Polisi waonyeshe vitambulisho, namba zao wanapokamata watu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,133
Polisi waonyeshe vitambulisho, namba zao wanapokamata watu
Maulid Ahmed
Daily News; Friday,December 26, 2008 @00:01


Katika harakati zangu mbalimbali za kila siku katika maisha yangu, nimekutana na polisi wengi wanaotumia sare zao za polisi kugeuza mradi wa kujipatia kipato. Polisi hawa naweza kuwaweka katika kundi la watu waliojaaliwa ubunifu na akili nyingi katika kujipatia fedha, lakini wamenyimwa akili na ubunifu katika kupambana na wahalifu.

Nasema hivyo nikiangalia nyanja mbalimbali, polisi wajuzi kuwakaba machinga au wafanyabiashara ndogondogo, waendesha daladala, vibaka na hata waendesha magari ya kawaida tu. Sehemu zote hizo wanahakikisha hawakosi fedha kwa siku na licha ya mishahara yao kuelezwa kuwa ni midogo, lakini kwa polisi anayekwenda mtaani naamini ana kipato kikubwa kwa mwezi kuliko hata bosi wake aliyemwacha ndani akila kiyoyozi.

Sina haja kuelezea maeneo niliyoshuhudia polisi wakichukua rushwa au kwa matukio yaliyowahi kunikuta na kujikuta nikikamuliwa fedha bila kupenda na polisi hawa, lakini lengo langu leo hii ni kuwakumbusha viongozi wa polisi hawa wadogo kuwa sasa waangalie njia nyingine ya kuendelea kuwabana ili wapunguze au kuacha kabisa tabia hii ya kupenda rushwa.

Katika matukio mengi, polisi wanaodai rushwa wanakuwa makini sana kuficha namba zao wanazovaa kifuani huku wengine wakidiriki kuziondoa kabisa na kuzificha wanapokujua wenyewe. Nikizingatia hilo pamoja na tukio lililotokea juzi la kijana aliyekamatwa jijini Dar es Salaam akiwa na sare za polisi inaonyesha wazi jinsi kazi hii ya upolisi ni rahisi kufanywa na kibaka yeyote ili aweze kujipatia fedha.

Katika kipindi hiki cha sikukuu ndicho kizuri kwa polisi hawa ambacho wenyewe wanakiita ni kipindi cha mavuno na utawaona wakiwa wameficha namba zao ama kwa kuweka mkono au wanajidai kushikilia kofia na kuificha na baada ya hapo ndipo wanapolazimisha rushwa tena wasivyo na aibu wanataka fedha nyingi kulingana na eneo walipokukamata wakidai eti maisha magumu wapewe fedha nzuri wakafurahi na familia zao.

Kutokana na matendo ya polisi wetu, nawashauri viongozi wao miongoni mwa njia za kuwadhibiti na kuwafanya wawe na woga ni wao kutoa amri kwao na kuwatangazia wananchi kuwa sasa kila askari anapokukamata, lazima namba yake ionekane kwanza na akupe kitambulisho chake kinachoonyesha kuwa yeye ni askari kweli.

Naamini njia hiyo itasaidia kuwaogopesha wale wanaojifanya polisi ili kutapeli wananchi wasijiingize katika utapeli huo, lakini pia kwa namna moja au nyingine itawasaidia wananchi kuweza kwa haraka kunakili kichwani nambari ya polisi aliyemkamata. Pia itasaidia kupata taarifa nyingine kuhusiana na polisi husika hali itakayomfanya hata yeye awe na woga kwani hajui aliyemkamata ni mtu gani hivyo kwa kuhofia ajira yake anaweza kutoomba rushwa.

Iwapo utaratibu huu utatekelezwa utasaidia kupunguza kama si kuondoa kiburi cha polisi wanaojiona miungu watu na kutumia muda mwingi kukamata vitu vidogovidogo kama magari na kuachana na jukumu kubwa kama kulinda mali na watu ikiwamo kupambana na majambazi au kulinda benki kadhaa.Tumeshashuhudia nchi nyingi zilizoendelea zikitumia utaratibu huu wa kuonyesha kitambulisho hali inayompa amani aliyekamatwa asihofu kama amekamatwa na jambazi na pia polisi mwenyewe kutenda kazi yake kwa uadilifu zaidi.
 
Polisi waonyeshe vitambulisho, namba zao wanapokamata watu
Maulid Ahmed
Daily News; Friday,December 26, 2008 @00:01

Mama mia, some countiries they do have the right to privacy and a police must have a good and probable cause to stop you. Tanzania , hakuna kitu kama hicho. In U.S., they have a miranda rules ....a suspect need to be told of his rights ...Tanzania is the opposite. Jeshi letu laitaji elimu kwanza atawakikuonyesha kitambulisho, haitasaidia.
 
Mama mia, some countiries they do have the right to privacy and a police must have a good and probable cause to stop you. Tanzania , hakuna kitu kama hicho. In U.S., they have a miranda rules ....a suspect need to be told of his rights ...Tanzania is the opposite. Jeshi letu laitaji elimu kwanza atawakikuonyesha kitambulisho, haitasaidia.
Kuna mambo wanaweza wakaogopa mf Kupokea rushwa na wakati unajua kabisa jina lake. Itasaidia. Trust me ukisimamishwa na polisi muulizie kitambulisho utaona ana back-up kidogo.
 
Pamoja na kuonyesha vitambulisho pia wawapeleke watuhumiwa vituoni na si vichocho ili aweze kuomba rushwa.Polisi wawaelimishe raia utaratibu unaotakiwa kufuatwa mtu anapokamatwa kwa tuhuma fulani,matapeli wanatumia mwanya wa kutofahamika taratibu katika nja zao za uovu.
 
Back
Top Bottom