Polisi wadai Dr Slaa alikuwa na bunduki

Slaa Daktari wa Kanoni, Padri mstaafu wa Kanisa Katoliki, mara tuu baada ya kugunduwa kuwa wamezingirwa na Polisi, alichopoka kijaasusi na kujificha ndani ya gari. Baadhi ya vijana ambao ni macho na masikio ya ziada ya polisi waliojichanganya na wakeshaji, wakawatonya makachero waliovamia hapo alfajiri kuwa "Slaa yupo kwenye gari lile pale".

Mwenyewe Slaa kwa uzoefu wake wa kijasusi, alijuwa ame "save" inasemekana alikutwa kakilaza kiti cha gari ki "James Bond" ili asionekane. Vijana hawakuzugika na inasemekana waliufunguwa mlango huo wa gari kimaajabu, na ndipo Slaa akatoka huku kaweka mikono kichwani, kukaguliwa haraka haraka akakutwa na bastola “Walther Pistol T2-CAR-61074-327963” ambayo mpaka sasa inashikiliwa na polisi kuthibitishwa kama alikuwa anaimiliki kihalali.

Nakupa heko Slaa kwa ukomando, lakini kumbuka, miaka imekutupa mkono, ujasusi wako ilikuwa zamani, sasa kuna vijana hao sio kawaida.

MSAGAJI on duty
 
Ukatili wa jeshi la polisi kwa raia pamoja na vitendo vya ubaguzi katika kusimamia sheria kama linalivyolalamikiwa jeshi la polisi la Tanzania ni moja ya mambo makubwa yanayochangia na kuichonganisha serikali ya CCM na wananchi. Ukatili wa polisi kwa raia haswa kwa wafuasi wa chadema unaofanywa na jeshi la polisi la Tanzania sidhani kama unaridhaa na serikali na chama chake. Ingawa ukimya wa serikali na kutokukemea ukatili huo kunatia hofu na mara nyingine kuonyesha kuwa inawezekana kabisa kuwa ukatili huo unaridhaa ya serikali. Hata hivyo njia pekee ya kukomesha ukatili wa polisi kwa raia ni kubadilisha katiba ili polisi atakaye tenda makosa hayo awajibishwe yeye kama mtu na si kama jeshi la polisi ama chombo cha dola mpaka pale tuu atakapothibitisha kwamba ukatili huo ulitendwa kwa ridhaa ya dola ama serikali. Leo hii Major Ali aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya ameshtakiwa the Hague yeye kama Ali kwa matendo yake na amri alizozitoa yeye na si kama muwakilishi wa serikali wakati wa vurugu za kiraia kufuatia utata katika matokeo ya uchaguzi mwaka 2007 nchini Kenya.


Jambo jingine kubwa linalofanya Jeshi la polis Tanzania liendelee na ukatili kwa raia ni ukimya wa Tume ya Haki za Binaadamu Tanzania. Na ukimya huu unatokana na ukweli wa kwamba Tume yetu ya Haki za binaadamu haiko huru kwasababu inawajibika kwa dola na si kwa raia. Tume huru ya Haki za Binaadamu Kenya ni moja wa vyombo vichache ambavyo ndiyo vimeweza kuweka bayana na kutoa ushahidi wa ukatili wa polisi kwa raia na ukiukwaji wa haki za binaadamu na jeshi la polis la Kenya. Tume huru ya Haki za binaadamu hufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo yake huru bila kuingiliwa na vyombo vya dola. Nii Mabadiliko huru ya katiba ndiyo yatakayotoa tume huru ya haki za binaadamu na kukomesha ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na jeshi la polisi la Tanzania. Kwa masikitiko makubwa uwezekano huu wa tume huru ya haki za binaaadamu na ukomeshwaji wa ukatili kwa raia na ukiukwaji wa haki za binaadamu na polisi wa Tanzania hautakoma kwani mswaada wa sheria ya kubadilisha katiba uliotolewa karibuni umeziba kabisa matumani hayo kwa kuendelea kujaza mamlaka ya kuteua tume ya kusimamia mchakato wa katiba mikononi mwa mhimili mmoja wa dola yaani rais. Kwa mantiki hii mswaada huu utapitishwa na rais atatumia mamalaka yake yaliyo makubwa kupita kipimo kuteua wale ambao wataendeleza aian na muundo waserikali ambao utaendeleza utaratibu uliopo wa vyombo vya jeshi la polisi kuwajibika kwa rais na siyo kwa wananchi. Kweli inasikitisha kuona kuwa pamoja na kelele zote za waTanzania ofisi ya mwanasheria wa serikali wa Tanzania ambayo imepewa nafasi ya kuwanusuru waTanzania kuingia katika janga la vurugu imeamua kupuuzia matakwa ya kuimarisha demokrasia na amani na kutoa muswaada ambao kweli matokeoa yake itaitumbukiza nchi hii katika hali mbaya sana na wala si mbali.

Kwamba yaliyopo kwenye mswaada wa Sheria ya Kubadilisha katiba yanawasilisha matakwa ya Rais siamini ni kweli kwasababu leo hii Rais wa Tanzania Mrisho Kiwete anasifika Kenya kwamba yeye ndiyo aliyeinuusuru Kenya isirudi kwenye mapigano pale alipomshurutisha Mwanasheria Mkuu wa kenya Amosi Wako atoe ushauri utakao inusuru Kenya kutoka kwenye machufuko. Raisi Kikwete mbele ya wajumbe wa ODM and PNU alimwambia wako toa ushauri utakaokufanya ukumbukwe katika historia na siyo ule utakaomfurahisha mtu mmoja. Hata wako alipotaka kuomba fursa azungumze na aliyemteua yaani Rais Kibaki Mhe. Kikwete alimtolea macho na kumwambia tena Amos huna nafasi hiyo je unafikiri katiba ibadilishwe iweke kipengele cha serikali ya shiriikisho ama la? Amos alifuata busara ya Jakya Mrisho Kiwkete na akasema ndiyo lazima hilo lifanyike. Kweli kama Mtanzania ninajivunia Rais wangu Kikwete kuingia kwenye historia ya dunia kuwa alitoa uongozi mahali ambapo wengine walishindwa na aliinusuru Kenya kwenye vita mbaya sana ya wenyewe kwa wenyewe. hii ni taarifa niliipata kwenye simuzlizi za Amos Wako siku yake ywa mwisho ofisini kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kenya. Ni kwa simulizi hii ya Amos Wako mimi binafsi siamini kuwa Mwanasheria Wetu Mkuu wa Serikali ametoa mswaada huu kutokana na maagizo ya Rais Wangu ambaye aliweza kuwasaidia wa kenya kupata mabadiliko ya sheria kuiruhusu Kenya iwe ni serikali ya uwakilishi na ya mpito kusimamia mabadiliko ya katiba yatakayoipa kenya demokrasia ya kweli.
 
Polisi mkoani Arusha wanadai kuwa baadhi ya wana-CHADEMA waliokuwa kwenye Mkesha wa NMC jumatatu usiku walikuwa na silaha za moto.

Kaimu Kamanda, Akili Mpwapwa amesema kuwa Dr Wilbroad Slaa alikutwa na Bastola "Walther Pistol T2-CAR-61074-327963" wakati alipokamatwa na Bwana Daniel Ezekiel Ogongo ambaye pia alikamatwa kwenye tukio hilo akidaiwa kuwa na 'Pietro Beretta H-447577 CAT5802'

Cha kushangaza ni kwamba wakati Polisi ikiwaburuza mahakamani wafuasi wa CHADEMA wale wanachama wa CCM ambao wiki kadhaa zilizopita walikutwa na kosa hilo hilo la kuandamana na kufanya mikutano bila kibali mjini Arusha ‘wamesamehewa' na kupewa ‘onyo kali!'

Polisi wamekiri kuwa pamoja na kwamba wakeshaji pale NMC walikuwa hawajajiandaa na walipovamiwa walikuwa tayari wamechoka kwa kuimba usiku kucha, bila chakula na kwenye mvua na baridi kali bado wasingeweza kuwadhibiti na hivyo kulazimika kutumia magari nane pamoja na lile lori lenye maji ya kuwasha.

Na haikuwa rahisi pia, pamoja na zana zote hizo.

Kama wana akili wangetakiwa kujua kuwa hakika hali inaenda kuwa mbaya.

kama hizi?
attachment.php
attachment.php

p99_2.jpg 300px-Walther_P99_9x19mm.png 1287739695.jpg
attachment.php
 
Nahoji tu unapopewa bastola unatakiwa umwachie mkeo akushikie AMA ni kwa ulinzi wako binafsi? Hakuna kesi hapa ni sifa za kijinga tu.
 
Mwananchi kutembea na silaha ni udhaifu wa jeshi la polisi kutoa ulinzi wa uhakika.
Kabla ya kumkamata wanapashwa wajihoji wenyewe kwa nini wananchi wameamua kujilinda wenyewe.
 
walitegemea figure kubwa kama slaa atakosa bastola ya kujihami?mbona Rage hawakutaja ni aina gani wala kuweka no zake magazetini?polisi waache kushiriki propaganda za ccm
 
Suala la silaha si la msingi hapa unless kama Dr. Slaa anaimiliki kinyume na sheria. Nakubaliana na wanaJFM wote waliosema kama risasi haijafyatuliwa hakuna kosa na pia hatujasikia kwamba kulikuwa na mapambano kati ya Dr. Slaa na polisi kwa maana ya kukataa kuwekwa chini ya ulinzi. Tatizo hapa ni polisi na hasa kamanda wa polisi wa wilaya ambaye haheshimu watu na kitendo chake cha kuonyesha bunduki alizodai ni za viongozi wa Chadema kinaonyesha kwamba mashtaka anayodai kutendwa na Slaa na wenzake ni ya kubambikia na ndiyo maana hakuthubutu kusema umiliki wa Dr. Slaa na mwenzake wa bunduki walizokamatwa nazo si halali. Acha waendelee lakini laiti wangejaliwa kujua ukweli kwamba inawezekana kuwaweka watu gerezani lakini "UKWELI HAUWEKWI GEREZANI and the truth will always prevail it is just a matter of time and justice will prevail. Mwisho naomba niwakumbushe maafisa wa polisi wanaokubali kutumiwa na wakubwa kama vile Bw. Zuberi kuwafanyia watu ubaya wajue kwamba wao wanakaa mtaani na siku moja raia watawahukumu. Wao ndio watakaosulibiwa ilhali wakubwa waliowatumia wakikaa salama na kulindwa kwa kodi ya Watanzania. Demokrasia ina gharama na wanaoitamani wako tayari kulipia gharama ya kuipata. Magereza kamwe hayataweza kuinyamazisha nguvu ya UMMA!
 
Binafsi kama Mtanzania, Mama na ninayeipenda nchi yangu namuomba Rais wangu Jakaya Mrisho Kikwete kama ambavyo alikwenda kinyume na hilla ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria na Katiba ya kukataa mabadiliko ya katiba Tanzania, aende kinyume na hila hizo na aingilia kati swala la muswaada wa kutunga katiba mpya Tanzania, akubali mapendekezo ya wananchi wa Tanzania wa kutaka tume huru. Kwa wale ambao tunalalamikia mamlaka makubwa aliyoewa rais katika kuteua Tume ya kusimamia mchakato siyo kwamba tunamchukia Rais Kikwete la hasha. Lakini tunasema huu ni wakati muafaka wa kupunguza mamlaka ya Rais ili wananchi waweze kushiriki kuchagua watu watakao simamia mchakato huo. Ni ukweli usiopingika na si kwa Tanzania tuu hali ya binaadamu inamfanya mtu apoteze uhuru wake na awajibike kwa aliyemteua. Kwamba mamlaka aliyopewa Rais wa Tanzania ni makubwa mno ni ukweli usiopingika na hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliliona hivyo. Tunashukuru Tanzania kuwa marais wetu hawajawahi yatumia mamlaka hayo kiukatili na kufanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu. Lakini tukiacha hali hii anaweza tokea Rais mmoja akaamua kufanya ukatili wa ajabu na tukajuta. Kama ambavyo Rais Obama aliwakusema huko nyuma Afrika iache kutegemea hisani na huruma za watu na viongozi lakini ijijengee miundo demokrasia na taasisi zinazosimamia demokrasia ya kweli. Kudai tume huru ya kusimamia mabadiliko ya katiba ni moja ya njia ya kujenga mifumo na taasisi imara za kujenga mifumo na taasisi indelevu kwa ajili ya maendeleo ya watu na ustawi wa jamii
 
Polisi mkoani Arusha wanadai kuwa baadhi ya wana-CHADEMA waliokuwa kwenye Mkesha wa NMC jumatatu usiku walikuwa na silaha za moto.

Kaimu Kamanda, Akili Mpwapwa amesema kuwa Dr Wilbroad Slaa alikutwa na Bastola “Walther Pistol T2-CAR-61074-327963” wakati alipokamatwa na Bwana Daniel Ezekiel Ogongo ambaye pia alikamatwa kwenye tukio hilo akidaiwa kuwa na ‘Pietro Beretta H-447577 CAT5802’

Cha kushangaza ni kwamba wakati Polisi ikiwaburuza mahakamani wafuasi wa CHADEMA wale wanachama wa CCM ambao wiki kadhaa zilizopita walikutwa na kosa hilo hilo la kuandamana na kufanya mikutano bila kibali mjini Arusha ‘wamesamehewa’ na kupewa ‘onyo kali!’

Polisi wamekiri kuwa pamoja na kwamba wakeshaji pale NMC walikuwa hawajajiandaa na walipovamiwa walikuwa tayari wamechoka kwa kuimba usiku kucha, bila chakula na kwenye mvua na baridi kali bado wasingeweza kuwadhibiti na hivyo kulazimika kutumia magari nane pamoja na lile lori lenye maji ya kuwasha.

Na haikuwa rahisi pia, pamoja na zana zote hizo.

Kama wana akili wangetakiwa kujua kuwa hakika hali inaenda kuwa mbaya.
..........ndio uvivu wa kutumia akili unapojitokeza hapa, kwani kukutwa na pistol ni dhambi/kosa? suala hapa ni kwamba hiyo pistol inamilikiwa kihalali/kisheria au la, jambo ambalo hata yule Mpwampwa au whatever they him hakutolea ufafanuzi, najua ni kwa makusudi kwa kujuia watz wengi tunakurupuka kimasaburi saburi
 
Kumiliki bunduki mbona ni kitu cha kawaida sana hasa kwa mtu ambaye ni public figure kama dr. slaa. Kitu cha msingi awe anamiliki kihalali slaha hiyo....Jambo la kumuhoji kwa nini alienda na silaha kwenye mkusanyiko kama ule halina mshiko kwa sababu hata ismail aden rage alienda na silaha kwenye mkusanyiko wa kampeni igunga.
 
Kumiliki bunduki mbona ni kitu cha kawaida sana hasa kwa mtu ambaye ni public figure kama dr. slaa. Kitu cha msingi awe anamiliki kihalali slaha hiyo....Jambo la kumuhoji kwa nini alienda na silaha kwenye mkusanyiko kama ule halina mshiko kwa sababu hata ismail aden rage alienda na silaha kwenye mkusanyiko wa kampeni igunga.
Mkutano ule ulkuwa halali. Wa NMC ulikuwa siyo wa halal baada ya jua kuchwea.
Halafu anakataa kuhusu uchochezi, sijui polisi hawaangalii alichopost kwenye Facebook?
 
Kamanda MBOWE mbona alisepa na kuteleza kama kambale tofauti na kauli zake za nguvu pepoooooooooooooo pawa, Binafsi nilidhani angeonyesha ukakamavu kwa wafuasi wake kwa kubaki uwanjani mpaka akamatwe

aliogopa virungu vya polisi.
 
Faiza Foxy una element za udini na najua ndo unavyofundishwa ubaguzi na viongozi wako wa kimwili na ki................. mbungu isahau[/QUOTE

Faiza kaahaidiwa pepo na wanaume arobaini walioshiba kama shwarzenigger siku akijilipua! Kaa nae mbali!
 
Nini cha ajabu hapa, au kwa vile Dr. Slaa ni CHADEMA. Mbona kuweka silaha kiounoni kwenye mikutano ni kawaida tu Bongo. Mbona Rage kule Igunga haikuwa issue kuwa na pistol kwenye mkutano wa Hadhara.

Acheni ujinga nyie POLICCM.

Ha ha haaaa! You have just given me a new name: 'Policcm'
 
Hii habari ni sumu humu JF sasa hivi Mods wataitoa waichanganye na thread zingine...

Dr Slaa risasi 17 unakwenda vitani?

Rage alikuwa vitani? Bastola bila risasi ni sawa na rungu!
 
MAGAMBA Wote masaburi yenu hee mungu tupe NGUVU ya kuwang'oa hawa panya wezi majambazi wakubwa ! Maluhuni. Shwaini.
 
Sasa tatizo ninini kama anazimiliki kihalali? Mimi nilifikiri walipompekua walimkuta na kichwa cha m-k-w-e-r-e!, Shame upon you POLICM
 
Napata wasiwasi Padre mstaafu kutembea na Bastola mbili, je sisi kondoo wake tutatembea na nini?

Nashaka na Mbowe ndio maana kakimbia inawezekana alikuwa AK-47
 
Back
Top Bottom