Polisi wanapohusishwa na ujambazi dhidi ya Wabunge serikali haipaswi kukaa kimya

Hili swala si dogo kama linavyoonekana na wengi. Nadhani ipelekwe hoja bungeni ili iundwe tume ya uchunguzi (ya bunge). Au iundwe tume huru ya uchunguzi (ya mahakama).
Hili suala la kutumia polisi hata sehemu wanapotuhumiwa wao si sahihi kabisa, tulishalisema wakati wa mauaji ya 05 January huko Arusha na kwenye sakata la Mwakyembe, lakin kinachoonekana ni business as usual
 
Ni masikitiko yangu makubwa kwa hali kama hii ambayo wanaofanyiwa ni watanzania, ila kwa vile wako upinzani. Hivi Tanzania ni nani, nijuavyo mimi Tanzania ni ya raia wote bila kujali awe wa chama chochote cha siasa. Tunakopelekwa na ccm siko, ccm wanatuandalia maafa ambayo haitasaulika katika historia ya Tanzania. Mpaka sasa ccm hawajakubali mabadiliko ccm inaona wale wote wanaojiunga na vyama ni adui yao na wanataka awe adui wa kila mtanzania. Wakati anaeonwa ni adui nae ni mtanzania. Ccm wanatuletea utengano katika Tanzania kwa tamaa yao ya madaraka. Najiuliza/nauliza hivi angekuwa wabunge wa ccm ndio wamecharazwa mapanga hao jamaa siwangekuwa ndani. Inawezekanaje Wanachama wa chadema zaidi ya 70 Arumeru juzi wamepigwa mabomu na kusekwa ndani kisa kuponda gari la kigogo wa ccm lakini waheshimiwa wabunge wa upinzani wamekatwa mapanga wakiwapo polisi lakini mpaka sasa hakuna aliekamatwa hata mmoja. hivi leo chadema wachukue nchi hawa watawala wanaofanya ivi si ndio watasababisha kulipizana kisasi.
 
Jeshi la Polisi limekuwa likitumika kisiasa zaidi kuliko tunavyodhani. Viongozi wake karibu wote ni CCM damu japo kuwa maadili hayaruhud. Ndiyo maana hata majuzi kamanda Tobias Andengenye alikpokuwa akihojiwa alisema Chama Cha Demokrasia na Maandamano akikusudia CDM!!!!!!

Kamanda huyu huyu alishawahi kutuhumiwa na wafuasi wa CDM kwa kuwaambia ni mapanya, alitoa amri ya kusema hebu ondoeni mapanya haya hapa mahakamani!!!!!

Lema nae alishawahi kumwambia kuwa ni lazima kesi ya ubunge imtie kidole!!!! Hiyo ni mifano ya viongozi wetu wa jeshi la polisi walivyojisahau na kuona wapinzani si watu na hawaamini na watu hali ya kuwa wananchi wamewapa dhamana.
 
Mzee mwanakijiji una maana gani na heading yako? Usiseme polisi wanapohusishwa na ujambazi, polisi hawahusishwi bali ni majambazi katika hili maana walisimamia kwa makini zoezi hili la kujeruhi hawa watu. Hii ina maana serikali ni majambazi; sasa una maanisha majambazi wasikae kimya? Jambazi unataka aseme nini wakati yeye tayari kajeruhi na lengo lake ilikuwa kuua, au unataka jambazi (serikali) avunje ukimya na kusema amekosea kidogo angeua kabisa.
 
Wangekuwa wabunge wa ccm wangetoa karipio kali na kutishia wananchi na tuhuma nyingi zingeelekezwa kwa vyama vya upinzani kuwa wanatishia amani ya nchi na wanataka kusababisha vurugu
 
Lengo lao ilikuwa wafe sijui ili serikali iitishe uchaguzi mdogo!
Sasa kama mbunge anapigwa na watu huku polisi analisimamia ilo zoezi sasa kwa Mtanzania wa kawaida itakuwaje?
Ama kweli mtetezi wa Tz alishakufa kuna haja ya kuibua mwingine.
This can only be done kwa kupeleka one of the oppossition party magogoni ile CCM wajue hawana hati miliki na hii nchi
 
Mimi naona ugaidi huu unaofanywa na polisi ni maelekezo mahsusi toka kwa mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ndiye amiri jeshi mkuu.Ukimya wa JK(Janga la Kitaifa) kwa vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na wana CCM chini ya usimamizi wa polisi ni ushahidi wa kuwa amebariki vitendo hivi.
 
Mmh, basi hatuna pa kukimbilia tena.
kama vyombo vya dola vinaanza kutumika hivi, inabidi tutafakati na kuchukua hatua kama taifa.
 
Yale mafunzo yanayotolewa pale CCP yatakuwa na walakini.
Askari wanafundishwa roho mbaya badala ya kufunzwa namna ya kukabili uhalifu.
 
Ni miaka michache tu iliyopita mambo kama haya tuliyaona Rwanda ambapo majeshi tawala yalihusika au kubariki raia kukatwa katwa na mapanga. Mimi naona kwa mtindo huu wa Mwanza, Tanzania sasa ndipo tunakolelekea huko. Lakini nawaonya wanaobariki vitendo hivyo vya kiovu: ni kawaida kwa uovu kushindwa na iko siku watajibu mbele ya mahakama zote (duniani na ahera) kuhusu matendo yao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom