Polisi wafunga baadhi ya barabara mjini moshi kuzuia wananchi kusikiliza kikao cha madiwani

mndeme

JF-Expert Member
Sep 2, 2008
323
57
Kuna mdau kanipasha kuwa kwa sasa polisi wa mjini moshi wametanda mji mzima na wamefunga baadhi ya barabara ili kuwazuia wananchi wasihudhurie kwenye ukumbi wa halmashauri kusikiliza kikao cha madiwani kinachoendelea.

Pia mkurugenzi amekimbia ukumbini akihofia ile hoja ya kuchukua viwanja vya wazi vilivyomilikishwa kwa cc.

Je polisi ni mali ya chama tawala?

Sipati majibu ni lini tutakuwa na demokrasia ya ukweli hapa tz.
 
mijizi yote hii yaani polisi watasema wamepata habari za ki itelijensia kuwa kuna umwagaji mkubwa na uvunjifu wa amani utatokea ....
 
Ufisadi uliofanywa na ccm wakati wanaongoza halmashauri unawapa shida. Waligawana viwanja vya mji kwa wingi wao kwenye baraza sasa cdm ni wengi na wanampango wa kuyafuta maamuzi ya kifisadi waliyofanya. Wanaogopa wananchi wasisikilize huo mjadala. Nawashauri madiwani warekodi hata kwenye simu halafu waje watuhabarishe. Haya yatafika mwisho tu!
 
Mh Jafari Meya mpambanaji usirudi nyuma mafisadi ni wengi pambana kamanda 2po pamoja Kamanda Hawa najua hapo kazi tuu msiwaonee huruma Wafisadi.
 
Back
Top Bottom