Polisi wa Madagascar waua waandamanaji 23

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Polisi wa Madagascar wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 23 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 80 wakati walipokuwa wakiandamana kuelekea ikulu kumpinga rais Marc Ravalomanana wa Madagascar.

318.jpg


316.jpg


317.jpg


source: www.nifahamishe.com
 
Rais Marc Ravalomanana alipokuwa Meya wa Antananarivo naye aliwahi kuongoza maandamano kama haya. Wanaua watu 23, kweli viongozi wetu wa kiafrika hutunza uongozi wao kwa njia yoyote. Manake watu wakirushiwa tu mabomu ya machozi ama maji hukimbia, sasa nguvu zote hizi mpaka kutumia risasi za moto za nini?. Pole kwa wafiwa.
 
huu ni unyama unaotokana na ulevi wa madaraka. Mauaji kama haya hayakubaliki kabisa katika jamii iliyostaarabika. Ni lazima sheria zinazolinda haki za binadamu/raia ziwe na meno ya kutosha ya kuwatafuna hata viongozi wauaji.
 
Kuna nini tena huku?

Sasa huko Ukulu walikuwa wanaenda kulalamika? Au kutaka ajiuzulu?

AU summit Julai imepangwa Madagaska..je itawezekana?

SADC region kuna tatizo gani?
 
Viongozi wetu Africa hawajali kabisa maisha ya watu wa kawaida....Maandamano hayo hayakupaswa kuvunjwa kwa kutumia ngumu kubwa ya namna hii.......Rabsha yote imetokana na kutokuelewana kati ya Mayor wa Antananarivo na Rais wa Nchi hiyo ya Madagascar,Tofauti ya mitazamo yao kuhusu hali ya Uchumi ya Jiji la Antananarivo imepelekea vifo vya watu wasio na hatia!!
 
Most Africans hate Americans and other developed nations but I luv them as when it comes to national democracy really they leavy things happen the way they are. I dont get astonished as I know the same had happened and gonna happen in Tanzania in 2010 and may be onwards.
 
Back
Top Bottom