Polisi na mauaji ya kinyama Kigoma

Hizi adhabu huwa zinatolewa hata mitaani na Raia wanapokamata hata mwizi wa "kufuli" tu. Hakuna cha ajabu hapo.

kupiga mwizi mitaani ni tofauti na Polisi wanapomkamata mtuhumiwa, Kazi ya Polisi ni kusimamia Sheria sio kuvunja sheria. Unabowa sana siku hizi dada yangu
 
Nilifikiri una mwona mpana lakini katika comment hii umepwaya mno.
Watu wa mitaani wengi wao ni wale wasiojua sheria ndio maana wanajichukulia sheria mkononi na ni jukumu letu na vyombo vya dola kuwaelimisha maana ya kufuata sheria ili mahakama ifanye kazi yake juu ya watuhumuiwa.

Kwa mtazamo wako unahalalisha polisi kuhukumu mtuhumiwa bila kufikishwa kwenye mahakama kadiri sheria inavyotaka kinyume cha miiko na mafunzo yao ya utendaji kazini?
Hawa polisi wamefunzwa taratibu zote hizo, kwamba wao ni walinzi wa wananchi na kuhakikisha sheria zinafuatwa na si kuhukumu na kufanya mambo kinyume cha haki za binadamu kama watu wasiostaarabika, sasa wananchi watakapoendeleza ubabe wa kujichukulia sheria watajitetea kwamba polisi ndio wanaowafunza na pengine kumalizia hasira juu ya unyama huu.

Na kitendo cha udhalilishaji wa kuingiza vijiti kwenye haja kubwa mbele ya wananchi na familia na wazazi wakishuhudia ukatili huo jambo hili haliwezi kutetea kwa jinsi unavyofanya. UCCM unawaharibu watu hata kutoa comment ambazo ni za kiitikadi badala ya kisheria.

Huo ni ukweli na hakuna aupingae, ikiwa Polisi wanashindwa kuzuia Raia anapoweza kuua mwizi hata wa kuiba kufuli, unategemea huyo polisi yukoje?
 
kupiga mwizi mitaani ni tofauti na Polisi wanapomkamata mtuhumiwa, Kazi ya Polisi ni kusimamia Sheria sio kuvunja sheria. Unabowa sana siku hizi dada yangu

Kazi ya Polisi ni nyingi sana, na mojawapo ni kukamata watu na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, hiyo pia ni kazi ya Raia yoyote mwema, kwanini iwe makubwa kwa Polisi na iwe madogo kwa Raia anayeuwa Raia mwenzake? Jee, Raia wanaouwa wapo juu ya sheria? halafu soma vizuri hiyo makala "ofisi ya kata walimfungia chumbani", toka lini ofisi za kata zimepewa majukumu ya kufungia watu?

Tatizo lenu mkiona jina la FF huwa hamsomi hata anachokiandika huwa mnakurupuka, someni mpate faida.
 
Hivi Da FAIZA FOXY wewe ni binadamu wa kawaida kweli!!!!??
Nahofia sasa huenda JF hata majini yanatoa comment!!!!!!!

Naona badala ya kuzisoma hoja zangu unataka kujuwa uhalisia wangu, unahusu nini? Soma vizuri hoja zangu, labda utanielewa.

Sasa nataka ujiulize swali moja, hujawahi kuona watoto wadogo wanatishiwa "kama haujala tutakuitia Polisi" jiulize kwanini inafikia kama hivyo kwa walinda usalama?
 
Policcm wamekosa vita wanaamua kumaliza raia, hizi damu za watz zinazomwagika kila siku itaigarim ccm na police. Namwomba Mungu awaumbue katika hili
 
huyo si ni kada wa CCM, Chama Cha Makatili!!

Mimi ni Mwanachama wa CCM lakini hainizuii kumshutumu yeyote kila afanyapo sivyo. Na hapa naongelea kwanini iwe ajabu kwa polisi tu? wakati hata Raia huwa wanafanya hivyo hivyo tena si kwa mtu kutuhumiwa ujambazi, kwa mtu kutuhumiwa kuiba "kufuli" tu. Naomba fikiri mantiki ya kauli yangu kabla hujanisulubu.
 
kwa hiyo raia huwaadhibu wezi wa makufuli kwa kuwapiga na vitako vya bunduki, kuwaingiza mijiti kwenye njia ya haja kubwa na kuwakwangua wezi hao tumboni kwa chupa?
Je raia wanapata wapi vitako vya bunduki?
 
Hizi adhabu huwa zinatolewa hata mitaani na Raia wanapokamata hata mwizi wa "kufuli" tu. Hakuna cha ajabu hapo.

Wewe tayari uko adkited na payroll ya magambo na dhamira yako imeshakufa kabisa unapaswa kuwaona wataalamu wa mambo ya kiroho(spiritual directors) usaidiwe
 
Labda hizo bunduki ndiyo hawana, tuongee "realistically", lakini hayo majiti ya huko nyuma, mipira ya shingo mpaka inawashwa moto, matofali, mapanga, mawe, chupa, ni mambo ya kawaida kabisa anapokamatwa mwizi mitaani. Hilo halina ubishi.
 
Wewe tayari uko adkited na payroll ya magambo na dhamira yako imeshakufa kabisa unapaswa kuwaona wataalamu wa mambo ya kiroho(spiritual directors) usaidiwe

Nakuambia badala ya kunishambulia mimi, shambulia hoja zangu, Jee, Raia hawaui wizi mitaani? hujasikia? hujaona au unajifanya punguani?
 
Naomba sana mnielewe naona mpka sasa mnanirushia shutuma na kunishambulia mimi binafsi, hakuna mahala nimeunga mkono hili la polisi kuuwa na au kutesa, si ubinaadam na kazi yao ilikuwa ni kuchunguza kumpeleka mtuhumiwa mahakamani akahukumiwe.

Nnachosemama mimi ni kuwa hata Raia huwa wanafanya mateso na hadi mauaji kwa wizi hata wa "kufuli" tu na Polisi hawawafanyi lolote hawa Raia wauaji, hawaedeshi uchunguzi wala hatujasikia kushikwa mtu kwa mauaji, Jee, katika hali kama hiyo mnategemea nini kutoka Polisi? mimi sitegemei zaidi wala sioni ajabu ya hawa Polisi kuyafanya waliyoyafanya. Ikiwa Raia wanafanya na kila kitu shwari, utegemee nini kutoka Polisi?
 
Msiihusishe CCM na unyama wa Polisi au wa Raia wanapotesa au kuuwa, CCM haijawatuma kuuwa, sheria zipo wazi kama hawazifati ni hao Polisi na si CCM hao Raia wanaouwa mitaani anapokamatwa mwizi huwa wa chama kipi?
 
Hizi adhabu huwa zinatolewa hata mitaani na Raia wanapokamata hata mwizi wa "kufuli" tu. Hakuna cha ajabu hapo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Rungwe Mpya, Mosi Kilenge, alisema: "Mimi nimesikitishwa sana na kifo cha Festo kwani ni mchapa kazi sana hapa kijijini, hakuwa mlevi wala jambazi,

Wewe Mama kweli una roho mbaya!

Duuh!
 
Ni kweli kabisa kuwa haya mambo ya polisi ni ya kawaida kabisa bongo...

Kisutu polisi pale penyewe ukiingia tu reception pale ni damu zimetapakaa kwnye sakafu...

Pia haitakiwi mtuhumiwa apelekwe pale kama havuji damu ama hajapigwa...

Polisi wanpigiwa kelele na mabosi wao kama wakipeleka wananchi watuhumiwa wakiwa wazima!

Ukienda pale kituoni kisutu,utashangazwa sana,hutaamini kama nchi ina utawala wa Kidemokrasia!
 
Wewe Mama kweli una roho mbaya!

Duuh!

hakuna roho mbaya wala nzuri hapo, kuna ukweli usiopingika, Jee, Raia hawauwi wizi mitaani? mbona hamuelewi hata kusoma na mnashindwa kupinga hoja zangu mnanivaa binafsi, nimeweka mpaka link hapo juu, za Raia wanaojichukulia hatua mikoni mwao na hakuna aonae kuwa ni ajabu. Vipi, kuwe na double standards? ikiwa polisi wanashindwa kulinda haki ya mtuhumiwa wa wizi mitaani mpaka anauliwa, wataweza kusimamia haki ya mtuhumiwa wa ujambazi mikononi mwao? hapo sasa! Tuwe wa kweli.
 
hakuna ukatili, Jee, Raia hawauwi wizi mitaani? mbona hamuelewi hata kusoma na mnashindwa kupinga hoja zangu mnanivaa binafsi, nimeweka mpaka link hapo juu, za Raia wanaojichukulia hatua mikoni mwao na hakuna aonae kuwa ni ajabu. Vipi, kuwe na double standards? ikiwa polisi wanashindwa kulinda haki ya mtuhumiwa wa wizi mitaani mpaka anauliwa, wataweza kusimamia haki ya mtuhumiwa wa ujambazi mikononi mwao? hapo sasa! Tuwe wa kweli.
nimesikitishwa sana na kifo cha Festo kwani ni mchapa kazi sana hapa kijijini, hakuwa mlevi wala jambazi
Bado tu huelewi?

Ama unajfanya hamnazo?
 
Labda hizo bunduki ndiyo hawana, tuongee "realistically", lakini hayo majiti ya huko nyuma, mipira ya shingo mpaka inawashwa moto, matofali, mapanga, mawe, chupa, ni mambo ya kawaida kabisa anapokamatwa mwizi mitaani. Hilo halina ubishi.

tunawalalamikia polisi kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kulinda usalama wa mali zetu na uhai wetu pia.
Kama polisi wanatuua na kutuangamiza, je tukimbilie wapi?
 
Back
Top Bottom