Polisi wazuia mikutano ya Chadema nchi nzima; Chadema wamekubali?

Hii nchi ya kipimbi sana... kwa style hii hatutaendelea kamwe!

kama vip tujikusanye na tuingie barabarani tu kwani kibali kitu gani bana?:disapointed:

Huyu mia kwa mia hayupo Tanzania, usiwaponze wenzako kwenda kula mkong'oto wa vichaa FFU.
 
Huyu mia kwa mia hayupo Tanzania, usiwaponze wenzako kwenda kula mkong'oto wa vichaa FFU.


Una uhakika? nipo sana hapa nasikilizia joto na mgawo wa umeme! hao FFU kuna siku watatukimbia nakwambia... ujue uoga bado umetutawala ila ipo siku mishipa ya uoga itakapokatika ndipo hata FFU watatamani kutujoin kwenye maandamano
 
Una uhakika? nipo sana hapa nasikilizia joto na mgawo wa umeme! hao FFU kuna siku watatukimbia nakwambia... ujue uoga bado umetutawala ila ipo siku mishipa ya uoga itakapokatika ndipo hata FFU watatamani kutujoin kwenye maandamano

Unaweza kutumia mbinu za amani kutaka mageuzi si lazima kuanza kushindana. Taratibu ndio mwendo.
 
Unaweza kutumia mbinu za amani kutaka mageuzi si lazima kuanza kushindana. Taratibu ndio mwendo.


Kwani maandamano si mbinu za amani? kwa nini wawanyime wananchi haki ya kuandamana ambayo ni haki ya kila mwananchi kikatiba?
 
Wangekuwa wameshinda kihalali, wasingezuia. wakiendelea kukataa, inabidi tulazimishe tupaze sauti zetu. Hata madikteta hawakutawala milele
 
Sasa hii kazi ipo.!!!!!!! Watoa vibali kwa ajili ya mikutano ya CDM wote wanatoka au kuteuliwa na chama tawala, hapa CDM isitegemee fair play. Namnukuu Seif Hamad alivyosema miaka ile" CCM haiwezi kuachia madaraka kupitia kwenye vipande vya karatasi vya kura, labda njia nyinginezo" .
Najua kabisa kuwa CDM mna ushahidi tosha wa kuwafumbua macho watanzania wizi uliofanywa na CCM na wanaamini kabisa kuwa wakiruhusu mikutano ya hadhara, basi watanzania watafunguka macho na kuingia msituni. Tafuteni njia nyingie, vibali havitatoka hata kwa dawa.
 
Ni Kweli Chadema Waliomba Ruhusa Wakanyimwa au Tunafikiria Chadema Walinyimwa Bila Ushahidi. Uwezi Kupata Kibali cha Mkutano TZ Kipindi cha Kampeni Kikipita ila Sheria Zipo za Kudai Maandamono Hata Mikutano, Jeshi la Polisi Watahakikisha Wanazuia Haya. Tuone Kama Chadema Wanaweza Kuomba Hivi Vibali. Ni Lazima Waombe na Wanasheria Wao Wafanye Kazi ili Kuonyesha Sababu za Mikutano ni Nini. Tunasubiri Chadema...Hii Approach Inaweza Ikawa Hatari kwa Sasa. Wananchi Wana Hasira Sana Sasa.
 
Taarifa rasmi zilizotolewa kwenye vyombo vya habari jana na leo vimeifahamisha jamii ya watanzania wenye mapenzi mema na Tanzania kutofanya mikutano ya hadhara na wameapa kutotoa vibali vya kutoruhusu mkusanyiko wa wa wananchi wanaokubaliana na sera chadema nchi nzima.



jamani wa jf-
  1. wametumwa na nani hawa?
  2. wana mpango gani na nchi ya tz?
  3. kauli hiyo ina madhara gani kisiasa?
 
Niungane na Mhariri wa Gazeti la Mwananchi kuhusu hatua ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini as a pretext ya kuzuia uvunjifu wa amani.

Mimi nadhani huu ni uzandiki unaoendelea kutamalaki katika jamhuri yetu ambapo ukiukwaji wa sheria na viongozi umekuwa business as usual.

Sheria inayosimamia vyama vya siasa iko wazi.

Rights and privileges of, and meetings of, political parties Acts Nos. 1 of 1993, 32of 1994 Sch.

11. -(1) Every party which has been provisionally or fully registered shall be entitled

a) to hold and address public meetings in any area in the United Republic after
giving notification to the police officer in-charge of the area concerned for
purposes of publicizing itself and soliciting for membership;

b) to the protection and assistance of the security agencies for the purposes of
facilitating peaceful and orderly meetings:

IGP Mwema anatumia sheria ipi kuhalalisha agizo lake?

Ni huzuni isiyo mithilika kuona tuliyempa mamlaka ya kuilinda na kuhifadhi katiba, na kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi kama zilivyopitishwa leo anathubutu kuzipindisha bila aibu na hiana kwa kisingizio cha kujenga hofu kwa wananchi kwa mazingira ambayo yumkini hayapo. Kwa mtanzania mwenye akili timamu, anaposikia hali si shwari nchini bila shaka atawaona wenye kuchochea uvumi huo ni wendawazimu au pana walakini katika kufikiri na kuona kwao.
 
Ni jambo lililowazi kuwa wakubwa hawa wa polisi wameligeuza jeshi kuwa mwambata wa ccm.Na wapo katika nafasi hizo si kwa ajili ya maslahi ya taifa bali ni kwa ajili ya maslahi yao,waliowateua na ndugu zao angalia jinsi IGP said mwema alivyomchakachua RPC basilio matei na wenzake baada ya mwambata wao mkubwa ccm kushindwa katika maeneo yao.Mwema ni muumini mkubwa wa vurugu ili kuipatia ccm ushindi.Nilikuwa namuamini kama mtu makini lakini sasa wote lao moja!
 
toeni tssrifa zenye uhakika pls? hiyo kauli ni kweli imetolewa? ni sababu zipi zimepelekea kutolewa kwa kauli kama hiyo?
 
Mambo ya katiba, nadhani siku zijazo baada ya marekebisho ya katiba itabidi awe anaidhinishwa na bunge baada ya uteuzi wake
 
Hapa swali si udhalimu wa CCM na jinsi wanavyotumia vibaya nguvu za dola, haya yako wazi.

Swali ni, wananchi wa Tanzania, hususan kwa kuongozwa na CHADEMA katika kisa hiki, wamejitolea kufanya nini kuondoa udhalimu huu?
 
Back
Top Bottom