Polisi wakubali mashujaa wa HAKI kupewa HESHIMA za mwisho viwanja vya NMC kesho!!

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Wilaya wa CHADEMA Arusha ni kwamba polisi 'wamekubali' ibada pamoja na duwa kuwaaga mashujaa waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi tarehe 5-01-2011 ifanyike kesho jumatano kwenye viwanja vya NMC Arusha. Taarifa rasmi za ratiba ya ibada na dua zitaendelea kutolewa ili kila mwenye nia ya kushiriki aweze kushiriki!
 
Kama ni kweli tunashukuru. Tunaamini redio ya EL (5) itatangaza kuwahabarisha wakazi wa Arusha ili wenye mapenzi mema washiriki.
 
Hapo poa kama ni kweli. Ila utulivu ni muhimu kisije kikatokea kisingizio.
Nahisi kama IGP atakuja na taarifa za kiitelejesia usiku!
 
Mungu mkubwa, tukawaage mashujaa wetu, Naomba wanachadema tusiwashambulie polisi ili waweze kupata sababu ya kutokea, mungu yupo malipo huwa ni hapa hapa duniani, nawamba sana wapiganaji wetu arusha tuoneshe ukomavu na ustahimilivu wa hali ya juu ili tuweze kuwa prove wrong polisi na mafisadi wa CCM
 
Taarifa za kiintelijensia feki ya polisi huwa zinakuja jioni
 
Mmewadanganya marehemu kuwa wao ni mashujaa, hakuna mashujaa ambao wanakufa kwa kugombea kupewa kiti cha umeya.
 
Tuungane kuwaaga mashujaa wetu kwa amani na utulivu mkubwa,hakuna haja ya kuwashambulia polisi wauaji wa raia,damu ya mashujaa iko mikononi mwa polisi mashetani hao na serikali yao,ila malipo ni hapa hapa chini ya jua,na muda si mrefu they will pay for what they did!R.I.P Mashujaa wa kweli
 
Taarifa kutoka kwa Katibu wa Wilaya wa CHADEMA Arusha ni kwamba polisi 'wamekubali' ibada pamoja na duwa kuwaaga mashujaa waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi tarehe 5-01-2011 ifanyike kesho jumatano kwenye viwanja vya NMC Arusha. Taarifa rasmi za ratiba ya ibada na dua zitaendelea kutolewa ili kila mwenye nia ya kushiriki aweze kushiriki!

Safi sana, Wananchi wa Arusha kwa Ujumla tunaomba muhudhurie, sisi wa mbali tuko pamoja kuwaombea dua marehemu wote.
 
1. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 2. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. 3. Hunihuisha nafsi yangu; na kunio­ngoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa ma­baya; kwa maana wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji. 5. Waandaa meza mbele yangu, ma­choni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika. 6. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyu­mbani mwa Bwana milele. (ZAB 23:1-6)
 
no retreat no surrender... almighty god rest their soul in eternal peace...., and let hope and strength cherish for those who lost their loved ones..amen..amen..amen
 
Back
Top Bottom