Polisi yazuia Operation Sangara ya CHADEMA Morogoro kisa hakuna Askari

Ni kweli, wapo polisi wanaotosha kuzuia na kusambaratisha mkutano,sio kulinda
 
sasa mgomo wa walimu unahusiana vipi na mkutano wa chadema.? Ndio tabu ya makamanda kufanya kazi za makada.
 
Kama ni mikutano yote ya ccm na cdm hakuna shida na pia waweke tarehe baada ya nanenane.
 
Chadema hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya hizo operation mbuzi?

wewe umeona ni Chadema peke yao mbona ccm pia wana mkutano Morogoro na kama hujui ni kwamba wana operation yao inaitwa Vua Gwanda vua Gamba vaa Uzalendo. Hiyo ya ccm haivutii ndiyo unaona kama hawafanyi mikutano ila wanazunguka ndugu na posho kwa nape imezua mjadala kuwa makin na chuki zako kwa cdm usiwaonee.
 
Nadhani yuko sahihi kuuliza hinvyo, is too much. Wakumbuke kibaya Chajitembeza na kizuri chajiuza.

This is too much compared to what ? Waacheni wafanye siasa ndiyo kazi ya Chama cha Siasa Kama CCM mnavyo fanya siasa ndani ya Bunge
 
NUKUU YA MWEMA;`Jeshi la polisi linatakiwa lifanyiwe mabadiliko makubwa ili liwe la kisasa kuendana na changamoto za sasa''

kwa hiyo Jeshi la polisi bado la kizamani na wanatumia mbinu za kizamani zisizo na mashiko kwa wakati wa leo.
 
CHADEMA1.jpg


Chadema, Polisi wavutana
Thursday, 02 August 2012 20:52

Joseph Zablon
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeingia tena katika mzozo na Jeshi la Polisi nchini, baada ya mkutano wake uliopangwa kufanyika mjini Morogoro kuzuiwa kwa maelezo kwamba, hakuna askari wa kutosha wa kuuwekea ulinzi.

Pamoja na zuio hilo, Chadema wanasema lazima mkutano huo ufanyike kwa maelezo kwamba sababu zilizotolewa na polisi siyo za msingi na zina ajenda ya kuhujumu kampeni yao waliyoiita ‘vua gamba, vaa gwanda’.

Mvutano huo unatishia amani mji wa Morogoro na viunga vyake, ikiwa Chadema wataendelea na msimamo wao huo, hali polisi wakitumia nguvu kuzuia mkutano huo na mingine midogo katika kata 28 iliyoombwa isifanyike.

Chadema kiliwahi kuingia katika mvutano na polisi katika baadhi ya matukio makubwa ambayo ni pamoja na katika miji ya Mwanza huku mapambano ya jijini Arusha yakisababisha mauaji.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa wamepokea taarifa ya polisi ya kuwataka wasifanye mkutano huo, lakini wao kama chama hawatarudi nyuma.

"Mkutano wetu upo palepale na utahudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa, wakiwamo wabunge wetu wote na utafunguliwa na Mwenyekiti wa wetu wa Taifa, Freeman Mbowe," alisema Kigaila.

Kigaila alisema mikutano hiyo ni ya kukiimarisha chama na inaratibiwa na chama na sio polisi hivyo, kwa jeshi hilo walikuwa wanatoa taarifa na kuomba ulinzi na sio kulitaka liwapangie utekelezaji wake.

"Mkutano ni makubaliano ya ndani ya chama na ajenda yetu ni kuwahamasisha Watanzania kujiunga na chama na ni sehemu ya operesheni Sangara," alisema Kigaila na kuongeza kuwa, maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika.

Zuio la mkutano
Kigaila alisema zuio la mkutano huo limetokana na barua yenye kumbukumbu Namba MRG/SO.7/2/A/219, ya Agosti Mosi mwaka huu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Morogoro kwenda kwa Katibu Chadema wilaya.

Kigaila alisema baada ya kujitokeza hali hiyo aliwasiliana na kamanda wa polisi na walimuomba wafanyie mkutano wao eneo la Mvomero ombi ambalo pia lilikataliwa kwa madai kuwa haiwezekani kutokana na mgomo wa walimu.

"Mara waseme kuna Nane nane, CCM nao wana mkutano Morogoro hivyo haiwezekani, tunapomwambia tukafanyie Mvomero anadai kuna mgomo wa walimu sasa hoja yake ipi hapa tunashindwa kumuelewa," alisema Kigaila.

