Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,935
- 6,844
Polisi walimzuia Sharpton kwa kuzingatia kuwa kuandamana wakati watu bado wana majonzi ya kifo cha Sean Bell potentially kuna weza kufanya baadhi yao kumalizia hasira zao kwa raia wengine na/au mali zao. Hii inaeleweka na inakubalika. Mimi napinga flimsy excuses zinazotumika kuzuia maandamano hapa kwetu. Excuses kama hii yaati kwa sababu chombo cha wanafunzi kimesajiliwa kama kampuni na si NGO basi maandamano NO! Excuses kama hizi ambazo wengine wanazitoa, ati wangefuata taratibu na kukaa kwanza na uongozi wa Chuo. Uongozi ambao hata kuwatambua hauwatambui! Mimi sijaona ni namna gani raia mwingine au mali zake zinaweza kuwa "harmed" na maandamano ya hawa wanafunzi. Kuwaambia ati watimize sheria kwanza ni kuwaonea maana hamna jinsi wanaweza kutimiza kama Polisi hawataki hayo maandamano. Kuwaambia ati wangoje mpaka bunge wazibadilishe na kwenyewe ni kuwa disingenious. Ikiwa mtu kama Nyalali aliweza kutaja wazi sheria kibao za kigandamizi na serikali ikampuuza itakuwa hawa? Hapana umefika wa kuwaeleza hao polisi kuwa wao ni watumishi wa wananchi na moja ya wajibu wao ni kulinda uhuru wake wa kueleza kutoridhishwa kwake na jambo lolote.
Amandla......
Amandla......