Pongezi kwa jeshi la polisi na Kamanda Kova

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Majambazi NMB Temeke yanaswa

• Yumo askari wa JWTZ kikosi cha Mgulani

na Sophia Maghembe



SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kutangaza donge la sh milioni 5 kwa watakaofanikisha kutiwa mbaroni kwa majambazi waliovamia Benki ya Taifa ya Microfinace (NMB), tawi la Temeke, jijini Dar es Salaam, tayari watuhumiwa 13 wamekamatwa kwa nyakati tofauti.

Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi, Suleiman Kova alisema, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, akiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ). Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na magari manane pamoja na bunduki mbili.

Aliongeza kuwa, walikuwa na bastola moja na SMG iliyoporwa kwa polisi mmoja siku ya tukio.

Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari wa JWTZ SGT Mathew (42), mwenye namba MT 55935, mkazi wa Kibaha, Musa Abdallah (30), mkazi wa Yombo Buza jijini Dar es Salaam na Obadia Gabriel (23) waliokufa katika mapambano na polisi wakati wakijihami.

Wengine waliokamatwa ni Antony Jeremia (30), mkazi wa Dodoma, Issack Swai, maarufu kama Fataki (23), Deogratus Masawe (30) ambao ni wakazi wa Moshi, Salum Yasin maarufu kama Jibaba (28), Yusuf Rajabu (44), Boniface Joseph (34), Japo Salimu (27) na Saidi Hamisi (30), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa, watuhumiwa wawili ambao hakuwataja kwa majina kwa sababu za kiupelelezi, mmoja yupo Arusha na mwingine Kigoma.
Wengine wawili wapo Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam ambapo magari yote yatafikishwa jijini Dar es Salaam kwa utambuzi kujua wamiliki wake halali.

Alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili, na wengine wawili ambao hawajatambulika, watatambuliwa hivi karibuni katika gwaride la utambulisho baada ya upelelezi kukamilika.
Katika tukio hilo, majambazi saba walivamia benki hiyo na kurusha mabomu matatu ya kutupwa kwa mkono na kuua mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi, Seif Mwikwike, kujeruhi wengine wanne na kupora sh milioni 60.

Source: Tanzania Daima
 
Hivi watafanikiwa kuwafunga??!! Au ni kutuzuga tu!! Naomba mwenye taarifa ya maendelea ya ile kesi ya uporaji NMB pale mataa ya ubungo atudondoshee hapa. Kulikuwa na kesi ya wizi pale kisutu na ile ya mauaji mahakama kuu. Ile ya wizi kisutu nasikia walipatikana na makosa ya kujibu. Je hukumu je?? Na ile ya Mahakama kuu April 2009 kulikuwa na hearing, je imekomea wapi hatujui. Hivi ni kweli kuwa wenye feza hawafungwi!!! Labda kweli!!! I am kiding!!!!!
 
Hivi watafanikiwa kuwafunga??!! Au ni kutuzuga tu!! Naomba mwenye taarifa ya maendelea ya ile kesi ya uporaji NMB pale mataa ya ubungo atudondoshee hapa. Kulikuwa na kesi ya wizi pale kisutu na ile ya mauaji mahakama kuu. Ile ya wizi kisutu nasikia walipatikana na makosa ya kujibu. Je hukumu je?? Na ile ya Mahakama kuu April 2009 kulikuwa na hearing, je imekomea wapi hatujui. Hivi ni kweli kuwa wenye feza hawafungwi!!! Labda kweli!!! I am kiding!!!!!


Watafungwa vp wakati wabunge wakienda bungeni wao ni kuongea ufisadi mpaka wanasahau kutunga sheria za ufisadi na ujambazi huku polisi wetu wakiuawa bila makosa. Hapa ni jambo la kisiasa lahitajika to put policies in force, kutunga sheria au kuweka vizingiti vya sheria hizo na siyo kuwanyima au kuweka dhamana ngumu kwani linajitokeza sana kwenye kesi nyingi kwa muda wa miaka ya hivi karibuni.

Yatakiwa itungwe sheria inayokndamiza haswa na ndiyo maana wezi watoka kenya na kwingineko kwani bongo shamba shakua la bibi.
 
Kwa kweli hata mimi nacho kiona ni bunge kuwa busy na mambo mengine na kusahau kutunga sheria kali dhidi ya majambazi na wezi wengine, wauaji albino n.k.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom