Polisi Tunisia wajiunga na wanachi kuandamana mitaani kupinga serikali

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Jamani,
Mmeipata hiyo? Nimesikia kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku leo. Hivi polisi wa kibongo wanayasikia hayo?
 
safi sana!unakumbuka kuna askari pale benki ya akiba kinondoni alikaa lindo siku 3 mfululizo mpaka akaibiwa silaha.sasa polisi kama huyo ana haja gani ya utawala wa ccm?
 
Jamani,
Mmeipata hiyo? Nimesikia kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku leo. Hivi polisi wa kibongo wanayasikia hayo?

polisi bongo wanaiogopa sana serikali na ndio maana huwa wanaajili watu wenye elimu za chini kwa sababu wanakua waoga sana kwamba wakipoteza ajira hawatoipata tena ndio maana wanakua watiifu kwa serikali
 
Mkubwa kwa kichapo hiki cha maisha, wapende wasipende watajiunga tu na raia... maisha bongo yamekuwa ka tushaingia jehanam!!!:A S-fire1:
 
Haya maisha magumu hata polisi nao yanawapata. Ipo siku watajua kuwa serikali ya CCM inawaibia na wataungana na raia kudai haki yao.
 
Wajinga tu hao. Wameona wameishiwa risasi za moto. Sisyemu, agizeni risasi nyingi ili polisi waiishiwe, vinginevyo mtakyona cha mot pia
 
Hata siku moja Polisi wa TZ hawawezi kujiunga na kuleta mageuzi kwa sababu wanapokea rushwa ile mbaya na kipato wanachopata kupitia rushwa ni kikubwa kuliko mshahara wao wa halali! hivyo watakuwa wajinga kushiriki ktk kuleta mabadiliko! kwani mabadiliko yakija inamaana kutakuwa na utawala wa sheria na hivyo mianya ya rushwa kuzibika na wao kupoteza kipato!
 
Ukweli Jeshi la polisi Tanzania limejengwa kupitia orders na fear to low rank officers. Wananchi tuchunguze jinsi gani malipo ya mishahara, nyumba na maisha kiasi gani yana waumiza polisi na Jeshi la Tanzania. Ukiangalia mishahara ya maofisa wa chini walio wengi (98%) ni 80,000 kwa mwezi na maofisa wa juu walio teuliwa na Kikwete (kwa Katiba ya CCM) ni average of 1,000,000 kwa mwezi. Sasa figure out Kikwete amuagope nani hapa, Jk anaweza kuwadhibiti hao maofisa wa juu lakini huku chini no. Tukiangalia hata upigaji kura JK akupata kura nyingi kutoka kwa Jeshi la polisi na Jeshi la Wananchi. Kinacho subiriwa ni pressure kidogo tu, wanajeshi wote wata wageuka kama mchanga...
 
safi sana!unakumbuka kuna askari pale benki ya akiba kinondoni alikaa lindo siku 3 mfululizo mpaka akaibiwa silaha.sasa polisi kama huyo ana haja gani ya utawala wa ccm?

Sasa polisi wa benki ya Akiba ana uhusiano gani na utawala wa CCM? Naamini kuwa watu wanaropoka tu kuonekana ant CCM. Mnapoteza kabisa maana halisi ya upinzani.
 
Back
Top Bottom