Kwa issue ya DC na mtandio wake kule Igunga, Nape na Makamba waliiita waandishi wa habari huku Makamba akishikilia gazeti lenye picha ya DC aliyeshiliwa na wanaume (wafuasi wa CHADEMA) na akatoa wito,'akina mama na wanaharakati wa haki za binadamu,mama huyu kashikwa na wanaume,huu ni udhalilishaji,kemeeni hili'. Tusubiri tuone labda makamba au Nape watatoa tena wito kulaani kitendo hiki cha polisi wanaume kumbeba juu juu huyu mama wa Igunga wakimshika makalio nk, vinginevyo tutawaona ni wale wale mafisadi vijana wanaotaka CCM ibaki madarakani kwa njia haramu(mchezo wa DC wa Igunga) ili waendelee kuneemeka na ufisadi unaofanywa na CCM.