Posho...allowances..wadau nisaidieni ushauri/elimu katika hili

gizalucky

Member
Aug 5, 2011
44
10
Swala/Swali ni hili; Hivi posho( allowances) huwa zinakatwa kodi??
Je huwa zinajumuishwa kwenye mshahara then kupata gross salary ambayo inakatwa kodi...kwa maana hiyo na posho zimekatwa kodi???
Imenitokea kwenye kazi yangu ninayofanya sasa natambua/ nahisi kuna usanii umefanyika hapa.
Naombeni michango yenu nijue kama si sahihi kufanya hivyo ili niweze kujua cha kufanya..kama kufuatilia haki yangu kama imechezewa...
Kwani sheria za nchi za kazi zinasemaje?? Usikute hawa waajiri wetu wanatumia udhaifu wetu wa kutojua sheria kutunyonya...kwa faida yao/ au kwa vyovyote...Information is Power !!!!
Please wadau nawasilisha naomba msaada/ ushauri/ maoni yenu..ikiwezekana hata vifungu vya sheria za kazi....
Naomba kuwasilisha....Pamoja Jamii Forum Forever
 
Uko serikalini au private sector? tuanzie hapo kwanza ndo itakuwa rahisi kujua.
 
mhhh! ngoja tusubiri wataalam watueleze ila nachojua mimi posho huwa hakuna makato ya aina yoyote ile.
 
mhhh! ngoja tusubiri wataalam watueleze ila nachojua mimi posho huwa hakuna makato ya aina yoyote ile.
Mapato yote unayopata kutokana na ajira yanastahili kukatwa kodi. Hayo ni pamoja na overtime, bonus, hata kama unapewa gari na nyumba na kampuni nayo yanastahili kulipiwa kodi. Hivyo hata sitting allowances, housing allowances, responsibility allowances zote zinastahili kukatwa kodi. Kwamba waajiri wengi wamekuwa hawafanyi hivyo huko ni kukiuka sheria. Na wanapogunduliwa na TRA adhabu yake ni kubwa mno. Cha muhimu labda ni kuhakikisha kuwa hiyo kodi uliyokatwa imepelekwa TRA. Maana wengine hukaTA lakini hawaziwasilishi kunakotakiwa.
 
Kama alivyokueleza Bwana Ruge, kila allowance ni lazima zinakatwa kodi, isipokuwa allowance zote zinazotolewa bila upendeleo kwa wafanyakazi wote hapo ofisini mfano kama kuna gari linawabeba wote bila kubaguwa huyu ni Boss au mpiga deki, kama mnakula wote mlo mmoja bila kubagua cheo na vile vile ktk nyumba. Hivyo hawakuonei bali wanatekeleza sheria ya kodi.
 
Back
Top Bottom