Polisi yaendelea kumsaka Nanyaro Mwenyekiti Bavicha mkoa wa Arusha

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Ndugu wanaJamvi
Jana niliongea na afisa mmoja wa ngazi ya juu wa polisi hapa Arusha,katika mazungumzo yetu afisa huyu alikiri kuwa bado polisi inaendelea kumtafuta Nanyaro ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Arusha,alikiri kuwa jana jioni walimtegea maeneo ya December lakini ghafla alipotea kimiujiza,jioni akategewa tena eneo la soko kuu,na polisi walipofika tu akatoweka tena ghafla,hali hii imezua maswali sana kwa polisi,jinsi huyu Nanyaro alivyo na uwezo wa kuwapotea,hali inayofanya polisi kuamini penginne ana mafunzo ya maalum,kingine ni Utii walio nao vijana wa Arusha kwake,inasemekana kuwa Vijana wengi wanamsikiliza sana Nanyaro na wana nidhamu kama nidhamu ya Jeshi.
Kingine polisi wanahofia kumkamata kwa nguvu kwa hofu ya kuzua machafuko,kutokana na huo utii na nidhamu waliyonayo vijana wengi wa Arusha kwa kamanda wao Nanyaro
 
Labda nipo nyuma kidogo samahani,kwa nini anatafutwa na kwa nini wamtegee?kwa nini anawakimbia polisi?je kiongozi anapaswa kufanya hivi?
 
Nipo tayari kuwapelekea Nanyaro iwapo nitaahidiwa kukamilishiwa ujenzi wa kanyumba kangu.
 
Ndugu wanaJamvi
Jana niliongea na afisa mmoja wa ngazi ya juu wa polisi hapa Arusha,katika mazungumzo yetu afisa huyu alikiri kuwa bado polisi inaendelea kumtafuta Nanyaro ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Arusha,alikiri kuwa jana jioni walimtegea maeneo ya December lakini ghafla alipotea kimiujiza,jioni akategewa tena eneo la soko kuu,na polisi walipofika tu akatoweka tena ghafla,hali hii imezua maswali sana kwa polisi,jinsi huyu Nanyaro alivyo na uwezo wa kuwapotea,hali inayofanya polisi kuamini penginne ana mafunzo ya maalum,kingine ni Utii walio nao vijana wa Arusha kwake,inasemekana kuwa Vijana wengi wanamsikiliza sana Nanyaro na wana nidhamu kama nidhamu ya Jeshi.
Kingine polisi wanahofia kumkamata kwa nguvu kwa hofu ya kuzua machafuko,kutokana na huo utii na nidhamu waliyonayo vijana wengi wa Arusha kwa kamanda wao Nanyaro

Tusubili kuambiwa jamaa amefuzu mafunzo ya ujasusi Iraq
 
Polisi inaamini kuwa yeye ndio alikuwa kinara wa mgomo wa daladala,pamoja na hali hii ya Arusha unrest
Lakini pia alinukuliwa na vyombo vya habari akimtaka IGP amfukuze kazi OCD wa Arusha,kwa kuwaita wananchi Panya,na kama IGP hatafanya hivyo basi vijana wa Arusha wasilaumiwe kwa kitakachompata,kauli hii inasadikika kuwa ya kichochezi
 
Tusubili kuambiwa jamaa amefuzu mafunzo ya ujasusi Iraq

kwani hawapajui kwake,kwa nini mamtegee au kumvizia kihuni huni,kwani kamanda nanyaro amekuwa fugitive wa kuwekewa mitego ya kukamatwa.polisi waseme wanamtafutia kosa la kumbabika na yeye nanyaro amekuwa akiruka mitego yao.sitashangaa nikisika nanyaro kakamatwa kwa kosa la kupiga bar,au kuendesha baiskeli mwendo kasi.ili mradi tu wamtie nguvuni.
 
Polisi ni sawa na mbwa.....na hapa namaanisha wooote kabisa.
kwani hawapajui kwake,kwa nini mamtegee au kumvizia kihuni huni,kwani kamanda nanyaro amekuwa fugitive wa kuwekewa mitego ya kukamatwa.polisi waseme wanamtafutia kosa la kumbabika na yeye nanyaro amekuwa akiruka mitego yao.sitashangaa nikisika nanyaro kakamatwa kwa kosa la kupiga bar,au kuendesha baiskeli mwendo kasi.ili mradi tu wamtie nguvuni.
 
Tuna safari ndefu sana kufikia tanzania tunayo itaka lakini kwa mapenzi ya mungu tutafika
 
Nadahani hili wanalikazania sababu mkuu wa kaya-JK atakuwa AR hivi karibuni,sasa kwa kutojiamini kwao wana hofu pengine atahamasisha vijana kuonyesha hisia zao juu ya vitendo vya unyanyasaji na ubakwaji wa haki za raia na hasa viongozi wa Chadema jijini Arusha,au kama sababu ni hiyo ambayo mmeitaja wanashindwa nini kumfuata kwake?na kama kweli anakishawishi kwa vijana na wanamtii sana basi hilo nalo ni tatizo kwa polisi na akili zao mbovu,wanataka kuanzisha vurumai nyingine.
Mtuhabarishe zaidi wakuu mlioko AR
 
kama JK atakua A-Town asipoangalia vizuri yatamkuta yale yaliyomkuta Chuo kikuu kwenye maafali ya miaka 50. Vijana walikosa uvumilivu hivyo si ajabu arusha nako yakawa vivyo hivyo.
 
Mbona hata hajifichi ila wakati wanaenda kumkamata wajipange hawaendi kukamata kuku wa kisasa.....
 
Wanataka tu budget ya mafuta iongezeke, wachakachue.
Watawashika wangapi?
 
Back
Top Bottom