Polisi watumia mabomu ya machozi kuokoa maisha ya bibi kizee

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125




JESHI la polisi mkoani hapa limelazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kumuokoa bibi Hadija Kabeya Saloom (70) aliyevamiwa na watu wapatao 50 wakitaka kumuua kwa tuhuma za uchawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa polisi walitumia mabomu ya machozi Julai 11 saa 2.00 asubuhi mwaka huu huko eneo la Shede jijini hapa.

Alisema uamuzi huo ulikuja baada ya watu wapatao 50 kuvamia nyumbani kwa Hadija kwa nia ya kumuua na ndipo polisi walipolazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu katika eneo hilo na kufanikiwa kumuokoa bibi huyo ambaye yupo chini ya uangalizi wa Polisi.

“Polisi tulipopata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa wa Shede kuwa kuna kundi la watu wapatao 50 wanakwenda kumuua bibi kizee Hadija kwa kumtuhumu kuwa ni mchawi na ndipo tulipokimbia hadi nyumbani kwake na kukuta tayari wameishafika nyumbani kwa bibi huyo,’ alisema na kuongeza kuwa

‘Tulitumia mabomu ya machozi na kuwatawanya watu lakini tayari walikwisha bomoa nyumba tatu za bibi huyo na kuiba vitu vyote vya ndani jambo ambalo linasikitisha,” alisema Kamanda.

Akifafanua zaidi juu ya mkasa huo,alisema kuwa kabla ya watu hao kuvamia nyumbani kwa bibi huyo walikwenda kwa mwenyekiti wa mtaa wa Shede kwa nia ya kumshitaki bibi huyo kuwa ni mchawi na kwamba alimchukua msukule mke wa mjukuu wake , Hadija Ramadhan ambaye yu hai .

Alisema watu hao walivumisha kuwa Hadija amechukuliwa msukule na bibi huyo baada ya Hadija kuulizwa na majirani hao kuwa ni kwanini mtoto wake Ramadhan, kakonda na yeye kuwajibu kuwa bibi yake hampi chakula ndipo walipoamua kuvumisha kuwa bibi huyo alikuwa amemchukua mke wa mjukuhu wake msukule na hivyo kupanga kumuua.

“Jamani haya ni mambo ya kushangaza kweli, yaani watu wanaamka tu na kutaka kukatisha maisha ya watu wakiwatuhumu eti ni wachawi hivi kweli hii ni haki,’ alisema Kamanda Sirro.

Alisema kuwa mume wa bibi huyo Hamis Said Malela (76) alishangazwa na kitendo cha kukuta nyumba zake zote zimeharibiwa na watu hao kwani wakati tukio hilo linatokea yeye hakuwepo nyumbani alikuwa kazini katika kampuni ya ulinzi ya Eastern na kwamba aliomba Polisi wampe mkewe amsafirishe na kumpeleka Tabora.

Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa jeshi hilo linawashikiria watu watano wakihusishwa na tukio hilo.

Chanzo Polisi watumia mabomu ya machozi kuokoa maisha ya bibi kizee

Imani za kipumbavu kama hizi zitakwisha lini ? kila anapoonekana kizee hudhaniwa kuwa ni Mchawi? tutandelea kweli Nchini kwetu kwa fikira kama hizi za kipumbavu?
 
Back
Top Bottom