SAKATA la ushuru wa kuku limeendelea kuchukua sura mpya,baada ya mfanyabiashara wa kuku 'kutekwa' na askari polisi sita na kupelekwa kwenye vichaka vilivyopo kando kando ya bwawa la Kindai nje kidogo ya mji wa Singida na kutishiwa kuawa kwa kupigwa risasi.
Mfanyabiashara huyo Ayubu Yussuph (28)amedai kuwa baada ya kufikisshwa kwenye eneo hilo la vichaka,aliteremshwa kutoka kwenye gari na kisha alikandamizwa na mdomo wa bunduki shingoni na kuamriwa kuvua shati na suruali.
Mfanyabiashara huyo ,Ayubu alisema siku ya tukio desemba mbili saa 4.00 asubuhi alikamatwa na askari hao akiwa nje ya mahakama ya Utemini walikokswenda kuwawekea dhamana wafanyabiashara wenzao.
Alisema akiwa na kaka yake mahakamani hapo.askari trafiki kwa jina anaitwa Eliudi alimwendea na kumwambia kuwa,jana yake alishiriki kumpiga na kumchania shati.
"Basi baada ya kunitupia lawama za uwongo, alinichukua na kuniambia kuwa ananipeleka kituo cha kati cha polisi kwa ajili ya kunifungulia mashitaka.Trafiki huyo akiwa na polisi wengine watano, walinipandisha kwenye gari lao na badala ya kunipeleka kituoni,walielekeza gari lao barabara ya kuelekea bwawa la Kindai",alisema.
Ayubu alisema walipofika Kindai,walimteremsha chini na kisha kumwingiza kwenye kichaka na kumkandamiza shingoni kwa mdomo wa bunduki. Polisi mwingine naye alimkandamiza kwa bundiki kwenye makalio yake, jirani na sehemu ya kutolea haja kubwa.
Mfanyabiashara huyo wa kuku za kienyeji,alisema kipindi chote hicho,alipambana nao vikali baada ya kubaini kuwa walitaka kumwingilia kimwili kinyume na maumbile kabla ya kumuuwa.
"Baada ya kuhangaishana nao kwa muda mrefu,askari hao walienda kuchota maji bwawani na kisha kunimwagia mwilini mwangu na wakaniambia eti tukifika kituoni,nieleze kuwa nimekamatwa ndani ya bwawa la Kindai baada ya kuwatoroka",
Tunaendelea kumtafuta RPC au RCO ili aeleze kinagaubaga suala hili tutawajuza wana JF kila kinachojiri. Hili ndio Jeshi la Usalama wa raia na mali zao.