Polisi wa mizani, wanaomba rushwa haoo!

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
522
331
Nimekodi gari napeleka mzigo wangu kwa wanyalukolo kutoka dar. Kama kawaida ya magari ya mizigo,dar tumetoka usiku. Kufika kibaha mizani tukasimamishwa na polisi mmoja(hana sare ya trafic) umri wake ni kama miaka 25,dereva alipomsalimia akamwambia sasa, nipe chochote! Dereva mchaga, akamwambia hali ngumu. Aliangalia gari,akaturuhusu. Tulipofika mikese mida ya saa tisa usiku jumapili tukasimamishwa na polisi mwingine(hana sare ya trafic) umri wake kama miaka 28. Akamwambia dereva nipe kadi ya gari, dereva akajadiliana na kiongozi wake wa msafara,tumpe ngapi? Dogo akasema sina chenji(ule mtindo bado unatumika).dereva akampatia kadi tupu, yule polisi alizunguka gari akiangalia cha kukamata akakosa. Mara akauliza, wapi FIRST AID? Wakatoa ile kit wakampa, maskini kumbe kulikuwa hamna plaster! Akatuambia pakini gari pale.... Tukamsubiri kama dk 10 hakutokea, madogo ikabidi wamalizane naye kiaina na tukaondoka. Hivi kwani lazima kila anayepita akupe hela? Au mnapewa kiwango cha kukusanya? Pambaf sana.!
 
Tumefika moro kituo cha ukaguzi saa 10 usiku tukasimamishwa tena. Kama kawaida, kadi madogo wakaweka na buku mbili. Yule polisi hakuridhika, akatuambia kasimame pale. Bahati nzuri katokea trafic akauliza kwani lina kosa gani? Ikawa ndo pona yetu,tukachukua kadi huyooo.... Tunakaribia mikumi.
 
Rushwa kwa askari wetu ndio tatizo je ungepita njia kuelekea Dom si ndo ungelia kuna askari kila mita mia,ukifika DUMILA ndo basi,kuna vitu vingi vya kukagua lakini ukiwa una hela unaweza kupita hata kama gari halina BIMA wanaangalia nini anapata
 
wale jamaa kama hujazidisha mzigo hawaombi rushwa. hakikisha gari unayo kodi imekidhi vigezo vya kuwa barabarani otherwise kila beria utatoa buku tano.
 
Rushwa kwa askari wetu ndio tatizo je ungepita njia kuelekea Dom si ndo ungelia kuna askari kila mita mia,ukifika DUMILA ndo basi,kuna vitu vingi vya kukagua lakini ukiwa una hela unaweza kupita hata kama gari halina BIMA wanaangalia nini anapata
 
Rushwa kwa askari wetu ndio tatizo je ungepita njia kuelekea Dom si ndo ungelia kuna askari kila mita mia,ukifika DUMILA ndo basi,kuna vitu vingi vya kukagua lakini ukiwa una hela unaweza kupita hata kama gari halina BIMA wanaangalia nini anapata

.
Ndio maana yake. Ukiwa mtaalamu wa kuuza lugha police unawalambisha buku buku tu ukiiambatanisha na kadi ya gari. Maisha yanaenda, masaa yanasonga na kesho inakuja. Kibongo bongo tutafika tu.
.
 
sasa unacholalamika ni nini wakati hata kadi ya gari ulikua hauna? ingekua nchi za nje hapo mngelaza gari kituoni msubiri mahakamani....
 
Back
Top Bottom