Pongezi Kwa WILLIAM MALECELA kwa Kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wa Wazazi kata ya Kivukoni

mkuu willy hongera sana ts a good start ila this time kua kiakili na kifikra pia kimatendo, kuwa na nafasi kama hyo ni kubwa ba yaweza kukupeleka mbali sana endapo utaaamua kujituma kwa hekima na busara. kila la heri
 
William Ana ban kutokana na zile thread zake za Nyerere

Ahsante mkuu nilikuwa sijui kama katandikwa ban! Inabidi modes watuwekee sticky thread kutuhabarisha nani kapigwa ban na kwa nini ili watu tiwe tunajua wenzetu ambao wana ban; isiwe siri.
 
Kwa ababu
si kweli kwamba wana nafasi na si kweli kwmba wanaweza simama wenyewe katika maisha yao.
Ukweli ni kwamba
ni wababaishaji watu waishio kiujanja ujanja na hila nyingi za ubabaishaji wa hapa na pale.
Ni watu tegemezi na hata pengine ni makupe wakubwa wanyonyao usiku na mchana.

Msukumo mkubwa katika kutafuta nafasi za kisiasa ni matumbo yao ,Njaa zao na kujikweza


Swali ambalo huwa najiuliza kwa nini watu ambao wana nafasi ya kusimama wenyewe katika maisha wanahangaika na kutafuta kwa udi na uvumba nafasi za uwakilishi? Kuna nini huko? Ulaji?
 
Mkuu Ritz unamuongelea Saggaf Diwani wa Mchafukoge (90% ya watu wanaoishi Dar hawajui hii kata iko wapi!) ambaye aligombea Umeya na Dr. Masaburi.

Mkuu hii ndo mitaa ya mkate wangu wakila siku.
 
Last edited by a moderator:
Safari ya kisiasa huanza kwa kuaminiwa na kuchaguliwa; ndio mwanzo wa safari hiyo... congrats!!!

mkuu mbona unamu-joke nyumbanyingi?kuna watu wa kupongeza lakini huyu janga sasa alikuwa segerea mara kigamboni?wanasiasa kama hawa wanaosaka vyeo kwa hali na mali ni hatari sana,huyu na wakumkemea na kumuseta kuzimu kama ibilisi ni disaster kama baba yake.
 
Yaweza kuwa ni makazi yake mapya. Katiba/sheria za Tz hazimzuii mtu kuishi popote hapa nchini. Hongera kwanza kupiga hatua.
 
Mkuu Ritz unamuongelea Saggaf Diwani wa Mchafukoge (90% ya watu wanaoishi Dar hawajui hii kata iko wapi!) ambaye aligombea Umeya na Dr. Masaburi.

Mkuu kweli hiyo kata watu wengi hawaijui.
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa kuchaguliwa.

Najiuliza naomba jibu lako jana Star Tv na baada ya kipindi cha Tuongee Asubuhi ulimshambulia sana Myika Mbunge wa Ubungo kusema Rais Kikwete ni dhaifu, inaonekana ulivyokerwa sana na kauli hiyo. Hujazungumzia Mwigulu alivyochana Maoni ya bajeti ya upinzani hata chembe hiyo inaonyesha ulivyokuwa kwenye maandalizi ya kutafuta kura za jana.

Lakini ninapohitaji kujibiwa ni kauli iliyotolewa na Mzee wako John Ara Malecela akiwa Waziri Mkuu (GO TO HELL) unaichukuliaje kauli hiyo kutuambia Watanzania wakati huo, pia kuna kauli nyingine ilitamkwa na Waziri kuwa (MTAKULA NYASI).

Lakini kuna wakati ulizungumza Mh. MBOWE kutumia gari la kifahari na ukamuona kama anakiuka maadili, ukasahau kuwa Mzee wako tangu astaafu anatumia magari ya kifahari pamoja na walinzi mbona hujafunguka kwa matumizi hayo au kwa kuwa yapo kwenye familia yenu MVUMI? Watz tunajua mengi sana juu ya familia zinazotumbua maisha huku sisi tukiwa hoi, Ndugu yangu wewe endelea kutafuta uongozi lakini jua ukitaka kula na kipofu........ au Ndio kusema NYANI HAONI KUNDULE?

Msimamo wako wa jana kwa Mbunge wetu haukuwa wa Mantiki maana tulio wengi tulikuwa tunashuhudia bungeni siku hiyo, lakini kwa kuwa katiba inaruhusu ulitoa mawazo yako, funguka kwa kauli ya MZEE WAKO.
 
Si kunakiupindi niliskia akisema ni mkazi wa segerea, naalijindaa kugombea jimbo iwapo makongoro angeshindwa kesi

hapo sasa..na alikuwa akimtetea makongoro kwamba ni mbunge wake..leo anasema mkazi wa kivukoni..kesho tutackia kawe mara kibaha..kweli huu ni upu..uzi wa ccm...
 
William Ana ban kutokana na zile thread zake za Nyerere
Hao jumuia ya wazazi waliomchagua Willy naamini msimamo wao kuhusu Nyerere +ve jee wanafahamu msimamo wake na familia yake juu ya Nyerere?
 
Huyu jamaa hanauwezo wa kuwa kiongozi. Tabia zake ni tofauti na nilivotegemea. Hebu pitia post zake kwenye fb ndo utajua huyu jamaa hamnakitu.
 
William, watu tunapenda kujua ukweli kuhusu wewe. Kwako ni wapi kati ya Segerea na Kivukoni/kigamboni? Inanipa tabu kuwa na imani na wewe zaidi ya kukuona mbabaishaji na mganga njaa. Hutaki unafiki wakati wewe pia ni mnafiki?

Watu wa Segerea watakuelewa vipi? Umeonesha wazi kwamba unatafuta uongozi kwa hali na mali, je unataka kulifanyia nini taifa ambacho baba yako alishindwa kufanya?

Je hicho unachotaka kulifanyia taifa ulishawahi kumshauri ama kumwambia baba yako alifanyie taifa?

Kwa ushauri wangu naona kaombe kazi mission to seaman pale kurasini ama endelea na blog yako ya the udakuz.
 
Time will tell labda kaka Willie ameona walipokosea wazee wetu kwa anashauku ya kujarekebisha makosa
 
Back
Top Bottom