Kila siku tunalia ajali za barabarani zimezidi mno na zinamaliza watanzania wengi. Kuanza kwa mfumo wa leseni mpya za udereva kulilenga kupunguza ajali hizo. Mapema mwaka huu JK alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa waandamizi wa polisi mjini Moshi aliwaagiza wapunguze tatizo la kuongezeka kwa ajali za barabarani kabla halijawa janga la kitaifa. Lakini kilichopo ni kwamba; sasa leseni mpya za udereva zinatolewa kama njugu na hao hao Polisi wa kwa kushirikiana na baadhi ya watu wa TRA. Wakaguzi wa magari, na wakuu wa usalama barabarani katika baadhi ya Mikoa wanajua na wanahusika. Kwa mfano Leseni ya udereva daraja ABDE inatolewa kwa sh. 250,000 hadi 300,000/- kwa mtu ambaye hajawahi kabisa kuwa na leseni ya aina yoyote. Hakuna cha kufanyiwa test. Maana yake ni kwamba hata mtu ambaye si dereva kabisa anaweza kupata leseni. Leseni hii ni kwa ajili ya pikipiki, magari madogo na makubwa isipokuwa ya abiria.
Kwa upande wa leseni daraja C1, C2 hizi zinatolewa kwa sh. 400,000/- na watu wanamiminika kuzichukua. Vyeti vya VETA pia vinaghushiwa kwa kushirikiana na Polisi hao hao kwa malengo ya mhusika kupata leseni ya madaraja hayo. Kibaya zaidi wakaguzi hao wa magari wanadaiwa kupeleka return kwa baadhi ya vigogo wa Polisi Makao Makuu. Hapa maana yake nini? Hivi Polisi kwa nini wameamua kuwa wanyama kiasi hiki dhidi ya raia? Hapa ajali zitapungua au ndiyo zitazidi kutumaliza kutokana na baadhi ya watu kupata leseni na kuendesha magari yakiwemo ya abiria ilhali hawana ujuzi wala sifa za kazi hiyo? Usalama wa Taifa wako wapi? IGP hajui haya?, JK hajui haya? Au mpaka nani apate ajali kutokana na madereva wenye leseni za aina hii ndio wachukue hatua?