Polisi yazima uchawi bungeni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
Polisi yazima uchawi bungeni


Na Kulwa Mzee, Dodoma

UCHUNGUZI uliofanywa katika sampuli zilizokusanywa ndani ya ukumbi wa Bunge na vumbi lililopatikana katika mashine ya kusafishia ndani ya ukumbi wa Bunge, umebaini hakukuwa na sumu yoyote inayotambulika.

Taarifa hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Kamishna wa Polisi, Bw. Omari Mganga, ambaye ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma.

Katika taarifa yake, Kamanda alisema baada ya sampuli hizo kukusanywa zilitumwa kwa Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, na baada ya uchunguzi hakuweza kuona sumu yoyote iliyotambulika.

“Kwa maana hiyo basi hakuna ushahidi wowote uliopatikana wa ama mtu kuona, au picha za mitambo ya CCTV au wa kisayansi unaothibitisha kufanyika kwa vitendo kama hivyo,” ilisema.

Taarifa hiyo ilisema wakati kikao cha Bunge kilipoanza kulitokea minong’ono kuwa kuna Mbunge na ofisa mmoja walionekana ndani ya ukumbi wa Bunge wakizunguka kwenye viti vya wabunge, huku wakinyunyizia unga uliohisiwa kuwa ni kwa ajili ya kudhuru binadamu au imani za kishirikina.

Ilisema baada ya uvumi huo kuenea hadi kwenye vyombo vya habari, uchunguzi ulifanyika kwa kukusanya ushahidi mbalimbali, watu walihojiwa na hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha kuwa aliona watu wa aina hiyo wakifanya hayo yaliyokuwa yakizungumzwa.

Pia uchunguzi ulifanywa na wataalamu wa Kampuni ya SSTL GROUP wakisaidiana na maofisa wa usalama wa Taifa na Polisi kwa kupitia picha zinazochukuliwa na mitambo ya CCTV ndani ya ukumbi wa Bunge, milango ya kuingilia na kuzunguka eneo lote na Bunge waliona kuwa hakuna kamera zilizozimwa tangu mwaka juzi.

Katika kumbukumbu hizo za picha hakuna iliyoonesha mtu au watu wakifanya vitendo vilivyokuwa vinavumishwa.

Hata hivyo, sampuli mbalimbali zilichukuliwa kutoka katika ukumbi wa Bunge na vumbi lililopatikana kutoka ndani ya mashine ya kusafishia ukumbi huo ambao kama kungekuwa na kitu kilichonyunyiziwa ukumbini Juni 9 mwaka huu na kuendelea, ingesaidia kwa kiwango kikubwa.
 
Back
Top Bottom