Polisi yazuia maandamano ya 'kuunga mkono hotuba ya JK' Dar

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Yale Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kuunga mkono Hotuba ya JK yamezuiwa na Polisi kwa madai kuwa yatasababisha msongamano kwenye barabara watakazopita.

Nauliza:
Polisi/CCM wameshtukia nini?
Je! Ni ujanja wa kuja kuzuia maandamano yenye tija kutoka Chadema kwa sababu hiyo hiyo?
 
maandamano hayo yasingefanikiwa na yangekuwa ni aibu kubwa sana kwa serikali na rais .... hivyo wamepotezea kwa kisababu cha polisi
 
Walikuwa wapi siku zote kuandamana mpaka waje na wazo hilo leo? Tangu JK atoe hotuba ni muda mrefu sana hata hivyo hotuba yenyewe haina tija kwa taifa zaidi ya kueleza vitu visivyotekelezeka.

Polisi wangewaacha tu waandamane tuone nguvu yao ipo wapi kama si kukodi watu kwa kuwalipa ili waandamane.
 
Hayana tija afadhali yamezuiwa.Tumechoka na maadamano ya kupongezana ujinga na kupoteza muda tu hongera polisi kwa kuona hilo
 
sababu za kiintellejesia teh! wamesitisha wakitaka kutuhadaa wapo nyutro kwa vyama vyote!
 
ya kwetu CDM tutafanya usiku hakuna msongamano yataanzia manzese, mbagala, bunju, kibamba, kigamboni mpaka karimjee!jk akiamka asubuhi akute tupo tayari ikulu
 
tunaomba wawaachie waanamane kama ni foleni waanzie magomeni to mazense ikishindikana hataa wafanye public rally, tunataka kuwaona maadui wa umma kwa sura zao
 
Wangeachwa waandamane kwani ni haki ya msingi kama tatizo ilikuwa route si wangeshauriana na polisi then wabadilishe route? Na vipi gharama walizotumia?

Mimi nafikiri kuna namna hapa ikiwa polisi waneweza kuzuia maandamano ya kikundi kisichokuwa na impact kwa sababu nyepesi 2 ya foleni namnagani maandamano ya CDM ambayo yatavuta idadi kubwa ya watu nafikiri pana tatizo.
 
Wanahofia maandamano ya Chadema. Hivyo siku Chadema wakiomba kibali watakataliwa na kuambiwa hata CCM tuliwakatalia.
 
maandamano hayo yasingefanikiwa na yangekuwa ni aibu kubwa sana kwa serikali na rais .... hivyo wamepotezea kwa kisababu cha polisi
Hii ndio wameshtukia........!

Je! Ni ujanja wa kuja kuzuia maandamano yenye tija kutoka Chadema kwa sababu hiyo hiyo?
Na hii ndio ilikuwa target yao kwa maslahi yao.......! Shame on them.....!
 
wameambiwa kuwa hawatapata waandamaji wakakwepa aibu? au huenda Dr. augustine mrema kashtuka, si mnajua yule mzee ni kinyonga? kesharudi loliondo?
 
wameambiwa kuwa hawatapata waandamaji wakakwepa aibu? au huenda Dr. augustine mrema kashtuka, si mnajua yule mzee ni kinyonga? kesharudi loliondo?

karudi leo saa nane atakuwa Bahkresa manzese akiwadanganya wajinga.Yeye ndiye main speaker wa huu mkutano wa ccm na wake zake cuf,nccr
 
Hii ndio wameshtukia........!


Na hii ndio ilikuwa target yao kwa maslahi yao.......! Shame on them.....!
ila nadhan hayo maandamano kwa upande mwingine yangeongeza chuki dhidi ya serikali so yangeibeba CDM dats why yamepigwa stop.

Personaly nlitaka waandamane tena wabebe mabongo yakumsifu JK na Pinda.
 
Duh! Kweli Jf kuna great thinkers jana kuna mtu alitoa híi kwamba yatazuiliwa na polisi naona yamekosa watu, vijana wamechukua chao af wakaingia mitini.
 
Wajanja hao, wameshtuka! Ingekuwa ni aibu ya karne. Nguvu ya umma ingejibu mapigo ndiyo wangeona cha moto. Kikwete anashindwa kutamka hadharani tu lakini ukweli ni kwamba hana raha na jinsi wananchi walivyomchoka.

Hata wakitumia propaganda za maandamano ya kuunga mkono hotuba yake haitasaidia kitu kwani hata wanaccm wenzie wamemchoka.
 
Vijana wa CCM wameahirisha maandamano ya kumuunga mkono JK baada ya kuzuiliwa na polisi kwa madai kuwa maandamano hayo yatasababisha usumbufu kwa watumia barabara ya morogoro.[Mbona kampeni za uchaguzi hawakuzuia?!!].

Hawa vijana wakamalizia kwa utamu zaidi walipomualika mrema kuwa mgeni rasmi!

Kule Kigoma Mbatia na Lipumba wameungana kupambana na CDM. Kwa hayo mapambano ya anga na ardhini kutoka kona zote za nchi, CDM mtatoka?

CCM WONT SLEEP, CCM WONT EAT, CCM WONT LISTEN AND CCM WONT STOP UNTILL THEY BRING YOU DOWN........... THEY ARE AFTER YOU GUYZ AND YOUR ONLY SURVIVAL IS STOPPING BEING CHASED RATHER CHASE THEM!!!!
 
Si kwamba maandamano yamezuiliwa ila waandaaji wameshutukia baada ya kuona hawatapata vijana wa kuandamana maana vijana wa kukodisha wangetakiwa kulipwa jana ili leo ndo waandamane, baada ya utafiti ikagundulika vijana walikuwa wanataka hela tu na wasingetokea kwenye maandamano. Kuondoa haibu wakasingizia maandamano kuzuiliwa na polisi kwa sababu ya foleni.

The route was clear from day one na kama ni kuyazuia sababu ya foleni isingelikuwa ya kushutukiza to that extent! Watanzania wa sasa wameamka, pesa watakula na kuandamana hawataandamana. Kwa mkutano itakuwa hivi ukifika kabla ya kuingia mktanoni unapewa posho na kuesikotiwa ili usitoroke mkutano!

Aibu tupu
 
Hawana jipya hao wanaoitwa 'VIJANA WA CCM'. Kwanza siyo vijana wa CCM, ni vijana wa mafisadi. CCM haipo, ilishakufa. Kilichopo ni genge la mafisadi.

Hakuna mtu anayeweza kuandamana kuunga mkono wapambe wa mafisadi halafu akajiita ni 'KIJANA WA CCM YA NYERERE'. Hakuna kitu kama hicho. Wapuuzwe kwani ni watoto wa mafisadi, nao ni mafisadi au ndiyo wako darasani wakifundishwa ufisadi ...
 
Back
Top Bottom