Goldman
JF-Expert Member
- Dec 10, 2010
- 1,930
- 2,397
mkwere anafanya vitu kama mbuni kukitokea tatizo anakimbia au anaficha kichwa ardhini! Hapa nilipo kila siku kuna mgao wa umeme kuanzia juzi wameuongeza tena yaani nina hasira kwa nini cdm au vyama vingine tusiandamane kupinga kutokupatikana kwa umeme? Hakuna umeme, maji ya bomba tushasahau yanavyotoka, bidhaa zote bei juu, elimu inazidi kuporomoka, wazee wa east africa hawalipwi wakati dowans wanataka kulipwa faster, mishahara haiongezwi etc matatizo yako mengi sana nchi hii, kuna watu wanatoa solution kama jinsi ya kupunguza foleni za magari kwa ku built fly over eneo za trafick light na njia za chini lakini hakuna viongozi anaye react. Mpaka watu wagome ndo watawa please hao, then wakitokea wengine wanagoma wakiwa wachache hawasikilizwi. Hivi mkwere & your co mnatutakia nini? Kama hela mnazo maisha ya anasa mnaishi lakini hata kutupa solution za matatizo yetu huwezi? Hivi ukienda ukakopa 2 billion US $ ukaja nazo ukatutengenezea steigler project inayoweza kuzalisha mw 2000 ili tupate umeme wa uhakika, itakuathiri nini ktk anasa zako? Hivi ukimwita Slaa na Mbowe na vichwa vingine mkaunda "think tank" jinsi ya kututoa hapa tulipo ili tusonge mbele itakufanya upungukiwe na nini? Kweli unasema unaanzisha miji ya viwanda wakati umeme hakuna? Watu wa migodi wanatumia ma generator yao wakati tuna eneo lina mw 2000? Hata kama litachukua ten years kuwa ready we will know you have solved the problem. Tuna madini mengi sana ushaenda Zambia ukauliza walifanyaje wakavunja mikataba yenye kodi ya kuwapendelea wawekezaji badala ya wananchi, nenda Botswana kaangalie walivyofanikiwa ktk kuinua pato la nchi kwa kutegemea madini. Kama unawaogopa isije ikawa mambo ya icc kwa nini Zambia waweze sisi tushindwe? Uliunda tume ikakupa majibu lakini wananchi hatuoni kitu. mkwere uwezo wa kututoa hapa tulipo kutupeleka mbele upo na bado ukaendelea na anasa zako, kama huwezi mpe Magufuli awe waziri mkuu kuliko huyo pinda ambaye ni "yes boss" unajua nikitafakari nashangaa ilikuwaje ccm wakakupa u president? Inakuwaje unajibu "hujui kwa nini watanzania ni maskini" hujui! Mi nakushauri weka urafiki pembeni linapokuja swala la taifa, unda "think tank" vikiwemo vichwa vyote Slaa, Mbowe, Magufuli, cuf etc, lets build our tz together.