Alidai ni wazi jeshi hilo linatumika kwa manufaa ya kisiasa kwani yeye anavyofahamu ni kwamba ikiwa kuna vyama viwili vinavyotaka kufanya mikutano yake, basi hupangiwa maeneo tofauti.

"Kama wengine wakipanga eneo fulani basi sheria inataka chama kingine kifanye mkutano wake mita 500 kutoka walipo wenzao,” alisema.

Kigaila alisema mkutano wao huo utafuatiwa na mingine katika kata 28 za mji huo kabla ya kuelekea katika miji ya Iringa, Dodoma, Manyara na Singida na awamu inayofuata itahusisha mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mwanza.

Operesheni hiyo itaendelea katika miji ya Mara, Kagera na Geita kabla ya kurudi kumalizia mikoa iliyokuwa imesalia Kusini na ni operesheni ya kawaida ya kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho

Taarifa ya polisi
Kulingana na taarifa hiyo (ambayo Mwananchi limeona nakala yake), sehemu yake inasomeka: “Rejea barua yako ya Julai 30, 2012 ya kutoa taarifa na kuomba ulinzi kwa ajili ya maandamano na mikutano ya hadhara mliyokusudia kufanya K/Ndege Agosti 4, 2012 na Agosti 5 kwa Kata 28”.

"Katika tarehe zilizoainishwa hapo juu Chama cha Mapinduzi (CCM), wamekusudia kufanya mikutano ya hadhara ya wanachama, wapenzi na makada wao katika maeneo hayo hayo," inasema taarifa hiyo.

Inaongeza kuwa Agosti mosi hadi 10 mwaka huu, maadhimisho ya sherehe za Nane Nane yanaendelea katika Mkoa huo na kama vile haitoshi, katika tarehe zilizoanishwa, mgomo wa walimu wa shule za msingi na sekondari unaendelea nchi nzima.

Sehemu ya taarifa hiyo iliongeza kwamba, kutokana na sababu hizo shughuli zote zinahitaji ulinzi na usalama ambao utasimamiwa na polisi, hivyo kutokana na mgawanyo uliopo wa askari itakuwa vigumu kusimamia shughuli zote kwa wakati mmoja.

"Kwa mantiki hiyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro amesitisha mikutano ya hadhara na maandamano hayo kwa mujibu wa kifungu namba 43 (1-6) cha sheria za Polisi na polisi wasaidizi sura 322 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002," inabainisha barua hiyo.

 
Tanzania Democrasia bado iko mbali kutokana na ukirikimbwa na Udikteta wa Ubaguzi wa Vyombo vya Dola, hivi ccm wakifanya mikutano yao huwa wanaekea vizingiti vingi?.

Hii ni moja ya kuto kupendwa ccm kutokana na kuitumia nchi vibaya na kulazimicha mombo kinguvu, mara nyngi ukiskia mauwaji zidi ya Jeshi la Polisi huja disain hii.
 
chadema hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya hizo operation mbuzi?
we mbona hivi au unafikiri kwa kutumia masaburi?mbona ccm wako kigoma na kwingineko husemi,hutaki bibi yako au babu yako au dada yako wa kijijini ajue ukweli afahamu mafisadi wanavyotafuna nchi hii?jinsi tulivyo matajiri lakin rasilimali yetu inaliwa na wachache,au we na rama inghondu ni ndugu?
 
waulize polisi kule singida walilindwa na nani?CDM nizaidi ya jeshi la polis mwambie kamanda wa polis,kila mpenzi wa CDM nikamanda kwaiyo asiwe na shaka juu ya ulinzi.
 
Chadema hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya hizo operation mbuzi?

Kwani chama cha siasa kazi yake nini ni pamoja na kufanya mikutano hata hao CCM wanaruhuisiwa kufanya hiyo mikutano ila tu kasheshe ni wale wahudhuriaji kama wanaweza kufika kwenye mkutano, Nape si naye anajiandaa kufanya hiyo mikutano na Operation Vua gamba Vua Gwanda Vaa Uzalendo sijui hii itakuwa operation Kondoo au
 
Chadema hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya hizo operation mbuzi?

Mtajibeba wanamagamba kazi ya chama cha siasa ni kufanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujua haski zao huu ni wakti wa CHADEMA kufanya hiyo kazi.ACHA KUWA KAMA:shetani:
 
Back
Top Bottom