Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Kuna rafiki yangu kaniambia kuwa mkewe amemuomba watengane vitanda kwa kuwa mama hataki harufu ya pombe na sigara. Rafiki yangu hataki kufanya hivyo kwa kudai ndoa ni kuvumiliana; na zaidi kuwa walipooana miaka 10 iliyopita pombe na sigara halikuwa tatizo; isipokuwa kuanzia mwaka jana ambapo mkewe alimpokea Bwana Yesu na kuyaacha ya kale. Rafiki yangu anasema yuko tayari kuoa mwanamke mwingine badala ya kuacha mazoea yake au kulala vitanda viwili wakiwa wanandoa.
Mnawashaurije wanandoa hawa?
Mnawashaurije wanandoa hawa?