufisadi na hivyo kuna haja ya kufanya mambo mazuri kama haya!! Mungu atawabariki sana
 
Spika ni CCM, anajua kabisa jambo analotaka kulifanya Zitto litakuwa ni mkuki kwa CCM. Sasa wewe unategemea angefanyaje? Sijawahi kumwona spika Boga kama huyu!
ni


ni!

kwa kuwa wabunge wa ccm hutumi rushwa kushinda chaguzi, hapo wapo vitumbo joto kwa kuwa bado wana madeni mengi
 
NI KUHUSU POSHO BUNGENI, SASA AKATAA KUSAINI MAHUDHURIO
Neville Meena, Dodoma
HOJA inayoshinikiza kufutwa kwa posho za wabunge pamoja na watumishi wengine wa umma imeendelea kuzua majibizano baina Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe na Ofisi ya Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Wakati Ofisi ya Spika wa Bunge inasisitiza kwamba fedha za posho za vikao zitawekwa katika akaunti ya Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema) hata kama hazitaki, Zitto amesema kwamba sasa hatasaini karatasi ya mahudhurio.

Zitto alisema jana mjini hapa kuwa tangu Juni 10, mwaka huu alishamjibu Spika akikataa "kushinizwa kuchukua posho za vikao" (sitting allowances) akisisitiza kwamba hatua atakayoichukua ni kutosaini karatasi za mahudhurio katika vikao vyote. Mahudhurio hayo ndiyo hulalalisha mbunge kupewa posho hizo.

"Kuanzia kikao cha juzi cha Tume ya Mipango, sikusaini na mkitaka nendeni mkaangalie ile orodha na kesho ndani ya Bunge sitasaini ili kuondoa uhalali wa kupewa posho hizo, sasa hapo tutaona watanilazimisha kwa njia gani," alisema Zitto.

Juni 10 mwaka huu, Bunge lilimwandikia Zitto barua likimweleza kuwa ofisi yake haiko tayari kupeleka posho zake katika Taasisi ya Kigoma Development Inititive (KDI), kama alivyoomba na kwamba fedha hizo za posho zitaendelea kuwekwa katika akaunti yake benki.

"Nimeelekezwa na Spika nikufahamishe kuwa, pamoja na nia yako nzuri uliyoionyesha, utaratibu wa Ofisi ya Bunge kwa sasa ni kulipa stahili za wabunge moja kwa moja kwa wabunge husika kwa mujibu wa sheria...," imeeleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Nenelwa Mwihambi Wankanga kwa niaba ya Katibu wa Bunge na kuongeza: "Isipokuwa mara baada ya kupokea stahili zako wewe mwenyewe unaweza kuamua uzipeleke wapi."

Barua hiyo ilikuwa ikijibu ya Zitto aliyoiandika Juni 7, mwaka huu kwa Katibu wa Bunge akikaataa posho zake za vikao na kutoa maelekezo kwamba iwapo ni lazima alipwe basi fedha hizo zielekezwe KDI kuanzia Juni 8, mwaka huu.Lakini Juni 10, Zitto alijibu barua ya hiyo akikataa kile alichokiita: "Shinikizo la kupokea posho za vikao" kwa kusema asilipwe fedha hizo kuanzia Juni 8.

"Kwa kuwa umesema kwamba sheria inawataka kulipa stahili za wabunge moja kwa moja (ingawa hukutaja ni sheria ipi) na kwamba ni kama ofisi yako inanilazimisha mimi kupokea stahili ambayo ninaamini sistahili. Nakupa taarifa kwamba nimeonelea bora kukataa stahili hii," inasema sehemu ya barua ya Zitto kwenda kwa Spika na kuongeza:

"Hivyo ninaelekeza kwamba ofisi yako isinilipe stahili ya posho ya kikao (sitting allowance) kuanzia Juni 8, 2011".

Gazeti hili lilipomuuliza Zitto ni kwa jinsi gani atakavyokataa fedha hizo alisema: "This is very simple (ni rahisi sana) kwani hata juzi kwenye ile semina ya mipango sikujiandikisha na kuanzia kesho nikiingia bungeni sitajiandikisha, hapo watanipata vipi?"

