Elections 2010 Poor Media Houses and Journalists

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
Inasikitisha kuona kuwa vyombo vya habari vinashindwa wanashindwa kutangaza matokeo ya kura za urais katika majimbo ambapo kura zimekwishatangazwa kwa kisingizio kuwa wanasubiri matokeo hayo yatolewe na Tume. Hii ni aibu hasa kwa kituo kama ITV ambapo leo asubuhi nimemshuhudia Leinfred Masako akimzuia mwandishi kuripoti kura za mgombea urais kutoka Morogoro kwa kisingizio kuwa matokeo hayo yatatangawza na Tume muda ukufika. Maana ya hali hii ni kuwa waandishi pamoja na vyombo vyahabari wamepewa specific instructive details juu ya namna ya kutangza matokeo ya kura za urais; shame!!!!!!!
Ki misingi ukweli ni kwamba kura za urais zinatangazwa katika ngazi ya majimbo sambamba na kura za ubunge, hivyo hakuna sababu ya waadishi kushindwa kutangaza matokeo ya kura hizo. Wala kutangaza kura ambazo tayari ROs wametangza katika majimbo siyo kuvunja sheria. It is sheepish behavour na kujikomba komba kwa waandishi na vyombo vya habari husika.
Haiingii akilini kuona vyombo vya habari vinatangaza kura za ubunge jimbo la Hai lakini vinaacha kuripoti kura za urais katika jimbo hilo, wakati kura za ubunge na urais zimetangazwa kwa wakati mmoja! Mbaya zaidi vyombo hivyo hivyo, tena bila kuhoji, vinakimbilia kutangaza matokeo ya kura za urais na ubunge katika jimbo la Peramiho! Hata wanashindwa kuhoji inakuwaje matokeo ya Peramiho yatoke kwa seti, wakati matokeo ya Hai yatoke kivyakevyake.
Majimbo anakoungwa mkono Kikwete, matokeo yanatangazwa kwa seti, anakoungwa mkono Dr Silaa/Chadema, matokeo yanatoka kivyakevyake.
Waandishi/vyombo vya habari tuondolee aibu hii.
 
Hasa ITV yaani wana upendeleo wa wazi kabisa kwa CCM.
Huko ni kujipendekeza.
 
Your very correct bro hii imenisababisha nisiangalie hata hizo tv station,kwa kuwa report ziko biased kweli.Njaa tu inawasumbua hawa halafu wamesahau kuwa huwezi kuizuia mvua kunyesha!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom