Polisi waua tena mtuhumiwa mara

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Jeshi la polisi limedaiwa kufanya tena mauaji,mugumu mkoani mara ambapo safari hii,askari wa kituo cha mugumu wilayani serengeti wamedaiwa kumuua Nyitamboka Mwita(28)kwa kumpiga risasi akiwa nyumbani kwake kwa madai yakuwa ni jambazi.
 
Source please?
Tusifikie conclusion za kulaumu jeshi la polisi,hebu wadau tufanye uchunguzi.
 
Polisi wote inabidi wastaafishwe kwa manufaa ya umma: wanasababisha tatizo la Yatima nchini kuongezeka kwani wanaowaua wanaacha watoto wao bila wazazi.
 
Hakuna tatizo polisi kumua jambazi maana sikuhizi nasikia polisi ndiyo mahakimu hivyo lazima walifata kifungu furani ambacho mimi sikijui cha kuharalisha polisi kuuwa bila kumfikisha mtuhumiwa mahakama samahani siyo mtuhumiwa ni jambazi....
 
Nimeisikia habari hii kwenye uchambuzi wa magazeti leo asubuhi nimesikitika sana inaonekana kweli inchi haitawaliki
 
Kama Serikali yenu siku hizi haifati RULES OF LAW bali sheria mkononi.

Vipi na wananchi wakiamua kufata sheria mkononi vipi kutatawalika huko?
 
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa mara robert boaz alipoulizwa alisema marehemu alitoka na panga na kumshambulia PC sixbert kwa kukamata magazine na kumuangusha chini.Alisema PC rajabu alimpiga risasi mkononi,lakini marehemu aliendelea kutaka kumshambulia na kwamba ndipo PC huyo akampiga risasi ya mgongoni iliyo tokea kifuani na kumuua.
 
Hivi mnaonaje Wananchi kuuwa Mafisadi sorry majambazi yanayotumaliza utajiri wetu.... "Akuanzae......!!!:laser::laser:"
 
Jeshi la Polisi maana yake USALAMA WA RAIA, lakini sijui hili la kwetu
kama kweli ni usalama wa raia au UHASAMA WA RAIA.
 
Kama kawaida ya jeshi la polisi na ukandamizaji wa haki za binaadamu.Hata Kama mtu ni jambazi sheria hairuhusu kumuua.Alibishana na polisi kwa kuwarushia risasi?jibu ni hakuna sasa kwa nini wamemuua!!?Halafu IGP Saidi Mwema analitetea jeshi la polisi kutumia nguvu kali.Ipo siku Wasomali watatuletea silaha na kitu tutafanya watafurahi
 
Kama kuna taasisi itakayo suffer magamba wakitupwa nje 2015 ni hawa police. Nadhani jeshi hili litaundwa upya kabisa , sidhani kama kutakuwa na wachache watakao baki.
 
Jeshi la polisi limedaiwa kufanya tena mauaji,mugumu mkoani mara ambapo safari hii,askari wa kituo cha mugumu wilayani serengeti wamedaiwa kumuua Nyitamboka Mwita(28)kwa kumpiga risasi akiwa nyumbani kwake kwa madai yakuwa ni jambazi.

Japo Majambazi wanaudhi, lakini si kazi ya Polisi kuua mtu kwa tuhuma tu za Ujambazi. Na hawa polisi wamethibitishaje kwamba hilo ni jambazi! Na hata kama ni Jambazi si linatakiwa Polisi walikamate na kulipeleka mahakamani ndipo watakapo-declare kwamba ni jambazi na kisha hukumu ya haki itolewe, ambayo kwa kwetu nachojua si adhabu ya kifo bali ni kifungo? Au hawa Polisi sasa wameamua kufanya lolote walitakalo bila kuhojiwa? Au wamejivika cheo cha Ziraili!

Kama Wao ndio wameshajiona ni Mahakama na Watekeleza hukumu, kwanini wasiende kumkamata Mwizi Chenge ambae ushahidi wa Wizi na Usaliti wake kwa nchi hii upo wazi!

All in all Time will tell.
 
Jeshi la polisi limedaiwa kufanya tena mauaji,mugumu mkoani mara ambapo safari hii,askari wa kituo cha mugumu wilayani serengeti wamedaiwa kumuua Nyitamboka Mwita(28)kwa kumpiga risasi akiwa nyumbani kwake kwa madai yakuwa ni jambazi.

Police akiua jambazi shujaa! Wanachi wakiua oh' wamejichukulia sheria mikononi! Jaman tusipokuwa makin polisi watatumaliza.HATA HIVYO POLISI WAMEISHIWA MBINU ZA KUKAMATA NDO MAANA WANAWAUA WATUHUMIWA! Kuna mtu inabidi aachie ngazi hapa.
 
Sasa hivi wenyewe wanauwa tu alafu kisingizio majambazi na akili zao mbovu,wasubiri tu muda wao uishe jeshi lote litapanguliwa na kupangwa upya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom