mkomatembo
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 1,477
- 816
Huyu Ndugulile hajui analoliongea na siamini kama wapiga kura wake watamuunga mkono katika hili. Lazima atambue kuwa mama Tibaijuka japo yuko CCM ni mtu mabye anakubalika sana katika jamii nzima ya Tanzania na dunia kwa ujumula. Sioni mantiki ya kuzuia mradi ambao umedumu miaka zaidi ya 4 na sas tumepata Jembe, mama Tibaijuka ambaye katumia kila mbinu kukoa mradi ambao ulikuwa unaelekea kufa.
Nina mashaka kwamba huenda Mr.Ndugulile ametumwa na baadhi ya mafisadi wachache walioko huko kigamboni ili waendelee kuuteka na kuutawala mji huu wa Kigamboni kwan wao wameshajinyakulia maeneo kadhaa kwa njia isiyohalali ya kuwaonea wanyonge.
Hujui unachoongelea , huyo mama yako tibaijuka ndio fisadi nambari wani na huyo mpuuzi mwenzake alieanzisha huu mradi.
Kwa taarifa yako wakaazi wa Kigamboni majority labda nikufahamishe 99% HAWAUTAKI huu mradi, sasa sijui wewe umetoa wapi haya majibu! hebu fanyeni kura ya maoni ndio utakapobaini hili.
Tunafahamu kuwa Dar es salaam sasa maeneno yote yameisha, na mawaziri wanazaliwa wapya kila siku, leo tunasikia Kigamboni na Bwagamoyo esho wakizaliwa marais wa kipindi kijacho tutasikia Kongowe, mpak kwendea mbele. tunajua watu wa pwani tunaonewa kila kukicha na kinachotuponza ni bahari.
wameona maeneno yameisha sasa wanataka kuja kuipora Kigamboni wagawane viwanja, tunasema kwa kinywa kipana MRADI HATUUTAKI! mimi ni CCM damu ukiikata damu yangu inatoa chembe chembe za kijani, lakini MRADI HATUUTAKI, na wasipoangalia wasubiri nini kitatokea, wajue kuwa watu wameamka sasa sio enzi za ujima hizi na za nyerere watu wamesoma na wameenda shule na wameelimika.
Mwambie huyo mama yako kama amekutuma kuwa atafute sehemu nyingine ambayo haijaendelezwa akaiendeleze, ameshindwa UN habitat sasa huku anataka kuja kutulezea kitu gani? Alishindwa chiligati akaondoka na yeye mueleze kuwa nae ataondoka , HAPATAJENGEKA!
Mwambie sisi wakaazi wa Kigambni tuna Mwenye Ez Mungu, ambae ndio mmiliki wa ardhi na mbingu na vyote vilivomo, kama wanataka kudhulumu basi yeye mwenye Ardhi yake asubiri atawafanya nini, nakuapia utakuja kukumbuka haya maneno yangu, pale PATAJAA MAJI NA HAPATAJENGEKA! kama huamini sibiri na uone!