POSHO: Bunge lamjibu Zitto Kabwe; atoa msimamo wake

Mhh...nadhani dhamira za kifisadi ni kubwa kuliko tunavyofikiri.Hapa ndipo utakapotofautisha kati ya wazalendo wa kweli wenye nia ya mabadiliko na wabinafsi.Zitto endelea kuonyesha njia,usitarajie kuungwa mkono na wengi.Siku zote ukweli husimama hata kama una sapoti ya mtu mmoja.Kasi ya kutaka mabadiliko inabidi iendane na vitendo dhahiri kama hivi.Bado tunahitaji kuongeza spidi,tuonyeshe dhamira yetu ya dhati katika yale tunayoyaamini

Well said !
 
ninawasiwasi kuhusu baadhi ya wabunge wa chadema,as far as suala zima la teamwork linavyohusika. kama tunavyowasikia wenyewe kuhusu suala kufutwa posho inaonekana ni suala la kichama na kambi yao nzima ya upinzani. sasa iweje mtu mmoja aanze ku execute mpango mzima wa chama peke yake? ndo maana zinajengeka hisia za ubinafsi ndani ya chama na hata uzito wa issue yenyewe unapungua inapapelekwa hoja na mtu mmoja mmoja tofauti na ambavyo ingepelekwa na kambi ya upinzani kama hoja ya pamoja. 2. tukiangalia majibu ya ofisi ya bunge, kwamba utaratibu uliopo sasa ni" kumlipa mbunge moja kwa moja" hatuoni kwamba kuna umuhimu wa kupeleka hoja kwanza bungeni au popote panapohusika ili kuubadili kwanza utaratibu huo ili hoja ya kuzifuta iweze kupata nguvu?

Kuhusu Zito kuwa mbinafsi kidogo naona si kweli. Wajua mpaka muda budget ya upinzani inasomwa tayari watu wengi watakuwa aware na ishu ya Zito kukataa malipo ya sitting allowance. Sasa hapo kambi ya upinzani nayo kama team itakapokataa awareness kwa public inaeza kuwa mara tatu au zaidi na kupata support kubwa. Ni move nzuri kumtuma Zitto achokoze ili watu waanze kutafakari while waiting for a big Support.

Hapo nakiunga mkono chama kwa kuwa makini katika kupeleka hoja KITAIFA zaidi
 
Dogo Mheshimiwa Zito IQ yako iko juu sana. Ni hivi, seating allowance ni kwa ajili ya mtu ambeye ameacha kazi zake na kuitwa kwenye seat (Kikao) hivyo inamaana ya kumfida muda wake aweze kujikimu. Kuwapa wateule wachache seating alowance kwanza ni kosa. Mtu aliyekwishapata fedha ya kujikimu, au mshahara kwenye station yake, hakuna justification yeyote ya kumpa seating allowance. Huu ni uwizi kwa umma wa watanzania. Nami namuhakikishia mbunge yeyote atakayepokea hii seatin allowance, anajiondoa mwenyewe kuwa mwakilishi wa umma wa waTanzania, na hakika hatarudi bungeni, na Jehanamu ataiona.

Je Mkulima atalipwa na nani seating alowance kwenye vikao vya serikali ya mtaa, kwanza anaacha kazi yake, halipwi pesa ya kujikimu, halipwi mshahara, na business siku hiyo inakuwa imefungwa (no income)

Aibu kubwa sana kwa nchi maskini kama Tanzania kuwa na wabunge wabinafsi, wezi, wabadhilifu na wasio na utu.

Chondechonde, ripoti ya kiinteligensia inaonyesha, hawa ni wabunge watakaongia bungeni kwa mara ya mwisho.

Duh aibu Kubwa

Hongera sana mdogo wangu Zito Kabwe na CDM, Mungu amekusikia, na atakutendea makubwa sana, usirudi nyuma.:hug:
 
Natamani wabunge wooote wa CHADEMA waandike barua moja ya kukataa posho. Hata kama office ya Speaker itakataa kusitisha posho lakini for the record wafanye hivyo. Then wazunguke nchi nzima kuwavua nguo wabunge wa ccm-wala posho. Kwa kuanzia ningeomba wafanye hiyo campaign KARIAKOO. Itaondoa amani na utulivu (kama bado vipo) ndani ya ccm! and that is what you want as a political party- create chaos for your opponent until they are out of the equation.
 
Mkuu u are right, lakinik nadhani zitto amefanya hivyo akiamini is a right move na angeungwa mkono na wabunge wengine.

Nadhani Zitto alijua kuwa haitaungwa na wabunge wengi hata wale walio kwenye chama chake ndio akaona bora achokoze mambo hadharani. Sasa tuone kama watayaoga maji waliyoisha yavulia nguo!

Amandla......
 
Ofkoz lazima wafanye hivi manake inaonyesha ni kiasi gani ofisi ya bunge ikiongozwa na spika walivyokuwa wagumu kufikiri kuhusiana na dhamira aliyoionyesha mhe. Zitto Kabwe
 
Nadhani Zitto alijua kuwa haitaungwa na wabunge wengi hata wale walio kwenye chama chake ndio akaona bora achokoze mambo hadharani. Sasa tuone kama watayaoga maji waliyoisha yavulia nguo!

Amandla......

Wabunge wote wa CDM wasipoiunga mkono watapoteza imani kubwa waliyopewa na wananchi ..watch out guys!
 
Asaalamu aleykuma wadau wote wa JF. Zitto Kabwe amesalimisha posho yake: That is good. Kila mtu ana hamu ya kusikia habari kama hiyo kutoka kwa Mbunge wake aliemchagua: lakini mimi nina hofu kadhaa wa kadha labda wasalimishaji wote wa posho hizo waliopo na watakakaofuata wanawaeza kunitoa hofu hizo; Tukirudi kwenye ukweli ZITTO ZUBERI KABWE HAJAACHA AU KUIKATAA posho yake. Ipo kwenye aya ya Tatu ya Barua yake kwa Katibu wa Bunge kuwa posho yake iwekwe kwenye akaunti ya KDI. Taasisi kama hizi huwa zina viongozi waratibu na pengine wanaohudumiwa na Tasisi hizi ambazo pia wanalipwa posho za vikao vyao vya uendeshaji1 Sijui ZITTO KABWE ana wadhifa gani kwenye taasisi hiyo lakini ukweli unabaki pale pale Posho ya ZITTO ameitanguliza Kigoma au Posho yake ameipangia matumizi mengine tofauti na wabunge wengine ambao eidha wananunua Vyangudoa nk. Nitapata faraja pale wabunge wote wawe wa CDM au Wanamagamba au CUF na wengine watakaoamua kufuata njia ya Zitto wawe na mfuko wa pamoja na kuzipangia fedha hizo matumizi wao wenyewe kulingana na shida za watz wanaowawakisha. Hii maana yake ni kuwa wazisimamie wenyewe kwani kuziacha serikalini zifanyiwa ufisadi .
 
Uroho wa posho na ubinafsi bila kujali maslahi ya taifa letu, trilioni moja, hali mbaya ya shule zetu na walimu na mambo mengine itatupeleka pabaya.

visingizio vingiiiiiiii

Posho hizi zifutwe.
 
Excellent zito,hapo ndipo tunapotaka tuone wabunge ambao wapo kipesa zaidi na ambao wapo kwa ajili ya wananchi.Mkulo bora ungenyamaza tu ya nini kujizalilisha,unaonyesha ni jinsi gani unavyofurahia tunavyoliwa kodi zetu,hebu uwe na soni hata kidogo.Hivi watz wakichachamaa kweli mtakuwepo madarakani?kaeni mfikiri kwa makini maana chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho
 
ZITT ZUBER KABWE (ZZK), naomba nikushauri, fedha zenu za posho za wabunge wa chadema tunazihitaji wana chadema kuimarisha chama chetu ktk ngazi zote. Tunazihitaji fedha hizo kujenga ofisi za mikoa na wilaya, pamoja na kugharamia shughuli zingene za uenezi wa chama. Zikusanyeni tuzitumie kuwaondoa mafisadi wa ccm.
 
Kama hawataki posho zao kufutwa,basi na sisi wananchi huku vijijini hatutahudhuria vikao wala mikutano hadi kuwe na posho ili twende sawa...!
 
What does this mean? Au alifikiri watu wanabeep walipokuwa wanataka posho ziondolewe?

Posho-Za-Vikao-Majibu-Ya-Bunge.jpg

Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg

Kama huu ndio mpango wa chama , Mbona wabunge wengine wa Chama cha Demokaya na Magwanda (CHADEMA) hawajajitokeza kuandika kama hivi ? nadhani Zitto wamemuingiza mkenge wenzake huku wao wakiendelea kutia pesa mfukoni. Mnyika, Mbowe, Mdee nk vipi mbona kimya au nyie huu mpango wa chama chenu hauwahusu?
 
Uroho wa posho na ubinafsi bila kujali maslahi ya taifa letu, trilioni moja, hali mbaya ya shule zetu na walimu na mambo mengine itatupeleka pabaya.

visingizio vingiiiiiiii

Posho hizi zifutwe.

Acha kuwa mbayuwayu wewe, lete data za mafao ya wabunge wa tanzania ukilinganisha na nchi za zingine za east africa, acheni kutumiwa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa
 
Hili wazo ni zuri sana na linaweza kupata Masss support lakinilinapaswa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa sana kuliko kurupuka natumaini Zitto hakukurupuka labda tuaimini amelianzisha kama chambo kupima upepo wa Ndani ya Bunge lakini kama Zitto alilifanya kwa matakwa yake mwenyewe labda kasababu taayari CDM wanalipigia kelele au watalizungumzia kwenye Bajeti ya upinzani linaweza kuleta mgawanyiko kuliko tunavyofikiri na huenda ilinakaonekana kama ni mtego kwa wabunge wenzake na CDMA kwa ujumla. Pia linaweza kuonekana ni mkakati wa wasiokitakia mema CDM

Tunaomba Zitto aje hapa alitoleee maelezo ikiwa amefanya hivyo kibinafsi au ni mpango wa kichama na kama amefanya hivyo kwa matakwa binafsi basi ataonekana ni mbinafsi kwani impact yake inaweza kuleta matatizo katika chama hasa kwa wabunge ambao hawakuwa tayari kwa sasa kutokuchukuwa posho zao.

Nafikiri lingekuwa ni la kichama , Chama kingeweza kuja na CONSTRUCTIVE PLAN ya jinsi posho hizo zituike kwenye maendeleo INDIRECT au DIRECT. any way inawezekan Zitto amefanya hivyo kuona Bunge liltalichukuliaje then waje na Collective ideas let wait and see.
Ningependekeza wazo hili liwe ni la kichama zaidi
 
attachment.php

Alivyojibiwa sawa sawa, sasa tunamngoja Zitto atangaze aseme mimi sizitaki na kuanzia leo nisilipwe, hapo ndio tutajuwa kweli.

Inamaana we ni kipofu au unasoma taarifa bila kuzielewa na unazijibu. Angalia vizuri utaona barua ya mh. Zitto akizikataa kabisa hzo posho zao wanazolazimisha azichukue ili wao wasipate aibu.
 
Nadhani Zitto alijua kuwa haitaungwa na wabunge wengi hata wale walio kwenye chama chake ndio akaona bora achokoze mambo hadharani. Sasa tuone kama watayaoga maji waliyoisha yavulia nguo!

Amandla......

Mkuu u are right, lakinik nadhani zitto amefanya hivyo akiamini is a right move na angeungwa mkono na wabunge wengine.

Zitto is very clever! Ameitega ofisi ya Bunge. Kwa vile wamekataa kumkata pesa hizo na kuzipeleka kwenye mfuko wa KDI; basi endapo wakikubaki kumkata (kwa barua ya pili); basi atawauliza kwa sheria ipi wamefanya hivyo. Tukumbuke kuwa wamesema sheria haiwaruhusu kuzi-deposit kwenye account ya KDI.
Ni vema pia tukajua kuwa mlipwaji anaweza kutoa maelekezo namna gani malipo yake yalipwe. Hilo limefanyika mara kadhaa. Je, hiyo huwa ni sheria gani?
 
Hivi mwajiri hawezi kukulipa pesa kwenywe akaunti unayo itaka wewe na si ile ambayo ulikuwa unatumia awali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom