Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Ni kujisahau, kujiamini au nini? Hivi polisi wamezionyesha silaha walizokutwa nazo waanadamanaji wa Chadema kusapoti uhalali wao (wa polisi) kutumia risasi za moto dhidi yao?
Polisi wetu wamewahi kufanya hivyo huko nyuma:
Mwaka 1998 katika vurugu za Mwembechai Polisi walionyesha kwa waandishi wa habari silaha walisodai zilizokutwa kwa waandamanaji au zilizotupwa katika maeneo ya vurugu kuonyosha kwamba polisi ilibidi kutumia risasi za moto kuwaua waanadamanji wanne. Silaha hizo zilikuwa ni mvisu, mawe, miti ya bendera n.k.
Mwaka 2001 katika mauaji ya makumi ya wana-CUF kule Pemba, polisi walionyesha silaha walizodai zilikutwa kwa baadhi ya waandamanaji au kuzitupa kwenye maeneo ya vurugu. Silaha zilikuwa ni mapanga, mawe, fimbo, viberiti n.k.
Katika matukio yote hayo mawili hakukuwepo silaha zozote za moto kama vile bunduki au bastola. Swali ni vipi huko Arusha polisi hawakuja na kitu kama hicho kutilia nguvu hoja yao ya ulazima wa kuuwa kwa kutumia risasi? Walisahau?