Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Nakubaliana na wewe, wanasiasa
wooote waliofanya mkutano kwa nguvu wapelekwe mahakamani, na hapa
naamanisha wote including Dr Bilali aliyefanya mkutano mkubwa wa CCM
huko Bububu jana 2nd Sept 2012.

sawa,na wa fiesta nao tuwaweke kundi gani???
 
hawajaita hata wataalam wa milipuko kuja kuchunguza eneo latukio kabla hawajahamisha ushahidi hivyo tegemea ziro ripoti
 
Kifo cha mwandishi Daudi kilipangwa mimi nilikuwepo kwenye eneo la tukio, hakuna aliyesababisha vurugu isipokuwa Polisi
Chadema walipofika waliruhusiwa kufanya mkutano wa ndani wakati wakijiandaa kusaini kitabu cha wageni na wanachama wengine wakiwa nje amri ikatolewa na viongozi wa chadema kuwa wasio wanachama waondoke kwani hakuna mkutano. sekunde chache Kamuhanda akatoa amri ya watu wote kutawnyika. Wakati wote huo Mwangosi alikuwa akichukua matukio ya pande zote zaidi sana alikuwa jirani na polisi pasipo wasiwasi wowote.....

Asante mkuu. Nimependa sana
 
Kuuwa muuewe nyie na kujichunguza mjichunguze nyie. Kweli hawa polisi wanatufanya hatunazo
 
Mwaka jana Mwenyekiti wa CCM Rungwe aliuwawa na "mahasimu " wake wa kisiasa.
Baadaye kidogo Prof Mwandosya akaugua.
Hatukukaa sawa Dr Mwakyembe akaugua lwa sumu isiyoeleweka.
Sakata la Dr Ulimboka bado hatujalisahsu.

Sasa Mwanfishi wa habari CH 10 Ndg Mwangosi ameuwawa.

Wandugu pamoja na UCCM wangu sasa nakosa amani


Pole mdogo wangu masopakyindi ila uliyoyataja wazungu huyaita "just the tip of an iceberg". Nitakachokuomba ni kitu kimoja tu, zidi kufunguka macho uweze kuyaona yale ambayo wengine tunayaona na kuyashuhudia kila siku na kila saa...yanasikitisha, yanaudhi na yanakasirisha. Maswali utakayoamua kujiuliza hivi sasa kama tu ungethubutu kujiuliza awali hapo nyuma, labda mchango wako katika kurekebisha hali kama hiyo ingeweza kuleta tofauti. Kama ilivyokuwa kwa Farao wa Misri, ilibidi ampoteze mtoto wake mpendwa ndipo fahamu za kujiuliza maswali magumu zilipomjia. Ni kweli finally alisalimu amri but at what cost!

Sina hakika una umri gani lakini Marehemu Daud Mwangosi angeweza kuwa mwanao au mdogo wako...sasa shuhudia wauaji wake wanavyoendelea kutamba. Kwa nini wanatamba? Kwa sababu wengine tulipopaza sauti zetu, ndugu zetu mliziba masikio, tulipolalamika hamkutuunga mkono, tulipotoa tahadhari mlitucheka...Kiburi cha Kikwete, kiburi cha CCM, kiburi cha Said Mwema na kiburi cha Kamuhanda kinatokana na waliokaa kimya kama wewe. Kwa mauaji yaliyofanyika hadi leo na kwa shida na taabu zinazotukabili, wewe masopakyindi ni mshiriki na huwezi kukwepa lawama.

Haya matukio lazima yapate maelezo ya kisiasa ili wananchi tupate kuelewa.
Maelezo rahisi rahisi kidogo yanaanza kukosa mantiki, ukifikiria kwa kina kuna pattern inaanza kujitokeza.
 

1346667662.jpg
Daud Mwangosi

1346667711.jpg
Paul Chagonja
Francis Dande, HabariMseto blog -- JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjauchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.

Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

966099517.JPG


Source: Jeshi la Polisi launda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi - wavuti

Hivi hawaoni aibu huu upuuzi wa maigizo wanayotufanyia???? TUME JUU YA TUME...Hivi wingi wake zinakuwa NYUME??? Huu ni ulaji wa wajumbe wa TUME na hamna jipya lolote litatoana na TUME HII!!!!
 
Hivi Nchimbi, Mwema ni watu wenye akili timamu au ni mataahira/zuzu wasiojijua.

Tume ni ya nini kwenye hili? Ni wazi wameshindwa kazi ndiyo maana wanaunda tume iwasaidie na kama tume inaundwa basi Nchimbi na Mwema wajiuzulu tume ifanye kazi.

