Polisi wafufua kitengo cha kuchunguza uhalifu mtandaoni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
JESHI la Polisi limeunda timu ya kuchunguza matukio ya uhalifu kwa njia ya mitandao, simu za mikononi, ATM za mabenki na huduma nyingine za mitandao cha Ant cyber crime Unity ili waweze kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu.
Hatua hiyo, imekuja baada ya kutokea matukio ya wizi katika ATM za benki, wananchi kutumiana ujumbe wa matusi kupitia mtandao na simu za mikononi na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, (DCI) Robert Manumba alisema matukio hayo, yameibuka nchini hivi karibuni na kusababisha baadhi ya wananchi kupata matatizo.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu, na kusababisha upotevu wa fedha.
Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo litawashughulikia wananchi wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo, kinyume na taratibu.
“Kuna baadhi ya wananchi wanatumia mitandao vibaya, baadhi ya wanatumia ili waweze kuwatukana wenzao, wengine kuiba na kusababisha malalamiko mengi kutokea,” lisema Manumba.
Alisema timu hiyo, itahakikisha wanaofanya vitendo hivyo, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Manumba alisema hivi sasa wanaboresha timu hiyo ili iweze kufanya kazi na kwamba anaamini mpango huo, utafanikiwa.
Alisema timu hiyo, ilikuwepo muda mrefu, lakini ilishindwa kufanya kazi kwa sababu matukio ya wizi kwa kutumia mitandao, haikuwepo.
Wakati huo huo, Manumba alisema hivi sasa wanakichunguza chama cha kiislamu kinachojishughulisha na kutetea haki na maslahi ya waislamu nchini.
“Kuna baadhi ya kundi la watu linalojishughulisha na masuala ya siasa ndani ya dini, jambo ambalo linaweza kusababisha mvutano kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, tunatakichunguza kwanza ili tuweze kubaini undani wake na kazi wanazozifanya na ikabainika wamekiuka taratibu, watachukuliwa hatua za kisheria,”alisema.
mwananchi

http://www.mzalendo.net/polisi-wafufua-kitengo-cha-kuchunguza-uhalifu-mtandaoni
 
Je, wanayo rasilimali watu / wataalamu wa kuhimili cyber crimes? Je, sheria zetu nazo zinaendana na wakati kuhusu hili suala la cyber crimes? au ziko 'kimya'?
 
kwakweli inabidi jeshi letu lijipange si kusubiri kuua watu na kusema majambaizi waingie na kwenye wizi wa mitandaoni sasa
 
Ni kitu kizuri sana kwa watanzania, lakini nina maswali kidogo
kwa kusema jeshi linafufua, ina maana hicho kitengo kilikufa?
Je kama kipo, kina vitendea kazi vya kutosha
Na kama vipo, je walikuwa wapi? ina maana hawakujiandaa?
Ninategemea jeshi letu ni preventive, kwa hiyo kusikia linaanzisha kutokana na wimbi fulani, hii inanitatiza!!
 
Back
Top Bottom