Polisi waua mmoja kwa risasi Mbeya

Ni kweli polisi wameua watu watatu kwenye ghasia huko Ubaruku lakini chanzo cha ugomvi si mpaka wa shamba bali kuzuiwa kwa malori ya zaidi ya tani 8 kupita kwenye barabara hiyo kwenda kuchukua mpunga wa wakulima (hivyo wananchi wameshindwa kuuza mpunga wao) wakati mfanyabiashara wa mafuta ameruhusiwa kupitisha la lori lenye uzito zaidi ya huo kupeleka mafuta (kama kawaida wawekezaji kwanza wananchi baadae - inauma) huko Rujewa.

Wananchi waliamua kulizuia lori hilo ndipo polisi wakaja na kuanza kuwatawanya wananchi kwa kutumia mabomu ya machozi na kama kawaida yao wakawapiga risasi za moto na kuua watatu kwa uchache. Wananchi wakaamua kuchoma lori moto na kuunguza kituo cha mafuta pia.Nasikia vurugu zinaendelea na polisi wameomba msaada kutoka Mbeya baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi.

Tangu hotuba ya kikwete ya kuuaga mwaka na kuonya juu ya vurugu, askari polisi wamekuwa hawasiti kuwasha risasi za moto kwa wananchi, jamaa ameamua kutoa kafara wananchi wake ( kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia)

Hivi kweli JK, Nahodha na Mwema bado wanaona wanastahili kuendelea na nyazifa zao?
 
Wakubwa hakuna Polisi nchi hii!! Tuna killing squad kwa ajili ya kulinda maslahi ya wezi wachache!!!!
 
Taarifa za kiitelejinsia, zimesababisha balaa jingine, Haya sasa JK, na hapo UBARUKU chadema wanahusika?
 
Pole sana ndugu zangu waliofiwa wa Ubaruku,na adha ya mabomu pia.Yani sasa kuna double standards hata kwenye miundombinu kama barabara???? kweli watu alama za nyakati hawazisomi,watu wanajua haki zao!najua hayo magari makubwa yanaharibu barabara in the lobg run,sasa kuna barabara mbadala,na kwanini waruhusu gari la mafuta lenye tani hizo wanyime la kubeba mpunga????
 
Tanzania hakuwahi kuwa kisiwa cha amani hata siku moja bali watanzania walikua waoga na watu wa kusema yes yes na hawakua makini katika kudai hazi zao. Sasa hivi watanzania wamezinduka wameamua kupigania haki zao, polisi nao wanatakiwa kubadili mbinu za kukabiliana na raia. Kizazi cha mwalimu nyerere kinaanza kupotea na tunu ya amani ya mwalimu imetoweka. Polisi wanapaswa kua wavumilivu wasikimbilie kutumia risasi za moto. kama mabomu ya machozi yameshindwa kufanya kazi wabuni teknolojia mpya ambayo haina madhara kwa binadamu vinginevyo kila siku watakua wanaua watu.
 
Hawa wadudu wameshaonja damu ya watu sasa hawatak kuacha,ila mbona na wao (maaskar) ni sehem ya watanzania wanaoteseka na kupata shda? Kwa nin wanakubal kutumiwa without thinking twice? Hawa watakiwa walnz na marafk wa wananch na si maadui,let them watch their backs.
 
Hawa polisi ni bogus wandugu. Hawajui kwamba raia wanaweza pia kumiliki silaha na ku retaliate. Utafikiri hawana vichwa.
 
Fangfangjt tupe habari zaidi sababu ya wananchi kuchoma moto lori na kituo cha mafuta. Na kwanini polisi waue raia? Ni Mbarali sehemu gani ?Rujewa, Igawa, Chimala, Igurusi au wapi? More information is needed







Na Fredy Bakalemwa, Mbeya
Mtu mmoja amekufa na mwingine amejeruhiwa vibaya katika mapigano baina ya polisi na wananchi wilayani Mbarali kutokana na mzozo ulioibuka tangu mwezi uliopita baada ya serikali kuzuia magari yenye uzito zaidi ya tani 8 yasipite katika barabara ya Igawa hadi Ubaruku.
Kwa mujibu wa taarifa ya diwani wa kata hiyo Bw. George Mbila ambaye amezungumza na kituo hiki majira ya saa 10 :30 akiwa eneo la tukio kwa njia ya simu amesema tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa 8 mchana.
Bw. Mbila ameeleza kuwa wananchi walizuia gari lililobeba mafuta mara lililofika katika kituo cha mafuta kilichopo njini Rujewa ambacho ni mali ya mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Munifu.
Imeelezwa kuwa wananchi hao wakulima na wafanyabiashara za mpunga wanapinga kuruhusiwa gari hilo kupita katika barabara hiyo huku serikali ikiwa imezuia magari yote zaidi ya tani 8 yasipite hatua ambayo wakulima wanadai serikali haitendi haki kwao.
Diwani huyo ametaja jina la mtu aliyeuawa aliyetambuliwa kwa jina moja la Justine mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 na kwamba majeruhi hakutambiliwa jina lake lakini hali alikuwa mahututi yake baada ya kupigwa risasi.
Aidha Bw. Mbila amesema hadi majira ya saa 11 ruvugu zilikuwa bado zinaendelea na kwamba gari la mafuta limechomwa moto pamoja na kituo cha mafuta mali ya mfanyabiashara huyo Bw. Munifu mkazi wa Rujewa.
Kamanda wa polisi mkoani humo Bw. Advocate Nyombi majira ya saa 11 kwa njia ya siku amesema kuwa alikuwa bado anafutalia taarifa za tukio hilo na kuahidi kuzitoa pindi atakapokuwa anekamilisha mchakato wa taarifa juu ya tukio hilo.
Mwisho.
VN:F [1.9.7_1111]

source:
 
Sasa naona uchumi wa nchi kuzikwa kabisa.

Kama wakenya kuzuia mali kupita kwenye barabara zao na mireli kwenda nchi jirani hata njia ya Dar es Salaam kwenda Malawi, Zambia, sijui na wapi huko naona hivi karibuni wananchi watalazimika kuvizuia na mali ya shamba kutokuletwa mijini kama kweli polisi sasa wameingia mikoani na vijijini kuwaua wakulima namna hii.

Moto mkubwa sana uko njiani wananchi kulipa kisasi na huenda Kikwete akajuta zaidi.
 
Ndg zangu wana JF,
.............. Polisi wameingilia kati na mpaka sasa wananchi 3 tayari wamepoteza maisha. Muda si mrefu DEFENDER 12 zikiwa na askali polisi kutoka Jijini Mbeya zimewasili Ubaruku tayari kukabiliana na wananchi wenye hasira kali...................

JK, IGP anabehave hivyo na sasa polisi wadogo nao wanaiga MISIMAMO YA WAKUU ZAO; PIGA UA. Utakuta mwenye mafuta ana connection na mafisadi wa nchii hii basi anapiga simu polisi mbio wanakuja wakati wakiambiwa kuna majambazi wanakuwa kimya au usikute ni wenzao tu. Hivi hamjui kuwa watu watapandishwa vyeo kwa kuua raia huko Arusha na Ubaruku? Kweli siku za serikali ya JK zinahesabika. Poleni sana wafiwa Mungu awape moyo wa subira.
 
Unajua wakati wadau wanapiga kelele kuhusu nchi kuuzwa tulibaki tukishangilia na kushadadia kampeni za vyama ambavyo tangia uhuru tumeshindwa kumaliza tatizo la umeme lakini tunampango wa kujenga Flying overs kule dar,leo tunalia kuuawa?lazima tufe kwani tuliowachagua kwa kupewa tshirt,kanga na kofia ndio wakati mwafaka wa kulipa kwa damu na Dowans.Nakumbuka jana nilikuwa mahali naomboleza wale raia wema waliopotezewa maisha na serikali kule kwetu arusha akaja rafiki yangu wa karibu sana akanikumbusha jambo ambalo nilimwambia wiki mbili zilizopita kuwa "Wakati wazungu wanakuja hapa Afrika,sisi tulikuwa na ardhi,wakaja kutufundisha kwa kusema tusali huku tumefunga macho,tukafunga huku wameshika Biblia mkononi.Tulivyomaliza kusali wakasema tufungue macho tukajikuta tuna Biblia wao wana ardhi."Nielewe kwamba mimi ni Mkristu na sina maana ya kupotosha kuhusu Biblia ila nia yangu ni kujaribu kuonyesha namna wazungu wanavyorudi na kutufanya tuishi ugenini huku nchi ni yetu,kule mara wananchi walinyweshwa sumu serikali yetu wakakataa lakini baadaye wakaomba radhi,Loliondo kila mmoja anajua,kule arusha kwenye mashamba ya mzungu kila mwenye macho haambiwi tazama,hata hili la wenzetu wa Mbeya sishangai kusikia kesho Kamanda wa Polisi akisema Wananchi hao walikuwa wanaleta fujo kwenye ardhi ya mzungu kama walivyokejeli mauaji ya arusha,Kila mwenye akili na afikiri namna walivyowalazimisha wafanyabiashara na wawekezaji kuwachangia ili wafanikishe azma yao ya kupora.Hatushangai Ngeleja kukazana kuwalipa Dowans kwani ni kurudisha fadhila,Kuambiwa noti mpya zimeibwa pale Airport dar billioni 10 kisanii tumezoea,Fedha zilizochotwa BOT kwa ajili ya kampeni ya mwaka 2010 zaidi ya bil.2,nazo zimeibwa?Mauaji ya Arusha badala ya Kikwete kuongea na kuwaomba radhi wananchi aliwaita mabalozi wa LONDON na NEW YORK na kuwaambia hayatatokea tena. Ndugu wana Jf,nimeenda mbali sana kujaribu angalau kwa ufupi kuonyesha mtiririko wa hila na namna mtanzania anavyotendewa kinyume lakini kipindi cha uchaguzi anasahau kwa kuhongwa vitu vidogo.
 
'Polisi Jamii' imekuwa 'trigger-happy police'! Kikwete alidai yaliyotokea Arusha hayatatokea tena! Hata mmwangi wa sauti yake haujaisha Polisi washaua tena!
 
Poleni watu wa Ubaruku lakini pia nawashukuru watu wa Mwanza pale walipowaambia polisi " tuuweni na sisi watoto na wake/waume zenu tunaoishi nao uraiani halali yetu". Nchi nzima ikiwakumbusha polisi kuwa hawaishi kambini, hakuna risasi itakayofyatuliwa!!!
 
WATU wawili wamekufa na wengine kujeruhiwa wakati wa mapambano baina ya polisi na wananchi wilayani Mbarali. Pamoja na mauaji hayo, mamia ya wananchi wenye jazba walichoma na kuliteketeza kabisa lori la mafuta, lililodaiwa kupita katika barabara ya Igawa –Ubaruku, wilayani humo. Hatua hiyo imekuja kufuatia lori hilo lenye namba za usajili T 994 ASS, kupita katika barabara hiyo, ambayo serikali imepiga marufuku magari makubwa kupita.
Habari zinasema kuwa kupita kwa lori hilo kuliamsha hasira za wananchi, waliodai kuwa magari ya wafanyabiashara wa mchele yamekuwa yakizuiwa. Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu jana, Diwani wa Kata ya Ubaruku, George Mbila, alisema mamia ya wananchi walipandwa na jazba na hivyo kulizingira lori kabla ya kulichoma moto. Hata hivyo, wakati moto ukiendelea kuliteketeza lori hilo, polisi waliingilia kati ili kudhibiti wananchi hao, ambapo mapambano makali baina ya pande hizo yalianza. Alisema kwa muda mrefu wananchi wametii sheria ya kutopitisha magari mazito katika barabara hiyo, lakini baadhi ya wafanyabiashara wa Kiasia wamekuwa wakipitisha bila sheria kuchukua mkondo wake. Mbila alisema vurugu hizo zilikuwa kubwa kutokana na wananchi kukusanyika kwa wingi kukabiliana na polisi, ambao walilazimika kupambana ili kulinda usalama wa raia wengine. Aliongeza kuwa wananchi pia walichoma kituo cha mafuta. Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali mstaafu Cosmas Kayombo, alikiri kutokea kwa vurugu hizo, licha ya kwamba alikuwa nje ya eneo la tukio kufuatilia masuala ya mbolea za ruzuku.
Hata hivyo, alisema amewasiliana na mbunge Dickson Kirufi, ili kufuatilia taarifa hizo na kutatua ufumbuzi wa mgogoro huo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alipoulizwa juu ya tukio hilo, alikiri kulisikia na kuahidi kulifuatilia. Awali, Uhuru lililipoti juu ya mzozo huo uliotokana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mbeya, kuzuia magari yenye zaidi ya tani nane kupita katika barabara ya Igawa-Ubaruku.
Hatua hiyo iliyolenga kuiwezesha barabara hiyo kudumu kwa muda mrefu, pia hali iliyoathiri shughuli za kibiashara, hasa za mpunga huku zaidi ya tani 25,000 zikiwa hatarini kuharibika. Hata hivyo, wananchi walitii agizo hilo na baadhi kujitoa kuwa walinzi, lakini kupita kwa lori hilo jana kuliamsha hasira na hatimaye kuchukua uamuzi huo ambao ni kinyume cha sheria.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Uhuru, walisema kuwa gharama za usafirishaji wa mpunga zimeongezeka kutokana na kulazimika kutumia magari madogo hadi eneo la Igawa. Kisauti Mathayo, alisema anashangazwa na hatua ya TANROADS kuzuia malori, huku mengine yakiwemo ya mwekezaji wa shamba la Mbarali, kuachwa yakipita bila kuchukuliwa hatua. "Hakuna usawa katika hili, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wanavunja sheria, lakini wahusika wako kimya. Tumekubali agizo la serikali na tunaingia gharama kusafirisha mazao yetu," alisema.
 
Poleni sana ndugu zangu wa Ubaruku. MUNGU aliye hai ataipiza kwa hizi damu zinazomwagika.

Hivi hakuna njia mbadala zaidi ya kuua? Polisi wa Mbalali mtaishije na wananchi hapo mbalali maana ni kama kijiji! Tuwe makini na matumizi ya bunduki jamani.

POLISI kumbukeni kuwa KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.















life is god gift
 
Back
Top Bottom