Polisi tafuten wauwaji acheni kudanganya umma

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
HUU NI UTAPELI WA KIJINSIA
WALIOMUA HUYU MAMA WAALA SI HAWA POLISI WASIUE WATU WENGINE KUKOSHA WAMEUA MAJAMBAZI NASEMA HILI NIKIWA ARUSHA KILA AKISHANGAA HAO WATU WANAODAIWA KUUWAWA;POLISI TAFUTEN WAUWAJI ACHENI POROJO

POLISI mkoani hapa imewaua kwa risasi watuhumiwa wawili wa ujambazi wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mke wa mchimbaji madini ya tanzanite, Jacqueline Minja (2 yaliyotokea Jumanne usiku.

Jacqueline ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi minane aliuawa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake na watu wawili wakati akisubiri kufunguliwa lango hilo katika eneo la Lemara mjini hapa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Basilio Matei, aliwataja waliouawa katika mapambano ya silaha na polisi kuwa ni Gilbert Charles (32) mkazi wa Kijenge na Deus ‘Dosaa' ambaye anadaiwa kuwa mkazi wa Lemara jirani na nyumbani kwa marehemu.

"Watuhumiwa hao walikufa kutokana na majeraha waliyopata waliporushiana risasi na polisi eneo la Kaloleni jana (juzi) saa 12 jioni na wote walifariki dunia baadaye wakati wakipelekwa hospitalini kwa matibabu," alisema Matei.

Alisema siku ya tukio, polisi wa doria waliokuwa wakifuatilia nyendo za watuhumiwa hao, walikutana Kaloleni wakiwa na pikipiki aina CCXL namba T 522 ARB.

"Walipowaona polisi walikimbia kasi na kuwafyatulia risasi polisi ambao walijibu mapigo na walipoona wanazidiwa nguvu, walitelekeza pikipiki na kukimbilia ndani ya nyumba ambayo bado haijamalizika kujengwa," alisema.

Alieleza kuwa watu hao waliendelea kupambana na polisi wakiwa ndani ya nyumba hiyo kwa nusu saa ambapo polisi walilazimika kuongeza nguvu kutoka kwa wenzao wa kituo kikuu na kuwadhibiti muda mfupi baadaye.

Kamanda alisema baada ya kudhibitiwa, watu hao walikutwa na bastola aina ya Beretta ikiwa na risasi sita na ilibainika kuwa silaha hiyo ndiyo iliyotumika katika mauaji ya Jacqueline baada ya wataalamu wa milipuko wa Jeshi hilo kuoanisha risasi za bastola hiyo na ganda la risasi lililokutwa ndani ya gari la marehemu.

"Tuna uhakika wa asilimia 100 kuwa watu hao ndio wahusika wa mauaji ya Jacqueline kutokana na sababu mbili; kwanza, ni risasi na silaha iliyotumika na pili, hata mlinzi aliyefungua geti baada ya kuona picha zao alikiri kuwa ni wenyewe," alisema.

Alisema uchunguzi wa awali wa Polisi uligundua kuwa mtuhumiwa Charles aliachiwa kutoka jela mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kumaliza kifungo cha wizi wa kutumia silaha na mwenzake Deus, alitoka jela mwaka juzi baada kuachiwa huru akiwa amefungwa kwa makosa ya uporaji na wizi wa kutumia nguvu," alisema.

"Rekodi zao zinaonesha kuwa wote ni wahalifu sugu, lakini sisi bado tunafanya uchunguzi kujua sababu hasa ya kumuua mjamzito huyo, kwani mara nyingi majambazi wana tabia ya kupata fedha kwanza, kabla ya kufanya mauaji," alisema.

Hata hivyo, wakati Kamanda akitoa taarifa hizo, habari zilizopatikana baadaye jana mchana kutoka kwa ndugu wa marehemu, zilibainisha kuwa Deus alikuwa anaishi mtaa mmoja na Jacqueline na walikuwa wakifahamiana.

Ndugu huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alidai kuwa baada ya kumwuliza Jacqueline aliko mumewe na yeye kujibu kuwa hajui, mtuhumiwa alimpiga risasi iliyompata kwenye paji la uso na kupora simu ya mkononi na funguo za gari.

Alidai kuwa baada kumpiga risasi mwenzake alisikika akihoji sababu za kumuua na ilitokea hali ya kutoelewana baina yao na inavyoelekea, wakati anafanya kitendo hicho, mtuhumiwa huyo alikuwa katika hali ya ulevi.

"Kuna uwezekano kuwa baada ya kuona kuwa Jacqueline amemtambua akaamua kumuua … lakini sisi tumesema tuwaachie polisi wamalizie upelelezi wao," alisema ndugu huyo.

Mume wa marehemu, Deogratius Minja, akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili alieleza kuwa alikuwa Marangu na wanafanya taratibu za mazishi nyumbani kwao Marangu, kesho.
 
Back
Top Bottom