pongezi kwa wizara ya utalii

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wana Jf
naomba niipongeze serikali yetu ya Tanzania kwa kazi nzuri inayo ifanya kutangaza mbuga zetu nchi za nje,nalisema hili baada ya kuona mabango wakati naangalia mechi kati ya sunderland na tottham leo usiku,kwani niliona bango lililoandikwa WWW.VISIT SERENGETI IN TANZANIA,kwa kweli ni mwanzo mzuri na kama tutajitanuwa kimatangazo kwa mtindo huu bila kuogopa gharama Tanzania itakuwa inajizolea mamilioni ya watalii kutoka ulaya na hii ni kutokana na matangazo kwani mala nyingi tunasikia wahenga wakisema biashara ni matangazo

pamoja tutajenga
 
Waziri wake ndiye Ezekiel Maige? Naona kama huyu bwana at least anajua anafanya nini maana anazunguka sana kweny mambo yanayohusu wizara yake!
 
UNAWEZAJE KUWAALIKA WATALII KUTEMBELEA TANZANIA KUONA SERENGETI NA WAKATI HUO HUO UNAJENGA BARABARA KUU YA KIBIASHARA (UKIDAI KWA KUWA KIPANDE KIDOGO CHA KILOMETA 54 HAKITAWEKWA LAMI) KUKATISHA SERENGETI - UKIJUA FIKA KWAMBA BARABARA ITAHARIBU UOTO ASILI, NI HATARI KWA WANADAMU NA WANYAMPORI (KIVUTIO KIKUU CHA SERENGETI)?

WANANCHI WA LOLIONDO (nk) WANATAKA BARABARA NZURI ZINAZOPITIKA KUELEKEA ARUSHA. WALE WA MUGUMU (nk), PIA WANATAKA BARABARA NZURI ZINAZOPITIKA KUELEKEA MUSOMA/MWANZA. HAYO MAENDELEO SERIKALI INAYOSEMA YATALETWA NA BARABARA ITAKAYOUNGANISHA MIKOA YA ARUSHA NA MARA NI LAZIMA YALETWE KWA KUFYEKA SERENGETI NATIONAL PARK?

TAFAKARI KABLA HUJAANGAMIZA!
 
Nadhani pongezi ni kwa TANAPA sio UTALII.

Ila usiulize wametumia kiasi gani.
 
Ninachojua mm kuna mbongo mmoja anaishi na kufanya kazi UK, ndio alieanza huu mkakati siku nyingi akiomba FA nafikiri na wadau wengine wa soka UK hadi akakubaliwa na ndio serikali ya Tanzania ikaingia. Kimsingi sio jitihada za serikali ni za mtu tu kama ww au mm.. Mwisho wa siku mapato km mjuavyo wanakulaga tu hawa CCM.
 
Back
Top Bottom