Mimi ndiyo nauwa halafu najiundia tume najichunguza kama niliuwa kweli, Mwema huna akili sawasawa na nunda mwenzako Nchimbi
 
Hivi Nchimbi, Mwema ni watu wenye akili timamu au ni mataahira/zuzu wasiojijua.

Tume ni ya nini kwenye hili? Ni wazi wameshindwa kazi ndiyo maana wanaunda tume iwasaidie na kama tume inaundwa basi Nchimbi na Mwema wajiuzulu tume ifanye kazi.

Mimi ndiyo nauwa halafu najiundia tume najichunguza kama niliuwa kweli, Mwema huna akili sawasawa na nunda mwenzako Nchimbi
 
Mimi nina wazo binafsi NAOMBA ASKARI POLISI WOTE TANZANIA WAFANYIWE KIPIMO CHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.nasema hivyo kwa sababu ukiangalia picha ya mauaji polisi walikuwa wamaishamdhibiti yule mwandishi kitendo ambacho hakukuwepo sababu ya kutumia nguvu tena.Alafu kwa maelezo ya yule shuhuda aliyepiga picha anasema huyo plisi aliyenyosha fimbo juu alikuwa akiwakataza wenzie wasiendelee kumpiga mwangosi na huyo polisi alikuwa na nyota tatu.Kwa maadili ya polisi na jeshi afande mwenye cheo cha juu ndo msemaji /anayeamulisha matukio.Je kama siyo bangi kitu gani kiliwafanya hawa polisi kapuku kukaidi amri ya kiongozi wao? naamini madawa ya kulevya hasa bangi inayokamatwa na polisi hawaiteketezi yote wanabakiza inayaitwa vitendea kazi .KAMA NAONGOPA BASI WAPIMWE KAMA WANAVYOPIMWA WANAMICHEZO.
 
IGP si shemeji sasa nikimtimua sister atalalamika watoto watakufa njaa"....
 
Polisi wote jamani wapimwe kamahawatuii bangi vinginevyo watatumaliza!!!!!!!!!!!!!
 
Kwanza watuletee majibu ya tume ya Ulimboka. Huu sasa ni upumbavu. Hili jeshi limejaa madikteta, makatili, vilaza, wapuuzi ambao wanafikiria kuua tu na si kulinda raia. Wanatumia nguvu always hata pale panapohitajika akili. Nimependa kauli ya Jenerali Ulimwengu "uongozi dhaifu huwa brutal". Nasema "polisi ni adui wa wananchi, sio walinzi".
 
Hongereni Jeshi laporis kwakuendelea kufanya mauaji kwawatu wasiokua nahatia nchini, lakini ukweliwamambo utabaki palepale kua hamtoweza wabadilisha wanchi kwamawazoyao saizi, lakini yawapasa kukumbuka kua atendaye mabaya sikuzote hukumuyake pia hautokua nzuri mbinguni. Tanzania amani imepotea saiz tumekua kama nchi nyingine mauaji kila kukicha. Hiyotume haina umhimu kwasabab picha yenyewe inaonyesha kila kitu, huo niubadhilifu wafedha zawananchi. Tunauwawa halafu badomwatuundia tume. Mi nadhani undeni tume yakujichunguzeni nyie kua kwanini munaunda TUME.napia jichunguzeni kua mbona saizi munawaua sana WATANZANIA hapo nadhani hiyotume ikifanya hayomambo mtaweza fanikiwa. HOLEWAKO WEWE UTOAYE UHAI WAMTU KWAAJILI YAKUHAIDIWA ANASA YAPESA HUKUMUYAKO NIMBAYASANA MBINGUNI, YAKUPASA KUJITAKASA.:flypig:Wanchi wasasa wanabadilika kila kukicha wakombioni kutafuta maisha namaendeleo na sio kusinzia sinzia. Mtanzania mwenyeakili haweziona nchiyake inaenda hovyo akaKaa kimyi kamwe, ukiona hivyo huyo simzarendo nachiyake.
 
Wapendwa watanzania wenzangu, huku tunakokwenda ni kubaya sana. Kinachotusikitisha ni kwamba askali waliapa kutulinda sisi watanzania pamoja na mali zetu ndiyo wanaotuua. Ebu nioorodhesha kidogo matukio kadhaa. Kumbuka Arusha, Morogoro na hili la Iringa. Hivi hatujui thamani ya uhai wa binadamu???? Ata kama kuna chuki yoyote inayoletwa na sababu zozote ata kama za kisiasa basi tukumbuke sisi tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Unavyomuua mtu hujue umeua ata familia yake na wajuani wake wote. Wazazi wa mwanahabri marehemu huyu pamoja na watoto na mke wake fikirieni jinsi atakavyolichukia jeshi la polisi pamoja na serikali yake. Hivi atat kwa akili ya ngedere kwanini unaunda kamati ya kuchunguza mauuaji uliyofanya mwenyewe???? Huo ni utoto na kutumia vibaya madaraka na mali ya wananchi. Imefikia muda sasa watanzania tuamke na tuingie kwenye mapambano dhidi ya shetani aliyeizunguka nchik yetu. Inawezekanaje askali atumie silaha kubwa namna hiyo kutoa matumbo ya rahia mzalendo??? Binafsi imenisikitisha sana na kilio changu nampelekea Mungu ili ahukumu watu wakiwa hapahapa duniani. Kama Mungu atanisikia naamini atatenda kile kinachositahili kuwahukumu watu walitenda unyama huu. Nashauri serikali yangu isimamie haki ili wanyonge tutendewe haki yetu. Haya mambo ya siasa tunayatumia vibaya. Hivi kama chama hakina jambo zuri kwa watanzania ni kwanini unaendelea kulazimisha wakuamini???? Napenda kutoa wito kwa watanzania wenzangu tufunge katika sala na tumuondoe shetani mkubwa wa hatari anayeua wananchi wasio na hatia. Muheshimiwa Raisi ona busara katika jambo hili na utoa tamko juu ya mauaji yanayoendelea kwa wananchi uliopa kwa ajili yao kuwalinda. Nawachukia sana wote wanofurahia mahuaji haya.
966099517.JPG

Hii picha ina majibu mengi sana;
Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja katika mtutu ulioelekezwa kwake, moshi huo bilashaka ni matokeo ya bomu lililopigwa na huyo askari wa kushoto kabisa aliyeelekeza mtutu wake kwa marehemu.[/QUOTE]
 
CCM haiwezi kuachia madaraka kwa njia ya amani ingawa inatambua kuwa imechokwa na watu wameisusa na wanaitazama kama mbwa anavyotazama shillingi. Hata mkiua ni lazima tuwasukumie gizani hamuwezi kukwepa upepo huu wa mabadiliko. Lazima mtaondoka tuu...! Undeni tume ili mle pesa na kujifurahisha tu.Hakuna mtu mwenye akili timamu mwenye imani na usahihi wa kile kitakacholetwa mezani na hiyo tume.
 
Tume inayoundwa na jeshi la Polisi na JWTZ haiwezi kusema ukweli hata kidogo. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Polisi hawajawahi kusema kweli hata mara moja hasa kwa matukio ambayo wanahusika. Aidha haingii akilini Jeshi hili kuongoza tume au hata kushiriki kuchunguza kifo ambacho wao ni watuhumiwa nambari moja.
Tangu tukio la kuuawa Daudi litokee Polisi wamekuwa na kauli zinazojikanganya. Watanzania tukumbuke siku ya kwanza RPC Kamhanda asikika katika vyombo vya habari akisema Mwangosi aliuawa na kitu kilichorushwa toka kwa wananchi. Muda mfupi kupita Waziri Emanuel Nchimbi akanukuliwa akisema kuwa kilichomuua Daudi inasemekana ni bomu lililoripuliwa bila utalaamu na Polisi.
Jana kupitia BBC Kamhanda amesikika akisema "Marehemu alimkumbatia OCS wakati huo nilikuwa pembeni nikitazama, ghafla kukasikika mlipuko na kumwua kumjeruhi OCS". Kwa yeyote mwenye akili timamu akitazama picha zilizochukuliwa na waandishi wa habari katika tukio na kurushwa siku hiyo hiyo (angalia blog ya Francis Godwin) atajua kabisa Kamhanda anaongopa. Aidha kilichomfanya abadili kauli ni picha hasa iliyotolewa na gazeti la Mwananchi jana tarehe 3/9/2012 ikionesha Mwangosi akipigwa amezingirwa na Polisi wenye silaha na gari ya RPC ikiwa pembeni. Kamhanda anajua kilichotokea na walichopanga tangu awali. Walijiandaa kuua na hata kama asingekuwa Mwangosi lazima angekufa mtanzania mwingine yeyote yule. (Angalia picha ya Polisi wakishuka wakiwa na bunduki).

Kwa nini ninapinga Jeshi la Polisi kuunda tume? Chagonja ndiye aliyetumwa kuchunguza mauaji yaliyofanywa na Jeshi hili hili la Polisi huko Songea chini ya Kamanda huyu huyu Kamhanda; akiwa njiani kuelekea Songea Chagonja akihojiwa na radio moja alisema "hao walikuwa ni wahuni waliotaka kwenda kuleta vurugu ktk ofisi ya mkuu wa mkoa na kuteka kituo cha Polisi, sasa jeshi la Polisi likichukua hatua watu wanalalamika...." Je, ikiwa kabla hajafika Songea Chagonja alijua ni wahuni walioandamana na hatimaye wanne kati yao kuuawa alikuwa anakwenda Songea kufanya nini? Alitumwa kuchunguza au kwenda kujastify "perdierm" na kuweka mikakati ya kuua zaidi????
Chagonja alikwenda Tandahimba wakati wa kulipotokea kinachoitwa vurugu wakati wakulima wa korosho wakidai malipo yao; Chagonja aliahidi kushughulikia suala hili na kuwajibisha askari wote waliochoma vibanda vya biashara za wananchi, kupiga raia na kuwapora simu na bidhaa nyingine. Iko wapi taarifa ya uchunguzi huo au hata askari waliowajibishwa?

Nimgeukie Kamhanda; huyu ndiye alikuwa RPC mkoa wa Ruvuma; wananchi wakawa wakiuawa kila uchwao na kukatwa viungo akadai "sababu ya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi". Wananchi walipoandamana kudai haki yao ya kulindwa alituma Polisi wakawauwe zaidi! Huyu ndiye Kamhanda, kamanda wa mauaji! Atachunguza nini? Atatenda haki gani katika hili?
Kabla ya kuja Kamhanda Iringa tulikuwa na Kamanda Mangalla, CHADEMA na vyama vingine vya siasa walifanya mikutano kadhaa wa kadhaa lakini hatukuwahi kushuhudia vikosi vya FFU wakipita mitaani wamevaa mavazi ya kutisha na na silaha wakiongozwa na Kamhanda. Wakazi wa Iringa ni mashahidi siku alioingia mjini Iringa Dr Slaa (tarehe 28/8/2012 jioni). CHADEMA amefanya mikutano mingi, tena inafanyika Kihesa sokoni eneo liko pembeni ya barabara ya Iringa-Dodoma lakini hata barabara hazifungwi Polisi na vijana wa CHADEMA husimamia na kuona mkutano unafanyika na kumalizika kwa amani. CCM walimtuma Nape akafanya mkutano nje ya soko kuu (mahali penye watu wengi na ilikuwa week end) lakini hakukuwa na Polisi hawa tuliowashuhudia wiki iliyopita.
Kwanini Kamhanda anataka kujenga hofu kwa wana Iringa? Kwa nini amefika yeye ndiyo FFU wajue kuvalia mavazi yao ya chuma na ngao na kutembea na bunduki? Mkoa wa Iringa una uhaba wa askari kwa nini kama Kamhanda ameona FFU hawana kazi nyingi asiwapeleke Pawaga kulinda wananchi (wakulima na wafanya biashara wa mpunga) wanaouwa na majambazi??)

Sina imani na tume za jeshi la Polisi kutokana na kumbukumbu ya matukio ya nyuma:
1. Iko wapi taarifa juu ya maujia ya vijana wawili walipigwa risasi na kuuawa na Polisi katika kituo cha mafuta huko Arusha?
2. Iko wapi taarifa ya mauaji ya raia kule Nyamongo?
3. Iko wapi taarifa ya mauaji ya raia wanne wakati wa maandamano ya CHADEMA kule Arusha?
4.Iko wapi taarifa ya mauaji ya watu wanne kule Songea?
5. Iko wapi taarifa ya uchunguzi wa waliomteka Dr Ulimboka?

Haya ni matukio machache kati ya mengi ya mauaji yalifanyika mikononi mwa jeshi hili linaloongozwa na Said Mwema.
Itoshe tu kusema kuwa; Said Mwema na anaowaongoza wanapanda MBEGU MBAYA MIOYONI MWETU, KILA UCHWAO WATU WANARIPITIWA KUFIA MIKONONI MWA POLISI NA WENGINE KTK VITUO VYA POLISI. WaTz tunasikia na tunaona. Wanaokufa ni kaka/ dada/mama/ baba/ shangazi/ wajomba/ watoto na rafiki zetu. Iko siku watanzania tutasema BASIIIII! Je, Kamanda Mwema na Jeshi lako MNAZO RISASI NA MABOMU YA KUTUSHA KUTUMALIZA SOTEEEE!!!!


EJL
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom