Poor Dar..

Ni kweli. Maisha dar zero. Makazi duni n.k. Isingekuwa nimejifunga kwa majukumu ningerudi mkoa
 
Baada ya kuishi kwa miaka ya kutosha Dar es salaam... baada ya kuchakachua na kuchakachuliwa na maisha(katika anga zote unazojua)...nadiriki kusema..DSM HAIFAI...HASA KWA MAISHA YA KULEA FAMILIA/NDOA..

Uongo?:thinking:

KWa uozo umeanza leo, mbona ni siku nyingi sana? Uozo wote wa Tanzania umejaa dar. mashoga, masagaji, makahaba, mateja, matapeli, waswahili na yote yako ple. Kama serikali yetu ingekuwa na busara Capita ilitakiwa ihamishwe siku nyingi sana kwenda nje ya Dar.
 
Mkuu naunga mkono kwa asilimia zote... maisha ya Dar na hasa maofisini ni ya kufeki na hayana maadili kabisa, heshima ni ndogo na uongo umezidi, wengi tunaishi maisha yasiyo yetu na tunadanganyana sana

Upigaji ndio usiseme, uzungu koko ni balaa

Lakini je, tukaishi wapi?

kwa uzoefu wangu..na best zangu amba wamepata kazi mikoani na wameham na familia zao.... nikiwwambia kuhusu kurudi dar... wananisonya...HWATAKI HATA KUIOTA!!
 
Baada ya kuishi kwa miaka ya kutosha Dar es salaam... baada ya kuchakachua na kuchakachuliwa na maisha(katika anga zote unazojua)...nadiriki kusema..DSM HAIFAI...HASA KWA MAISHA YA KULEA FAMILIA/NDOA..

Uongo?:thinking:

Tuambie twende tukaishi wapi!!!!!!!!!!!!!!!!! Kupiga kelele peke yake bila kutoa suluhisho hakutoshi
 
Kwa mara ya mwisho kukaa DSM ni mwaka 2007 kule kinondoni kero kuanzia joto,foleni,maadili mbofu mbofu
Kwa sasa huwa nakuja tuu kuwacheki washikaji siku 2 au 3 then nachapa mwendo
 
Baada ya kuishi kwa miaka ya kutosha Dar es salaam... baada ya kuchakachua na kuchakachuliwa na maisha(katika anga zote unazojua)...nadiriki kusema..DSM HAIFAI...HASA KWA MAISHA YA KULEA FAMILIA/NDOA..

Uongo?:thinking:
Mkuu kwanza naomba uelewe kuwa mtoto anatokana na genes za wazazi, kama wazazi micharuko ni ya kurithi basi mtoto hata umlelee mbinguni atasala tu.Pili mtoto anazaliwa akiwa na akili tupu(tabolarasa),hivyo ni jukumu lako wewe mzazi kuijaza akili hiyo kile ambacho ni sahihi kwa maisha ya mwanadamu.

Kama utaijaza akili hiyo ugomvi,matukano,uzinzi,na yote yasiyofaa basi kwa vyovyote vile mtoto huyo atakuwa asiyefaa hata umlelee whitehouse.Tatu mtoto anaharibiwa na mazingira anayoishi pamoja na watu anaokutana nao,hivyo ni jukumu lako kama mzazi kujenga ukaribu na mtoto wako ikiwa ni pamoja na kujua muda wote yuko wapi na anafanya nini na sio wewe mzazi kuwa kama simba,watoto wakikusikia umerudi tu wao mbio kujifungia au kutoka nje ili kukukwepa.

Na unapokuwa karibu na mtoto jitahidi kuelewa ameitumia vipi siku yake na unapoona amekosea jaribu kumrekebisha mapema kwa upendo na upole na si kumrukia kwa makofi na bakora hata kwenye yale ya kuelezana tu.Hivyo basi kwa upande wangu naona sehemu yoyote haina tofauti katika malezi ya mtoto hasa kama unapokuwa makini katika kuwajenga na kuwatunza wanafamilia yako kama ukizingatia hayo niliyo kuambia hapo juu.Dar ni sehemu tu kama zilivyo nyingine kuna wanaoharibikiwa na wanofanikiwa.

Mimi nimezaliwa Dar keko magurumbasi,nimekulia sinza miaka 20 baada ya hapo wazazi wakawa wameshahama sinza na kwenda mbezi beach(yote hiyo ni dar).Mimi nimeweza kuondoka dar na kwenda mikoani ambako niliweza kufanya kazi mpaka nilipopata nafasi ya kufanya kazi nje ya nchi.Sasa hapo ubaya wa dar uko wapi.Kikubwa nachoweza kuwashauri vijana wenzangu ni kuwa makini wakati unapotaka kuwa na mwenzi wa maisha.

Sio unaona kidada kimepaka wanja nakupendeza basi unachanganyikiwa bila kujua tabia zake na ukoo wake.Mwisho wa siku utakuja leta viumbe wasioeleweka humu duniani na kuanza kuilaumu Dar es salaam yetu bila kukumbuka kuwa kila sehemu dunia hii ina wema na wabaya.
 
heshma kwako PM.... kwako wewe familia ni watoto tu? pili naomba usiitazame dsm kwa jcho la miaka 20 ilopita... tatu uschanganye baiolijia ya uzazi na maisha unayokabiliana nayo kila siku.
 
Asante mkuu kwa post yako lakini nadhani nimeelezea vizuri sana na wala sikusema familia ni watoto tu kwani hata mke nimemgusia.Hilo la baiolojia ya uzazi utalikwepa vipi kulizungumzia wakati malezi ya mtoto yameainishwa kabisa(waliosoma education watakubaliana nami)kuwa yanatawaliwa na urithi na mazingira.

Sasa urithi mtoto anautoa wapi kama sio kwa mzazi,mfano mzazi ana tamaa kila akionacho anataka kiwe chake na hiyo ni hulka yake utashangaa vipi akija kuzaa mtoto mwizi.

Na kwa hayo yote mawili nadhani nimeyaelezea vizuri tu naomba uipitie tena post yangu ya kwanza labda utanipata nilichotaka kulenga.Na Dar ninayoizungumzia mimi sio ya miaka 20 iliyopita huo nilitoa mfano tu wa jinsi mimi nilivyokua lakini nina uhakika kabisa hata dar ya leo mzazi ukiwa makini bado kuna uhakika mkubwa wa kulea familia bora na imara kabisa hata kama utaishi Tandale kwa mtogole au mtoni kwa chaurembo.

Kuiona Dar kama sio safe place kulea familia ni sawa na kukimbia kazi ya malezi na kuacha jamii ikulelee mtoto/mke wako, na wewe kama mzazi/mume lazima ukumbuke popote utakapokwenda na mtoto/mke wako kama wewe mzazi/mume hauko makini basi basi wanafamilia yako wana uwezekano mkubwa wa kuharibikiwa kumbuka wa kale walisema lakuvunda halina ubani,kwa hiyo kama limevunda limevunda tu hata uhamie wapi.
 
Kweli Mkuu maisha ya Dar nayachukia sana hata kama unakaa ostabei au masaki

Kwanza foleni - inabidi uamke 12 kasoro ili uwahi kazini
Pili watoto mfano wa chekechea utawaonea huruma wakiwa nndani ya daladala wanarudishwa home wote wamelala
kisa wanakurupushwa asubuhi mno

Ukiwa dar kama kuna ulichosahau nyumbani huna hamu ya kurudi nyumbani maana foleni itakuchakachua mpaka ukome

Kwa wenzangu waliopanga ushwahilini wakajitahidi kuwa na ka usafiri lazima ukapaki sisem ukiwa wa kwanza kuegesha
utakuwa wa mwisho kutoka maana ushazuiwa

Huku mkoani aah poa tuu maisha yanaenda traaatibu ila mzunguko wa pesa mdogo!!!!!
 
What you have said ndo ukweli mtoto anaweza kuwa na tabia mbaya hata kama angezaliwa Mbeya ,Mwanza ,Mtwara na kwingineko.Ninachoshauri ni kuwa tusiwaachilie watoto wetu wawe wanaiga vitu ambavyo si katika taratibu za mila zetu kwa mfano mtoto wa kiume anatoboa sikio na kuvaa hereni! Haya mambo yanaigwa tu kutoka tamaduni za wenzetu na hasahasa kutokana na tekinolojia ya habari na mawasiliano kufika kila sehemu! Vijana wakike na wakiume wanaharibika sana kwa kuiga tu!
 
Baada ya kuishi kwa miaka ya kutosha Dar es salaam... baada ya kuchakachua na kuchakachuliwa na maisha(katika anga zote unazojua)...nadiriki kusema..DSM HAIFAI...HASA KWA MAISHA YA KULEA FAMILIA/NDOA..

Uongo?:thinking:

Dar umekuwa mji wa biashara tu sasa na hapa nazungumzia biashara zote ..........:yield:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom