Polisi tanzania mnajua utawala wa haki na sheria?

fredmlay

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
1,849
388
Hivi nikweli kwamba utawala bora na wa haki unapatikana Tanzania? Hivi ni kweli waliopewa zamana ya kuhakikisha utawala wa sheria na haki unafuatwa wanatekeleza majukumu yao?

Nakumbuka siku ambayo Mh. Ole Sendeka Mbunge wa Simanjiro aliposhinda kesi yake dhidi ya James Millya wapenzi wake wengi walijitokeza na kuandamana kwa msururu mrefu toka mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Arusha, maandamano yaliyoishia katika baa ya moivo kwa mashabiki na wapenzi wake kujipongeza kwa kula nyama choma, mji wa Arusha kwakweli ulizizima, haikuwa siri kila pembe ya mji ilijua kuna tukio muhimu limetokea, lakini la kushangaza ni hivi juzi tu Mh. Godbless Lema Mbunge wa Arusha alikuwa akitokea mahakama kuu kanda ya Arusha kwenye kesi inayo mkabili, kwakuwa katika kesi hiyo washitakiwa walikuwa wengi Mh. Lema aliamua kutembea kwa miguu kuelekea ofisini kwake, cha ajabu wakiwa wamebakiza mita chache kufika zilipo ofisi za mbunge polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya wananchi, sasa wadau mimi nachanganyikiwa hivi utawala bora hapo ni upi? je sheria yaweza kuvunjwa ilimradi tu CCM (mwana CCM) wanafanya mambo yao?

Sipendi tabia hiyo tena nasema polisi jirekebisheni la sivyo mtakuja juta siku moja, hiyo staili yenu ya kulipua mabomu ovyo inawakomaza wananchi na siku moja hawatajali hata kama yatakuwa yanaua, busara zitumike kulijenga taifa letu, hatutaki ya Tunisia, Misri na Libya yatukie hapa, amani hewa (kwakuwa wengi wanalala njaa hivyo basi hawana amani) tuliyonayo msiivuruge, niukweli usiopingika kwamba wavunja amani Tanzania ni jeshi la polisi, iko siku mtajuta nyie polisi kwa tabia yenu hiyo
 
Back
Top Bottom