Kwa mujibu wa Zitto, posho za vikao hutolewa kwa kuzingatia mahudhurio bungeni na kwamba wabunge wasiosaini kwenye fomu hizo, huwa hawapewi posho hizo.Alisema kutoka na msingi huo, hakutakuwa tena na ugomvi baina yake na Spika wa kulazimishwa posho za vikao, kwani hawezi kulipwa fedha hizo kama asiposaini karatasi za mahudhurio hatua ambayo tayari ameanza kuitekeleza.

Msimamo wa CCM
Wakati Chadema wakiendelea kulumbana na Serikali kuhusu pendekezo la kufutwa kwa posho za wabunge pamoja na zile za watumishi wengine wa umma, CCM kimesema suala hilo linajadilika na kwamba si busara kupinga kila kinachotoka upande wa pili.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC-CCM), Nape Nnauye alisema mjini Dodoma juzi kuwa chama hicho hakipingi wala kuunga mkono kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa umma, lakini akabainisha kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa na kufikiwa mwafaka baina ya pande zinazopingana.

Alisema malumbano yanayoendelea nje ya Bunge baina ya pande zinazopingana hayana tija na kwamba wabunge wote wa CCM na wapinzani watumie fursa walizonazo katika vikao kufikia mwafaka wa suala hilo."Kama posho za vikao zipo kisheria au kisera, mifumo ya kufanya mabadiliko iko wazi na inajulikana, sasa malumbano yanayoendelea nje ya vikao vya bunge sijui ni kwa faida ya nani?" alisema Nape na kuongeza:

"Kwa mfano, mimi nafahamu Zitto kwamba ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge, angeweza kuanzia huko, lakini kwa kuwa ameishatamka hadharani si lazima wale wanaojibu nao wazungumze hadharani, wanaweza kuliingiza katika taratibu za kawaida za vikao na kujadili kisha kukubaliana."

Kauli hiyo ya Nape ambaye ni msemaji mkuu wa CCM, huenda isiwafurahishe wabunge wengi wa chama hicho ambao kwa nyakati tofauti wamesikika na kunukuliwa wakibeza msimamo wa Chadema kuhusu posho za vikao kwamba haziwezi kuondolewa na kwamba Chadema wanatafuta umaarufu usio na msingi.

Malipo ya Posho
Habari kutoka katika vyanzo mbalimbali zinasema kwamba malipo ya posho kwa watumishi wengi wa umma yamekuwa yakifanywa kiholela kiasi kwamba baadhi ya maofisa wengine serikalini wamekuwa wakipata posho zaidi ya moja katika tukio moja.

Habari kutoka serikalini zinasema kufutwa kwa posho za vikao kutaongeza tija kwani ni kweli kwamba watumishi wa umma hasa wale wa ngazi za juu wamekuwa wakiendesha vikao kila siku kwa lengo la kujikusanyia posho, hata pale vikao hivyo vinapofanyika katika ofisi za taasisi husika.

Mmoja wa watumishi wa taasisi moja ya elimu ya juu nchini ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema mjini Dodoma kuwa: "Pale kwetu mbona ndiyo mchezo, tena wakati mwingine utakuta idara inasimamia mambo matatu, lakini kila jambo linaandaliwa kikao chake na kila kikao kina posho yake, wasipofanya hivyo watakula wapi?"

Mtumishi mwingine katika moja ya wilaya zilizoko Kusini Magharibi ambaye pia yupo mjini hapa alisema katika halmashauri anayofanyia kazi, watendaji wakuu hulipwa posho za kujikimu (per diem) hata kama wasipolala nje ya kituo cha kazi."Unaweza kusikia kachukua posho ya siku 10 kwenda huko vijijini lakini baada ya siku mbili unamkuta karudi ofisini kwa madai kwamba kuna dharura na ndiyo safari imeisha wala haendi tena na pesa harudishi," alisema na kuongeza;

"Sasa bwana ninyi waandishi mtusaidie kufichua haya maana sisi wadogo ndiyo tunaonyayasika, ukienda kudai hata hela yako halali hupati, unazungushwa hata wiki mbili lakini hawa wakubwa wanachota tu."
 
Achukue posho,aiambie bank waipeleke kigoma hiyo posho....mengine ni umaarufu tu.
 
Achukue posho,aiambie bank waipeleke kigoma hiyo posho....mengine ni umaarufu tu.
Nadhani umaarufu wenye lengo la kuisadia taifa ni bora kuliko umaarufu wa kulihujumu taifa. Zitto amewahi kuhoji jambo hili ikiwa ni pamoja na wabunge kuwa katika board akionyesha conflict of interest. Wabunge walimpinga si kwa hoja bali kujua ulaji utaondoka. Huko Nyuma Dr Slaa alieleza akiwa Hedaru Same wingi wa marupu rupu ya wabunge huku wananchi wakiwa masikini.

Katika hoja zote wabunge walizikataa ima zisijadiliwe na hata kumzomea Dr Slaa bungeni. Jambo wasiloelewa wengi ni kuwa Zitto hajasema posho zifutwe, amehoji kwanini wabunge walipwe posho wakifanya kazi waliyoomba? Yaani ni kama wewe Kobello uajiriwe na kila ukiingia ofisini ulipwe posho, kama mfano huu utakusaidia kuelewa dhana halisi.

Zitto kama mwanasiasa ametumia mbinu ya kupata 'public support' kwasababu taratibu zingine hazitafikia lengo alilokusudia la kuondoa dhuluma. Masuala kama ya Kagoda yamepigwa dana dana hadi leo hakuna jibu unadhani hili linalogusa maslahi ya wabunge hasa wa CCM waliofanya bunge kama mradi ingepitaje au kujadiliwa vipi!!!

Anachokifanya Zitto ni kama kile cha rais kuongea na wazee wa Dar, kwani si angeweza kuongea nao kimya kimya kwanini awaite Diamond! Alichofanya Zitto ni kama kile cha wafungwa kugoma kula, kwanini wasikae kimya kama hawataki kula,kwanini walipanda ndani ya karandinga wakijua hawataki kushuka?

Anachokifanya ni ku-draw attention na hakika imesikika kwa wananchi. Anachokifanya ni kulionyesha taifa tofauti ya uzalendo na unafiki na kama kiongozi hana sababu ya kufanya nyuma ya pazia, anatakiwa aongoze kwa mifano. Namuunga mkono kucheza karata hii ya kisiasa itakayotunufaisha.

Hatuna 'moral authority' ya kunyooshea vidole mafisadi huku tukifumbia macho ufisadi kwa njia ya posho.
Hatuwezi kuhimiza uchimbaji wa madini na ukusanyaji kodi kama kodi hizo zinaishia kulipa posho.
Hatuwezi kuwaambia watu wajitolee huku wengine wakilipwa posho kwa kazi walizoomba.
Hatuwezi kumwambia mwaanchi achangie shule ya kata wakati kodi zake zinamlipa posho mtu anayesinzia bungeni.
Hatuwezi kudhibiti ufujaji wa pesa halmashauri wakati watunga sheria wanafuja kwa njia ya posho.
Hatuwezi kuwaambia wazee wa EA hatuna pesa za kuwalipa wakati waliopaswa kuwasemea shida yao wanakula posho kwa wasichokifanya.

Na mwisho kobello hebu kokotoa hesabu hii : 70,000*320*30
 
Hongera kwa kufikiria watu wenye mahitaji zaidi kadri mtu anapopanda juu na siyo kuwasahau.
Ushauri wangu kuhusu posho hizi ni kwamba zikatwe ziwekwe halafu kwa muda maalumu ijulikane ni kiasi gani kimefikiwa na hapo wale waliokatwa waamue zitumikeje na wapi ili kuweka kumbukumbu ya shabaha yao na kuthibitisha kuwa kweli fedha hizi siyo negligible kama wengine wanavyodai na kama wabunge wote wangesamehe posho zao kikubwa zaidi kingeweza kufanyika kuleta maendeleo au kuboresha huduma kwa wananchi. Katika kuamua zitumike wapi kuna mtazamo wa kitaifa au kupelekwa katika majimbo wanakotoka wabunge husika. Baada ya hapo itakuwa rahisi zaidi mtu kuelewa tungrfaidikaje kama posho hii ingefutwa kote ndani na nje ya Bunge. Vinginevyo watu hawataona impact wazi wazi yenye kielelezo kutokana na wao kuacha kuchukua posho hii wakati wengine wanaendelea kuchukua.
 
Nguruvi,
Zitto ni mbunge ambaye sidhani kama kutatokea mpinzani kwenye jimbo lake,inngekuwa ni vizuri zaidi kama wabunge wa CDM kwa pamoja wangekubaliana kufanya hivi.Lakini kama mbunge mmoja hii inazua uwalakini fulani kuhusu umoja wa wabunge wa CDM.Na kama hawakubaliani nae ,hii inamaanisha kuna uwalakini ndani ya CDM bungeni.
Forget politics,watanzania wote tunajua posho za wabunge ni kubwa,hii sissue iko popular,instead of using the money for his charity anakataa kuchukua kabisa na hizo hela zinaurdi kwenye chai na kalmati.

Wananchi wana loose opportuity kwa ajili ya politics(too much it annoys)
 
Nguruvi,
Zitto ni mbunge ambaye sidhani kama kutatokea mpinzani kwenye jimbo lake,inngekuwa ni vizuri zaidi kama wabunge wa CDM kwa pamoja wangekubaliana kufanya hivi.Lakini kama mbunge mmoja hii inazua uwalakini fulani kuhusu umoja wa wabunge wa CDM.Na kama hawakubaliani nae ,hii inamaanisha kuna uwalakini ndani ya CDM bungeni.
Forget politics,watanzania wote tunajua posho za wabunge ni kubwa,hii sissue iko popular,instead of using the money for his charity anakataa kuchukua kabisa na hizo hela zinaurdi kwenye chai na kalmati.
Wananchi wana loose opportuity kwa ajili ya politics(too much it annoys)

Kuna kitu kinaitwa 'partisan na bipartisan', halafu katika mabunge yenye vyama vingi kuna issue zinakuwa ' bind or non-bind'.
Kwa suala hili la posho sina shaka ni la CHADEMA ingawa wapo wadandiaji, lakini pia nadhani ni non-bindi ndiyo maana Zitto ameamua kwenda solo kama ilivyokuwa kwenye suala la kususia hotuba ya rais bungeni.
Suala kama la katiba ya nchi kuandikwa upya ni sera ya CDM na automatically inakuwa partisan and bind.

Tahadhari hata hivyo, ukiwa wabunge wa CCM hakuna bipartisan wala non-bind, wao wana partisan and bind kwa kutumia neno 'Yes' hata kama issue ni kuuza kipande cha nchi.
 
Siamini kama kutangulia kwa Zitto kunaharibu hoja ilioko mezani. Cha msingi CHADEMA wachukue kitendo cha kutangulia kwa zitto positively. Otherwise mtaji huu utatekwa nyara kama Zitto ataendelea kuonekana ni mbinafsi eti tu kwa kuanza kuandika barua ya kukataa posho.
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?


naomba ujue kuwa ww ni mnafiki sana, mbona huyo slaa alipiga mikelele tu na hakukataa kupokea hiyo hela na sasa analipwa hela posho kama ile aliyoipinga bungeni?
mm namsifu zitto, kwani amejua cdm hasa mbowe ana tamaa ya kufidisha pesa zake alizotumia kwenye uchaguzi na kuwalipa watu aliowaita makamnda vivuli wa kufanya umafia huko hai, hivyo alitaka hii hoja ipelekwe bungeni na ikataliwe tu au ipigiwe kura ishindwe na wananchi waone kuwa alikuwa na nia nzuri kumbe changa la macho, sasa zitto yeye kachukua hatua kuliko makelele yasiyozaa, heeeee shangaa mnaanza kumponda.
jamani mnashangaza sna, na hao wajinga akina fulani nawajua wameweka mata...ko miaka zaid ya 10 bungeni wakatae posho........ huu ni mtihan kwenu wanafiki mliojificha upinzani.
 
ZITT ZUBER KABWE (ZZK), naomba nikushauri, fedha zenu za posho za wabunge wa chadema tunazihitaji wana chadema kuimarisha chama chetu ktk ngazi zote. Tunazihitaji fedha hizo kujenga ofisi za mikoa na wilaya, pamoja na kugharamia shughuli zingene za uenezi wa chama. Zikusanyeni tuzitumie kuwaondoa mafisadi wa ccm.

acha upotoshaji wa kijinga wewe, nani kakwambia cdm haina uwezo huo wa kusambaza ruzuku nchi nzima na hii ndiyo hoja mfu ya kijinga anayoweza kuleta mbowe baadae ili apate nafasi ya kuzitumia hizo posho za watu. yaani usanii wa kijinga mwaka huu hauna nafasi kabisa...cdm inapata millions ngapi za ruzuku? usikurupuke wewe.
 
Hili wazo ni zuri sana na linaweza kupata Masss support lakinilinapaswa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa sana kuliko kurupuka natumaini Zitto hakukurupuka labda tuaimini amelianzisha kama chambo kupima upepo wa Ndani ya Bunge lakini kama Zitto alilifanya kwa matakwa yake mwenyewe labda kasababu taayari CDM wanalipigia kelele au watalizungumzia kwenye Bajeti ya upinzani linaweza kuleta mgawanyiko kuliko tunavyofikiri na huenda ilinakaonekana kama ni mtego kwa wabunge wenzake na CDMA kwa ujumla. Pia linaweza kuonekana ni mkakati wa wasiokitakia mema CDM


Nafikiri lingekuwa ni la kichama , Chama kingeweza kuja na CONSTRUCTIVE PLAN ya jinsi posho hizo zituike kwenye maendeleo INDIRECT au DIRECT. any way inawezekan Zitto amefanya hivyo kuona Bunge liltalichukuliaje then waje na Collective ideas let wait and see.
Ningependekeza wazo hili liwe ni la kichama zaidi

hapo sasa unamaana gani eti wazo liwe la kichama sawa!!! ila habari za mgawanyiko kwa wale wasio kuwa tayari hilo ni upofu wa akili yako, au ww ni mmoja wao? bila shaka ww ni wa viti maalum uliyepta kwa kugawa tu.....na ndio tutawajua wanafiki hapa
 
Hii ni changamoto ya ukweli kwa wabunge na bunge kwa ujumla! Namshauri na mbunge wa Arusha azielekeze posho zake kwenye maendeleo ya jimbo letu!


hahahahaaaaaaaaaaaaaa, huyo jamaaa anasubiri mkubwa wake amwagize tena, kama anavyofanya kwenye issue nyingne.
 
kwa kweli mie sijaona mantiki ya mbunge kukataa posho, ingekuwa anachallenge kiwango cha hizo poso, ningeelewa. mfano mimi kazi zangu ni za kusafiri sana na mshahara wangu huwezi hata gharama za siku mbili hotelini, sasa usiponipa posho nitawezaje kutekeleza majukumu yangu kikamilifu? najua wakati mwingine posho ni kubwa hasa ukulinganisha na tija inayopatikana, lakini siyo uiondoe bali ikibidi uangalie uwezekano wa kupunguza!

hujaelewa chochote kaaa chumbani usome vizuri maelezo na hoja yake wewe usikurupuke kujibu usichokijua....
 
  • YEYE ASEMA KAMA NI KWA KUKATAA POSHO YUKO TAYARI
VITA ya kufutwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, imechukua sura mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema kwamba Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge baada ya kuahirisha mkutano wa asubuhi, Makinda alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinazothibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vyake.

"Kwa mujibu wa kanuni zetu, asipohudhuria mara tatu anakabiliwa na adhabu tena ya kufukuzwa bunge, hizo ndivyo kanuni zinavyosema." Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika akisema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone. Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema Zitto.


Soma zaidi gazeti la Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom