Pombe tunazokunywa jamanii! Zitatutoa roho.

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Jumatatu asubuhi nimefika ofisini, punde nikaletewa bahasha kutoka kwa secretary. Bila kuchelewa, nikaifungua ili nisome kilichopo ndani. Kutahamakii Salary increment, nikafurahi kimtindo, nikasign, coppy nikarudisha.


Baada ya kutafakari, nikaona hii siku isiishe hivi hivi. Nikaona nikiwapigia washikaji wanaofanya kazi, watanizungua. Ikanibidi niwatafute washikaji majobless ili furaha yangu itimie. Nikaanza namshikaji wangu wa Upanga aka TBL, kisha nikampigia wa Kigamboni, keko pamoja na magomeni. Nikawaambia kabisa ruhusa kuja na totoziiii. Mida ya saa 11 jioni tukakutana pande za keko, kwa bahati nzuri washikaji wote walikuja single. Kwa utashi wangu nikafaamu mwezi dume January, ukiwa na mtoto alafu kilaji kinalipwa na njemba, unaweza mkuta mwana sio wako mwisho wa siku.



Round zikaanza, ya kwanza, pili, tatu, nne, tano sijui zilifika ngapi , sifahamu. Baada ya mimi kulipa bill, nilijichenga nikala kona huyo kimyakimya, huwa atuagi kwa wanaojua. Mungu sio athumani nikafika Stand ya bus. Mara mbagala mwenge ya mwisho hiyo, nikajichoma ndani kuelekea mbezi tangi bovu. Kuingia tu nikaanza kuporomosha matusi kutoka katika kamusi yangu ya tilalila. Nilikuwa naona dunia yote yangu. Mara konda huyo amekuja kudai hela yake, huwa kwa kawaida atuna ubishi kulipa, ile kujiseach pesa mfukoni, holaa, mifuko yote holaa! Daa! Nikakukumbuka nimesahau kuchukua change kwa waiter. Punde, valangati kali likazuka kati yangu na konda.



Baadae kidogo valangati likawa limeisha, kufika magomeni naitafuta mkwajuni, usingizi huo. Punde nilisikia kitu kama chuma kimenipiga kwenye paji la uso, kumbe konda kaninyuka ngumi ya kisawasa, akili yangu ikanituma gari imepata ajali. Katika yali ya kutaka kusave, kuruka dirishani, nilijibamiza kwenye uzio wa kati ya kiti cha dereva na abiria. Nilikaa katika siti ya nyuma ya dereva, wanao fahamu ma DCM wanajuja palivyo. Nikapasuka vibaya juu ya shavu karibu na jicho, kutahamaki shati limelowa damu balaa, kufika mkwajuni walinishusha kama wananipa huduma ya kwanza, punde sikuliona gari tena. Bahati nzuru nilikuwa aliwatani kidogo maeneo hayo ya mkwajuni na Moscow.



Jamaa moja aliniona akanipeleka kwa mshikaji wangu Moscow, haduma ya kwanza kupewa, waliniwekea spirit ili damu ikome kutoka, Walahii pombe ilikata stimu. Jumanne asubuhi niliamka na maumivu makali mno, sura imevimba, nikapelekwa hospital, nikapewa uduma na kupumzishwa. Nikatoa taharifa kwa ndugu na jamaa na marafiki kuwa nimepata ajali ya gari na marafiki zangu usiku. Kwa sasa nipo nyumbani, naugulia ongezeko la mshahara.



Pombe, pombe, Why me?
 
daah!kama hii story ni ya kweli then usije ukarudia tena.wanywaji wazoefu huwa hatunywi viwanja vya mbali tukiwa alone, bodyguard muhimu mkuu.wapenda sifa huwa wanapenda sana kuzingua walevi so unaweza kuumia kirahisi sana ukiwa umelewa na uko pekeyako.otherwise ugua pole
 
Sorry, ulipasuka chini ya jicho au macho yalihama kabisa kama unavoonekana??
 
1+1=2 lakini kwa walevi huweka 1.
Utakuta jamaa siku nyingine atarudia kulewa kama hajui nini madhara yake.
Halafu unaleta hiyo habari humu tuijadili.
Ugua pole!
 
This is what my friend sent me:

We do not choose to be born. We do not choose our parents. We do not choose our historical epoch, the country of our birth, or the immediate circumstances of our upbringing. We do not, most of us, choose to die; nor do we choose the time and conditions of our death. But within this realm of choicelessness, we do choose how to live.
 
Acha pombe mrudie Mungu wako. Ila huwa nasikia wanasema pombe si chai au??
Halafu wewe unaonyesha si mzoefu
 
Siku ukitaka kunywa jaribu kuwa na tahadhari au kunywa mitaa ya nyumbani maana inaonekana huziwezi
 
Hahahahaha..Umenikumbusha mbali sana kipindi nilipokuwa mwanachama wa TBL natoka ubungo nazifata popote pale nitapopigiwa simu +kitimoto..ukiniambia twende kwenye mambo ya msingi nakataa..lakini TBL nakwenda..usiku vituko home....hahahaha..

Kwa wale wako kwenye nchi zilizopitiliza unakwenda.., naked dance club..lol you become crazy for fun.HAAHAHA

Now i thank God i'm saved

SOLUTION:STOP IT.uache kwa kumaanisha na washikaji wambie umeacha,,utaweza.next next time you will die..na tutakumiss JF
 
pole sana ndugu

samahani pia nina ombi kidogo,unaweza badili avata hiyo?...sio lazima
 
5408309.jpg pomb 4.jpg pombe.jpg pombe6.jpg pombe 3.jpg pombe 4444.jpg pombe (2).jpg pombe (3).jpg wanawake_pombe (1).jpg wanawake_pombe (2).jpg
pencil.png
 
Back
Top Bottom