Polisi na kauli ya kijinga......

Baada ya IGP Mwema aliyekuwa interpol kabla ya uteuzi uliomweka hapo alipo kuanza ungunguri badala ya kutumia uzoefu wa interpol nikajua tu polisi hamna kitu tena, hivyo sishangai kusikia kauli zao kama wanasiasa uchwara. Hakuna professionalism bali ni kutishana na kuwekana ndani kama walivyokuwa wakifanya polisi wa mkoloni. We ukiona Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (kachero mkuu) naye anatumia mtindo wa kukamata watu na kuwaweka ndani kusaidia upelelezi ujue ni maguvu mtupu na hakuna weledi wa kikachero hapo na kwa lugha nyingine huo ni uvunjaji wa haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom