Polisi wampa kibano dully sykes

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Askari wa jeshi la polisi nchini wamempa kibano staa wa bongo freva, Abdul Sykes'Dully Sykes'.
Dully, alivuka mataa wakati askari wa usalama barabarani walikuwa wamezuia magari kupita ili kupisha msafara wa kiongozi mmoja wa kitaifa, hivyo kuibua timbwili zito kati yake na mamwela.
Mwendo aliovuka nao Dully barabarani, uliibua hisia kuwa mwanamuziki huyo ama alikuwa jambazi au haramia aliyetaka kufanya jambo baya kwa kiongozi huyo (jina tunalo).
Tukio hilo, lilitokea Jumamosi iliyopita, Barabara ya Mandela kwenye mataa ya Chang'ombe, Dar es Salaam.
Polisi wakitumia pikipiki mbili na gari aina ya Land Rover Defender, walilikimbiza gari la Dully na kufanikiwa kulizingira kabla halijafika mbali.
Gari la Dully lilikuwa na vioo vyenye weusi wa kukolea (tinted), kwa hiyo polisi walipolizingira, walikoki bunduki zao kwa ajili ya kulishambulia kama angefanya ukorofi wowote.
"Bahati nzuri baada ya kuzingirwa alizima gari, akafungua mlango na kutoka akiwa ameinua mikono juu," alisema mtoa habari wetu na kuongeza: "Baadhi ya askari walimgundua ni Dully lakini walimuweka chini ya ulinzi."
Baadaye polisi walimpeleka Dully Kituo cha Polisi Chang'ombe.

E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Unafahamu maana ya kibano mkuu!!??....

Nafahamu sana, ndio maana hata mimi nashangaa kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni kuwe ndio kibano. Those are just normal police procedures.

Niliposoma hii thread nilijua jamaa kapata kipondo cha nguvu!
Ndio maana ya kibano
 
mmh wabongo bna hvi mnajua maana ya kibano mbna con ata kofi moja kabgwa???achen kuuza habar ziczo za msng
 
Back
Top Bottom