Polisi wetu na sheria mkononi-- picha ya Tundu Lisu

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
lisu tarime.jpg
Kuna sheria moja imefunga watu sana hapa nchini, kujichukulia sheria mkononi au kupiga mtu hata kama amekuibia hivi polisi haiwahusu?
Kumdhalilisha hivi waziri kivuli wa sheria je sisi wengine itakuwaje?
Hiyo ni nguo ngumu lakini wameweza kumpa purukushani mpaka ikachanika, je mbavu zake ziko salama?

Mimi nadhani wananchi kuweke msimamo kama tukiona polisi anapiga mtu au kutumia nguvu kupitiliza tufanye nini?
Wenzetu uingereza juzi wamefanikiwa kuipasua sheria ya kuwawekea kinga kwa njia za mahakama watu wenye majina pale wanapofanya uovu kwa kutumia TWITTER.

Na tubuni mbinu ya kukomesha ukatili wa polisi, hata kama ni kuanzisha mfuko wa kuteteta watu wasio na kipato wanaonyanyaswa na polisi na mahakama tufanye, haki haiji kwa kuremba remba.

View attachment 30758
huyu ndio hafai kapisa hapo anamlisha sumu tu, huyo bwana kaisha zoea roho za watu kumlilia alianza toka akiwa msitini na kupindua serikali sasa kikwete anapochukua ushauri kwa mtu kama huyo mambo kama ya tarime itakuwa kawaida tu.
mpinzani wa uganda kwa sasa kwafungwa kifungo cha nyumbani haruhusiwi kutoka.
tundu lisu kapigwa marufuku kwenda NYAMONGO hayo yamefanya jana, na jana hiyo alikutana ha hiyo dubu
masharti ya LISU kutokanyaga nyamongo yamekaa kiuganda uganda ( museven style)

huko wa msevini maafisa wawili wapolisi kama masawe wameshafukuzwa kazi mpaka sasa, kwa sababu hawakuwa tekeleza amri ya kumfanyizia mpinzani wa mseveni
kwa maana nyingine polisi wakitumwa kwenye tukio hakuna kutumia akili unafanya ulichoagizwa, nadhani hata masawe kafanya huu unyama kulinda kitumbua chake, lakini moya anasimanzi kufunga ndoa ana serikali ya kikwete.
 
Inatia hasira sana kuona kiongozi halali wa wananchi, na mtunga sheria ndani ya bunge la Jamhuri anadhalilishwa kwa misingi ya kichama. Polisi nao imefika wakati watumie hata elimu ya utu wa mtu. Mbunge sio jambazi hawezi kimbia wala jificha, lazima atakamatwa, kwa nini kumdhalilisha ?

Hapo najifunza je kama mti mbichi unawaka moto mkavu utakuwaje? Gharama za kuwa mpinzani ni kubwa, gharama za kuitoa CCM ni kubwa na gharama za kutetea mali za Tanzania ni kubwa mno. Hya wananchi twende kazi.
 
ni kweli kabisa mbunge ni mtu wa kumwambia njoo polisi tunakesi na wewe
na anaweza kuja bila tatizo wangekuwa wanafanya hizi kwa kila mbunge bila kujari chama ningesema wanamafunzo mabovu.
toka kikwete hatoke kwa msevene kumpongeza naona kaanza tena maana Museven ni bingwa wa kudhalilisha viongozi
na hapa wako wote tena kwenye mkutano wa wakuu wa afrika , huu ni muda wa kukaza kamba
 
Nashindwa iona hiyo picha licha ya kuiona link ya "lisutarime.jpg Views. 0 size 43.3 KB"
 
Nampongeza Mheshimiwa Lissu kwa ujasiri, uzalendo, upendo na sadaka kubwa anayoitoa kutetea haki za wanyonge. Haki ya mtu inaweza kucheleweshwa lakini kamwe haipotei. Binafsi namfananisha mheshimiwa huyu na Nelson Mandela ambaye alisema "In my country we go to prison first and then become President."
 
tupo pamoja katika hilo mkuu
 
Waache wachane hayo makombati lakini siku si nyingi hawa polisi watakuwa wanayapigia salute. Mapambano ni pale pale hakuna kulala hadi kieleweke.
 
Amani ya nchi yetu, inahatarishwa na CCM, wamesahau ya kwamba, "THEY CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES, BUT THEY CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME" Itafika wakati wananchi watasema basi, na sijui watatokea wapi..
 
Bado wanahitaji elimu endelevu, Nafikiri mpaka sasa wanaamini mtu anayefanya kazi kwa "nguvu" hata kama kichwani hamna kitu atapanda cheo kama huyo kamanda wao Masawe!!!
 
Mbona hapo haionyeshi akipewa mkong'oto? Natamani sana hao CDM wapewe kichapo cha maana cuz wanatuvurugia amani yetu! Big up Kamanda Masawe, unafanya kaz yako vizuri!
 
Mbona hapo haionyeshi akipewa mkong'oto? Natamani sana hao CDM wapewe kichapo cha maana cuz wanatuvurugia amani yetu! Big up Kamanda Masawe, unafanya kaz yako vizuri!

Anaetaka kukosoa siku zote hatakosa maneno ya kusema,,wa magamba huyu na kipimo chake cha akili ni hiki msimshangae sbb ccm wote vilaza Kama huyu
 
Watawaua sana raia,watawatesa na kuwadhalilisha wale wote wanaokuwa kinyume na udhalimu wao,wataipindisha haki mara nyingi wawezavyo,watafuja raslimali zetu na kutuziba(wanyonge)midomo kwa kutumia polisi lakini wakumbuke kuwa yote hayo yana mwisho na siku yao inakuja.
 
Anaetaka kukosoa siku zote hatakosa maneno ya kusema,,wa magamba huyu na kipimo chake cha akili ni hiki msimshangae sbb ccm wote vilaza Kama huyu
Wangekuwa vilaza wangeweza kuifikisha nchi ilipo? Acha kuropoka tu, shirikisha na ubongo!
 
Watawaua sana raia,watawatesa na kuwadhalilisha wale wote wanaokuwa kinyume na udhalimu wao,wataipindisha haki mara nyingi wawezavyo,watafuja raslimali zetu na kutuziba(wanyonge)midomo kwa kutumia polisi lakini wakumbuke kuwa yote hayo yana mwisho na siku yao inakuja.

Utangoja sana! CCM na mikakati yake mizuri itaiongoza Tanzania milele!
 
Wangekuwa vilaza wangeweza kuifikisha nchi ilipo? Acha kuropoka tu, shirikisha na ubongo!

Kwa hiyo miaka 50 watoto wanakaa chini mpaka vodacom waisaidie Serikali ndio unaniambia niushirikishe ubongo wangu?Mimi na wewe nani anaropoka yaani wewe unautetea ujinga juu ya ujinga mwingine!!!!?
 
Utangoja sana! CCM na mikakati yake mizuri itaiongoza Tanzania milele!

Mawazo ya wenye uchu wa madaraka yanafanana na yako kwa kutaka kutawala milele,siku ikifika nntakutafuta mpaka uchochoroni usikimbie.
 
Back
Top Bottom