Shukrani Luteni, hizi ndizo analysis tunzozihitaji kwa kweli. Ukiziangalia kwa karibu kabisa, utaona kuwa nyingine zote zinatoa result kwa ukaribu sana, isipokuwa za REDET na wenzao wa Synovate. Naomba Mkuu apewe hizi data ikiwezekana.
Mzee Busara
Huu si utafiti ni average ya tafiti na poll mbalimbali zinazofanyika, average huwa inakusanya data unazozipenda na usizozipenda.
Kama hizi ndio analysis mnazotaka basi mko mbali sana na ukweli.
Kabla hujakubali matokea ya tafiti kuna mambo kadhaa, nitayataja kwa uchache wake, ya kuyazingatia. Pamoja na mengine methodology iliyotumika kwenye utafiti na namba ya watu walioshiriki, kundi la watu walioshiriki n.k. Kama watafiti wote watakuwa wametumia njia (methodology) na statistical analysis moja, hapo matoeka yatakuwa comparable. Zaidi ni kama namba ya washiriki itakuwa almost similar; na vile vile kundi lililotoa maoni. Kama REDET na SYNOVATE waliohojiwa wengi wao ni wapenzi, washabiki, wakereketwa na wanachama wa chama cha Kikwete, basi matokea yanareflect mapendekezo ya walio wengi. Kama hao wengine unaosema wana matokea yanayokaribiana walihoji wapenzi, washabiki, wakereketwa na wanachama wa chama cha Slaa, basi usitegemee kukubalika vinginevyo.
Hata hivyo hizi polls ni perceptions za watu waliofikiwa tu. Wale ambao hawajafikiwa wanaweza kubadilisha ukweli wa mambo kabisa. Hii ni kwa sababu unavyoongeza namba ya sample, ndivyo unavyokaribiana na ukweli wa hali halisi ya jambo linalofanyiwa utafiti.