Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Najua vurugu za Arusha au Mauaji ya Arusha yamejadiliwa sana. Pande mbili zimejitokeza.
1. Kama polisi wangeruhusu maandamano na kutoa ulinzi vurugu zisingetokea. Demokrasia ingekuwa imeheshimiwa. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuzuia maandamano. Polisi walichelewa kutoa taarifa na njia iliyotumika kufikisha taarifa haikuwa sahihi. Polisi walitumia nguvu kubwa kuzuia maandamano. Polisi walitembea na waandamanaji mpaka eneo la kwa Dr. Mohamed umbali wa km zaidi ya 2 ndipo wakaanza kuwatawanya wananchi. Polisi walipiga mabomu uwanjani katikati bila sababu. Polisi walichochea vurugu.
2. CHADEMA walikaidi agizo la polisi. Hakukuwa na sababu za kuandamana. CDM wasingepoteza chochote kama wangeenda uwanjani moja kwa moja. CDM walichochea vurugu kwa kulazimisha maandamano.
Kumekuwa na jitihada za kuweka 'ukweli' hadharani. Polisi wako busy na DVD yao. CDM wamesema watajibu mapigo na kutoa ya kwao. Matamko yametolewa kila moja na ujumbe wake. Kwa wanaoshutumu CDM hawathubutu kuisifia polisi. Wanasema polisi wana haki ya kulinda kituo lakini hawasemi waziwazi kama wana haki ya kuua, kupiga watu na kutoa taarifa za uongo kuhusu uvunjifu wa amani.
Wanaosema CDM wameonewa hawasemi kama CDM wana haki ya kulazimisha maandamano yakizuiliwa na polisi. Hawasemi kama haki ikinyimwa unaidai kwa nguvu. Hawasemi kama mtu akiwekwa kizuizini kwa uonevu ni haki kwenda kumtoa kwa nguvu.
Swali linabaki, kuku na yai kipi kilianza? Polisi na CDM nani alianzisha vurugu?
Vurugu zilianza wakati wa maandamano au baada ya mkutano? Risasi zilipigwa wakati gani? Waliopigwa risasi uwanjani na Jogoo house walikuwa wanaenda kuteka kituo? Josephine aliyepasuka kichwa kwa kupigwa na kitako cha bunduki na kuwekwa lock up saa tano asbh alikuwa anaenda kuteka kituo? Dereva wa Grace Kiwelu MB aliyetenguliwa kiuno alikuwa anaenda kuteka kituo? Mtui Katibu wa Freeman Mbowe aliyepigwa mpaka akazimia akaachwa chini sakafuni polisi kwa zaidi ya masaa 8 alikuwa anaenda kuteka kituo kipi? Mtoto wa miaka 14 alikuwa anateka kituo? Kijana aliyepigwa St Thomas Hosp risasi mbili za miguuni na kuporwa sh mil 2.7 alikuwa anaenda kuteka kituo?
CDM hawakuangalia TV kusikia maelekezo ya IGP? Viongozi hawakuona umuhimu wa kushauriana na polisi asubuhi mapema na kuwaeleza nia yao ya kuandamana kwa amani? Walionana na RPC kumwambia kwamba wanaonewa kunyimwa kuandamana na hivyo wataendelea na mpango wao?
Tukirudi kwa Polisi je wametoa taarifa nyumba ya Salim Ally ilichomwa na nani na kwa kutumia nini? Na je sio bomu lililovunja kioo na kuingia ndani ndio chanzo cha moto?
Nini kifanyike hali ile isijirudie tena? Kauli ya JK kwamba haitarudia haitoshi. Imerudia Mbarali, itarudia UDOM, itarudia wakati wa malipo ya Dowans!! WanaJF nini kifanyike? Great thinkers wanashauri nini?